TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, September 23, 2013

MOTO WA MSWADA WA KATIBA WAHAMIA VISIWANI ZANZIBAR

Posted: 23 Sep 2013 01:58 AM PDT

Na Mwajuma Juma, Zanzibar


  Chama cha Wananchi (CUF) kimemtaka Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, kujiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kusimamia maslahi ya Zanzibar.  Kauli hiyo ilitolewa mjini Zanzibar jana na Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF, Ismail Chusa Razu, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibanda Maiti. Alisema Balozi Seif amegeuka dalali wa kuiuza Zanzibar baada ya kukiri kuwa Zanzibar ilishirikishwa katika Mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Muungano katika kipengele kinachohusu Zanzibar, jambo ambalo sio kweli. 

Aliongeza kuwa, Balozi Seif akiwa kiongozi alistahili kuzungumza na Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Mwanasheria Mkuu ndipo apate cha kuzungumza."Namtaka Balozi Seif ajiuzulu nafasi yake kwa kushindwa kusimamia maslahi ya Zanzibar, ikiwa ana uchungu wa Zanzibar hakustahili kusema hivyo," alisema na kuongeza kuwa kuanzia sasa watakuwa wakimuita Balozi Mkazi wa Tanganyika na Zanzibar.Kwa upande wa kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru,kusema anashangaa wazee wenzake kuleta rasimu ya Serikali tatu wakati Serikali mbili zilizopo kila moja ina mipaka yake na Zanzibar na bara zilikufa mwaka 1964 wakati nchi mbili zilipoungana,Chusa alisema Zanzibar bado ipo hai na itaendelea kuwa hai hadi kiama.

  Alisema iliyokufa ni Tanganyika hivyo kama lengo ni kuizika Zanzibar bado hawajafanikiwa kwani Wazanzibari wapo macho."Zanzibar ipo hai na itaendelea kuwa hai hadi kiama, nchi hii haijazikwa," alisisitiza.  Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad, alimtaka Rais Jakaya Kikwete, asisaini mswada huo, kwani ana nia nzuri, lakini wenzake wanataka kumpeleka kubaya. "Rais Kikwete ana nia nzuri lakini wenzako wanakupotosha, usisaini mswada huu tunajua una nia nzuri,"alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa iwapo atakubali kusaini mswada huo atazuia wajumbe wa chama hicho wasishiriki Bunge la Katiba.

  Alishauri mswada huo urejeshwe Zanzibar ili kupata Katiba Bora. Kuhusu Balozi Seif, Maalim Seif alisema anamuonea huruma makamu mwenzake huyo kwa sababu hakujua ni mswada upi aliuona.
Alisema Mei 6, mwaka huu aliitwa Dodoma na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kuambiwa kuwa wanataka kufanya marekebisho kwenye vipengele sita ambapo walifanya marekebisho, lakini waliporudi Tanzania Bara walifanya marekebisho kwenye vipengele nane.
Alisema makamu wake hakujua hilo na anashangaa ni kwa nini wana-CCM wenzake wamemtosa. Alisema bila shaka walikuwa wamepanga jambo hilo.Alisema Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar, Mwanasheria Mkuu, Rais wa Zanzibar na yeye mwenyewe hawakubaliani na hilo.

MAMA AUA MWANAYE MCHANGA

Posted: 23 Sep 2013 02:11 AM PDT


 Na Elizabeth Joseph, Dodoma

   Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Cecilia Laurent (28) mkazi wa Uhindini mkoani Dodoma ambaye ni mhudumu wa baa na nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama CDA Club mkoani hapa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake mchanga.     Akielezea tukio hilo jana Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Mary Motto alisema kuwa mwanamke huyo alipokelewa majira ya saa 8 usiku ambapo pia hakuwa na kadi ya kliniki jambo ambalo lilidhihirisha kuwa hajahudhuria kliniki tangu kushika ujauzito huo, lakini walimpokea.  

   “Cecilia alifika hapa saa 8 usiku, bila ya kadi ya kliniki na ilipofika majira ya saa 9 usiku alienda chooni na kujifungua mtoto wa kiume, bila kutoa taarifa kwa wauguzi na baada ya kujifungua akamsukumiza mtoto katika tundu la choo kisha akafungua bomba la maji ili kukisukuma kiumbe (kuflash) jambo ambalo lilishindikana kutokana na tundu la choo hicho kuwa dogo kupitisha kiumbe hicho," alidai Muuguzi huyo.   

     Mmoja kati ya mashuhuda waliokuwa wodini hapo aliyejitambulisha kwa jina la Nyamizi Muhosi alisema kuwa, wakati akiwa bafuni anafua alimuona mwanamke huyo akianza kuzaa akiwa kachuchumaa kwenye tundu la choo, ndipo alipomkataza na kumwambia awaite wauguzi jambo ambalo hakulisikiliza.  “Nilikuwa bafuni nafua. huyo Cecilia alikuja chooni nikaona mtoto kashaanza kutoka nikamwambia awaite wauguzi wa zamu, lakini alikataa na kuendelea kuzaa mwenyewe bila kusaidiwa kisha akakisukumiza kichwa cha mtoto wake katika tundu la choo na kufungulia maji (kuflash) ili kuzidi kumsukuma, halafu akaanza kupiga kelele akidai mtoto wake kadumbukia chooni kwa bahati mbaya, jambo ambalo si la kweli,”alisema Muhosi. 

   Shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mary Chihuma alidai kuwa, mwanamke huyo alidhamiria kuua mtoto wake, kwani tangu alipofika wodini hapo alikuwa akijigonga kwa makusudi katika vitanda vya wagonjwa wengine, lakini walipomuhoji kwa nini anafanya hivyo hakuwajibu kitu.Mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Juma Alikanda alikemea kitendo hicho na kusema kuwa si cha kiungwana na kama hali ya maisha yake ni ngumu haikumpasa kuchukua maamuzi hayo na kuitaka serikali kuchukua hatua za kisheria ili kukomesha tatizo hilo.
   Kwa mujibu wa mfanyakazi mwezake na mtuhumiwa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa akiongopa kuhusu miezi ya mimba yake kwa kutaja miezi tofauti tofauti ambapo hata shangazi yake alikuja hivi karibuni kwa ajili ya kumuangalia, lakini mtuhumiwa huyo alimjibu mimba ni ya miezi minne jambo lililomfanya shangazi huyo kurudi kijijini kwao Usandawe Kondoa mkoani hapa. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Upelelezi mkoani humo, ASP Damas Nyanda alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa kichanga hicho umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Rufaa mkoani hapa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

AZAM FC 'YAINYUNYIZIA LAMBALAMBA

  • '
 Na Elizabeth Mayemba

   Azam FC  waliifunga Yanga mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.     Mpira ulianza kwa kasi ambapo Azam walipata bao la kwanza dakika ya kwanza lililowekwa kimiani na John Bocco kwa kichwa akiunganisha krosi iliyochongwa na Brian Umony. Azam walifuata tena lango la Yanga dakika ya tano, Humphrey Mieno akiwa na kipa Ally Mustafa 'Berthez' alipiga shuti lililotoka nje ya lango. Yanga ilizinduka dakika ya tisa ambapo, Didier Kavumbagu alipata nafasi nzuri ya kufunga lakini shuti lake likatoka nje ya lango.  Dakika ya kumi, Jerry Tegete aliachia shuti kali lililogonga mwamba na kurudi uwanjani ambapo mabeki wa Azam wakaokoa.

  Yanga waliendelea kulibana lango la Azam na kulitia kashikashi ambapo dakika ya 12, Mbuyu Twite alipiga shuti kali mpira wa faulo lakini kipa akapangua na kumkuta Kavumbagu alipiga nje ya lango.  Twite nusura angeipatia Yanga bao dakika ya 43, baada ya kuachia shuti kali akiwa nje ya 18 lakini mpira ukagonga mwamba na kutoka nje.  Yanga waliibana Azam kwa kiasi kikubwa na kuwafanya kurudi nyuma kulinda lango lao na kuwapa nafasi wapinzani wao kufanya mashambulizi kila mara.Kipindi cha pili dakika ya 49, Kavumbagu aliipatia Yanga bao baada ya kupewa pasi ndefu na Haruna Niyonzima na kuukwamisha mpira wavuni.

Dakika ya 59, Hamis Kiiza aliyechukua nafasi ya Tegete akiwa na kipa, alipiga shuti kali lililookolewa na kipa.Kiiza alirekebisha makosa yake dakika ya 65 baada ya kuipatia Yanga bao la pili baada ya kupokea pasi ya Simon Msuva.Dakika ya 69, Kipre Tchetche aliisawazishia Azam bao la pili kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Yanga Kelvin Yondan kuunawa mpira katika eneo la hatari.Azam ilipata bao la tatu dakika ya 90 kupitia kwa Joseph Kimwaga baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Tchetche.













KIVUMBI

Posted: 22 Sep 2013 11:14 PM PDT .

Wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa vya upinzani, wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubaliana na matamko ya viongozi wa vyama hivyo, wakati wa mkutano wa kupinga kupitishwa kwa mswada wa Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika kwenyeViwanja vya Jangwani Dar es Salaam jana.

  • Wapinzani wampa JK mtihani ndani ya wiki mbili
  • Askofu Kakobe nae amtaka asisaini mswada
  • Maandamano nchi nzima yanukia iwapo utapita
 Anneth Kagenda na Salim Nyomolelo
   Viongozi wa Vyama vya Siasa vya upinzani wamempa Rais Jakaya Kikwete, muda wa wiki mbili na nusu awe ametoa majibu kwa wananchi kama atasaini au hatasaini Mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, vinginevyo wataitisha maandamano nchi nzima ikiwa ni pamoja na kususia kuingia kwenye Bunge la Katiba    Msimamo huo ulitolewa Dar es Salaam jana kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na madhehebu ya dini. 

Akihutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema Rais Kikwete, anatakiwa awe amejibu madai yao ndani ya muda huo vinginevyo yatafanyika maandamano hayo.Mbowe alisema wataitisha maandamano hayo Oktoba 10, mwaka huu na hawataenda Polisi kuomba kibali isipokuwa watatoa taarifa kwani IGP Said Mwema ameelezwa jambo hilo.
Alisema safari hii hawatakuwa tayari kuitwa kwenda Ikulu kuzungumzia suala hilo kwa sababu hata madai yao ya awali waliyokubaliana na Rais Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam hakuna kilichofanyiwa kazi.

“Hatutakuwa tayari kwenda Ikulu kunywa chai wala juisi kwani hata makubaliano ya awali kuhusu mswada huo hakuna kilichofanyika,” alisema Mbowe. Alisema madai yao yote Rais Kikwete anayafahamu hivyo hawarudi kujadili suala hilo badala yake wanataka majibu ya madai yao.Alisema kwa sasa hatua ambazo tayari wamechukua ni kwenda kuona makundi mbalimbali ya kijamii nje ya wanasiasa ili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo kwa kuamini kuwa wananchi ndiyo msingi wa katiba.

Mbowe alisema migogoro ya ardhi inayoendelea nchini inachangiwa na Katiba, hivyo lazima ipatikane katiba ambayo itakuwa suluhisho la matatizo hayo. “Kosa kubwa kati ya makosa yote ni woga wa kudai haki, kinachotakiwa kwa sasa ni ujasiri,” alisema na kuongeza kwamba, kuwa na watu wenye woga ndiyo chanzo cha kuwa na katiba mbovu.

Mbatia
Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia, alisema katiba ni kitendo cha maridhiano na wala si cha kibabe kama CCM inavyotaka kufanya, hivyo watahakikisha inapatikana kwa gharama yoyote.Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar zinakinzana kwenye suala la madaraka ya rais. Alitoa mfano kuwa Katiba ya Zanzibar inamnyang’anya Rais wa Jamhuri ya Muungano madaraka katika suala la kuigawa nchi na hiyo inaonesha wazi kuwa kuna mgogoro wa kikatiba.

“Inabidi ieleweke kuwa, Tanzania kwanza vyama baadaye...ieleweke kuwa CCM itayeyuka lakini Tanzania itabaki,” alisema na kuongeza kwamba ieleweke wazi kwamba, nchi sasa tayari ipo kwenye mgogoro wa kikatibaAlisema katiba inatakiwa itokane na wananchi wenyewe na si kuhodhiwa na chama kimoja cha CCM na wananchi kupoteza haki ili kupata katiba bora kwa ajili ya miaka 100 ijayo.

Prof. Lipumba
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema CCM inatumia ubabe hadi ndani ya Bunge kiasi cha kufikia hatua ya wabunge wanapigwa. “Hiki ni kielelezo kuwa umefika wakati wa kuanza kufanya mazoezi ya viungo,” alisema na kuongeza kuwa tunahitaji kupata katiba inayohakikisha rasilimali za Tanzania zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote.

Aliongeza kuwa mswada uliopelekwa bungeni hauna ridhaa ya wananchi na umepitishwa kwa kuvunja katiba ya sasa ambayo inaeleza kuwa unatakiwa upitishwe na wabunge zaidi ya theluthi mbili, lakini idadi hiyo haikufika mswada ukapitishwa.Prof. Lipumba alisisitiza kuwa wananchi wa Zanzibar hawakushirikishwa kutoa maoni yao.

“Makamu wa pili wa Rais Zanzibar alidhalilishwa kwani alipigiwa simu na waziri Mkuu Mizengo Pinda, ili aende Dodoma na baada ya kufika mswada wenye vipengele 11 vimepitishwa na vitano vimeongezwa ambavyo hajawahi kuviona,” alisema Prof. Lipumba na kusisitiza kuwa; “CCM wabaya! Wanamdhalilisha hata mwana-CCM mwenzao?”

Askofu Kakobe
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, alimtaka Rais Kikwete asisaini mswada huo; na akifanya hivyo atakuwa ameshindwa mtihani mkubwa wa kitaifa kwani suala hilo lipo mikononi mwake.Alisema mwanzo alionesha njia nzuri kwa kukubali mchakato wa Katiba mpya na iwapo atasaini wataona ilikuwa danganya toto. Alisisitiza kuwa makundi ya jamii hayajashirikishwa.“Katiba ya kweli inaanza na sisi wananchi ambao ndio chimbuko la viongozi wote na 
  
Shekhe Kitimba
Naye msemaji wa Shiah ya Maimamu Shekhe Rajabu Kitimba ; “Hili la katiba ni letu, haki haiombwi na sisi tunaunga mkono viongozi wote kwa asilimia 100.”Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa pamoja na wale wa dini ambapo walitoa matamko ya kumtaka Rais Kikwete asisaini mswada huo.

SHAMBULIO LAUA WATU 22 NCHINI KENYA Posted: 22 Sep 2013 11:05 PM PDT



 NAIROBI, Kenya
  Watu 22 wanahofiwa kufariki baada ya watu wenye silaha kufyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti pia yalitumika katika shambulio hilo.

  Kwa mujibu wa Mwandishi wa BBC mjini Nairobi washambuliaji inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika. Taarifa za awali za BBC zilieleza kuwa watu sita waliuawa kwenye shambulio hilo.

  Polisi waliokuwa na silaha walizingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa walikuwa wakitolewa hapo kwa machela.Ilielezwa kuwa watu wengi walikuwa wamenasa ndani ya jengo.

  Magari yaliyoegeshwa nje ya maduka yaliharibika. Shirika la Habari la Reuters liliarifu kuwa mpiga picha mmoja aliona watu wamelala chini.Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kama kuna watu waliokamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo

MAGEUZI YA KILIMO YAMPAISHA KIKWETE

 Na Mwandishi Maalum

Rais Jakaya Kikwete, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Udaktari wa Sheria na Chuo Kikuu cha Guelph cha Toronto, Canada, kutokana na mchango wake mkubwa wa kuleta mageuzi ya kilimo nchini na Afrika kwa ujumla . Rais Kikwete alitunukiwa shahada hiyo juzi katika sherehe ya kufana iliyohudhuriwa na mamia ya wasomi wa chuo hicho wakiwemo wanafunzi na wahadhiri na Wana-jumuya ya Watanzania waishio Canada.  

Rais Kikwete ameitunuku Shahada hiyo kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania na hasa wakulima wadogo ambao wanapigana kufa kupona kuboresha maisha yao kupitia kilimo. Hiyo ni heshima ya juu kabisa ambayo Chuo Kikuu kinaweza kutoa; na Rais Kikwete anakuwa Mtanzania wa kwanza kutunukiwa Shahada hiyo katika historia ya zaidi ya miaka 100 ya Chuo hicho, maarufu kwa utafiti wa kilimo na magonjwa ya wanyama. Makamu Mkuu wa chuo hicho na Kaimu Rais wa chuo hicho, Dkt. Maureen Mancuso, alifungua rasmi Baraza la Kutunuku Shahada. 

Akieleza sababu ya kumtunuku shahada hiyo Rais Kikwete, Profesa Dkt. Kevin Hall, alisema chuo hicho kimeamua kutoa Shahada hiyo kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza, kuboresha na kuleta mageuzi katika kilimo cha Tanzania na Afrika. “Tumeshuhudia kwa namna isiyokuwa ya kawaida kabisa jinsi gani Rais Kikwete amekuwa sauti isiyochoka ya kusemea kilimo cha Afrika na kuishawishi dunia katika kusaidia kuleta mageuzi na mapinduzi ya kijani katika Bara hili muhimu sana kwa kukabiliana na changamoto zinazokabili kilimo katika Bara la Afrika,” alisema Dkt. Hall ambaye ni Makamu wa Rais wa Chuo hicho anayesimamia shughuli za utafiti.

Aliongeza kuwa kwa miongo mingi hawajashuhudia kiongozi mmoja wa Afrika akijitokeza kwa namna isiyofichika kabisa kukabiliana na changamoto zinazokabili shughuli inayoajiri watu wengi sana na ambayo ni tegemeo kubwa la maisha ya mamilioni ya watu. “Rais Kikwete tunakushukuru kwa mchango wako mkubwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo katika Afrika kupitia progamu zako kama vile Kilimo Kwanza na SACGOT,” alisema.Rais Kikwete, kama kawaida yake anapozungumzia shughuli za kilimo, ametoa hotuba ya kusisimua ambayo ilizungumzia hali ya kilimo katika Tanzania na Afrika, changamoto kuu za kilimo na hatua ambazo zinachukuliwa kukabiliana na hali hiyo.

   Akizungumzia umuhimu wa kilimo katika Tanzania, alisema kuwa asilimia 75 ya Watanzania wanaishi maeneo ya mashambani na kutegemea kilimo kwa maisha yao na kuwa hata wale wanaoishi mijini uhai wao unategemea kilimo kwa njia nyingi.  “Kilimo kinatupa chakula tunachokula, mali ghafi ya viwanda vyetu, mapato yetu ya fedha za kigeni na ajira kwa ajili ya watu wetu. Kilimo kinaingiza asilimia 25 ya Pato la Taifa, asilimia 34 ya mapato yetu ya fedha za kigeni, asilimia 95 ya chakula chetu na kinaajiri asilimia 75 ya watu wetu. Kwa ufupi basi, maendeleo ya uchumi na ustawi wetu unategemea kilimo,” alisema.

   Rais alisema pamoja na umuhimu huo wa kilimo kwa Tanzania na Afrika, bado kilimo cha Bara hilo kinabakia cha jadi, kilicho duni na chenye sifa ya uzalishaji mdogo.Niruhusuni nitoe takwimu kufafanua hoja hii. Katika Tanzania hekta moja ya mahindi inazalisha tani 1.3, wastani wa Afrika ni tani 1.9, katika China ni tani 5.7 na hapa Canada naambiwa ni tani 10. Vivyo hivyo, kwa uzalishaji wa mpunga na pamba.    Akizungumzia umuhimu wa kilimo katika Tanzania, alisema kuwa asilimia 75 ya Watanzania wanaishi maeneo ya mashambani na kutegemea kilimo kwa maisha yao na kuwa hata wale wanaoishi mijini uhai wao unategemea kilimo kwa njia nyingi.

  “Kilimo kinatupa chakula tunachokula, malighafi ya viwanda vyetu, mapato yetu ya fedha za kigeni na ajira kwa ajili ya watu wetu. Kilimo kinaingiza asilimia 25 ya Pato la Taifa, asilimia 34 ya mapato yetu ya fedha za kigeni, asilimia 95 ya chakula chetu na kinaajiri asilimia 75 ya watu wetu.    Kwa ufupi basi, maendeleo ya uchumi na ustawi wa wetu unategemea kilimo,” alisema.Rais alisema pamoja na umuhimu huo wa kilimo kwa Tanzania na Afrika, bado kilimo cha Bara hilo kinabakia cha jadi, kilicho duni na chenye sifa ya uzalishaji mdogo.


MSWADA WA KATIBA MPYA:RAIS KIKWETE SASA MTEGONI


  • NI KUTOKANA NA SHINIKIZO ANALOPATA KILA KONA
  •  JUKWAA LA KATIBA, CHIKAWE, WAPINZANI WAVAANA 
 Na: Darlin Said

Jukwaa la Katiba limemtaka Rais Jakaya Kikwete , asisaini Mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na badala yake atafute njia mbadala ya kuunusuru ikiwa ni pamoja na kurejeshwa bungeni ili ujadiliwe upya.Kauli hiyo ya Jukwaa la Katiba inaonekana kugeuka mtego kwa Rais Kikwete, kwani imetolewa siku moja baada ya Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, kumuomba Rais asaini mswada huo ili kuepusha vurugu zitakazoweza kujitokeza katika kikao kijacho cha Bunge kinachotarajia kuanza Oktoba, mwaka huu.

Mbali na Jukwaa la Katiba kutaka Rais Kikwete asisaini mswada huo, vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi, vimezidi kutafuta kuungwa mkono na wadau mbalimbali kwa lengo la kushinikiza mswada huo usisainiwe.Kauli ya kutaka Rais asisaini mswada huo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchakato wa katiba ulipofikia na matukio yaliyotokea bungeni.

  Kibamba alisema wanashangazwa na kauli ya Waziri Chikawe ya kumshinikiza Rais Kikwete asaini mswada huo wakati yeye (Rais Kikwete) ni kiongozi wa juu serikalini."Inashangaza kusikia Waziri Chikawe akisema kama Rais Kikwete atasaini mswada huo basi ataingia mgogoro na Bunge," alisema Kibamba na kuongeza kuwa hali hiyo ya kumlazimisha asaini au asisaini mswada huo ikiendelea anaweza kuvunja Bunge kwa mujibu wa katiba.   Kibamba, alisema mchakato wa Katiba Mpya kwa sasa upo njia panda, hivyo njia pekee ya kuunusuru ni Rais Kikwete, kurejesha bungeni ili ujadiliwe upya."Mjadala mkali uliojitokeza bungeni na kusababisha fujo na uvunjifu wa amani ni ishara ya mchakato wa Katiba Mpya kuwa njia panda na kuanza kukosa maelewano, uvumilivu na mwafaka ambayo ni misingi mikuu ya kuongoza mchakato huo,"alisema Kibamba.

Alibainisha kwamba kwa tukio hilo la bungeni, tathmini ya Jukwaa la Katiba inaonesha kuwa masilahi ya vyama vya siasa yametangulizwa badala ya hoja za wananchi. Kibamba, alisema Naibu Spika, Job Ndugai, alikuwa na nafasi ya kuahirisha mjadala mzima wa mswada huo baada ya vyama vya siasa kuususia hadi pale mambo yaliyokuwa yakigombewa yatatuliwe
Mbali na Jukwaa la Katiba kutaka Rais Kikwete asisaini mswada huo, vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi, vimezidi kutafuta kuungwa mkono na wadau mbalimbali kwa lengo la kushinikiza mswada huo usisainiwe.Kauli ya kutaka Rais asisaini mswada huo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchakato wa katiba ulipofikia na matukio yaliyotokea bungeni.

  Kibamba alisema wanashangazwa na kauli ya Waziri Chikawe ya kumshinikiza Rais Kikwete asaini mswada huo wakati yeye (Rais Kikwete) ni kiongozi wa juu serikalini."Inashangaza sikia Waziri Chikawe akisema kama Rais Kikwete atasaini mswada huo basi ataingia mgogoro na Bunge," alisema Kibamba na kuongeza kuwa hali hiyo ya kumlazimisha asaini au asisaini swada huo ikiendelea anaweza kuvunja Bunge kwa mujibu wa katiba.  Kibamba, alisema chakato wa Katiba Mpya kwa sasa upo njia panda, hivyo njia pekee ya kuunusuru ni Rais Kikwete, kurejesha bungeni ili ujadiliwe upya."Mjadala mkali uliojitokeza bungeni na sababisha fujo na uvunjifu wa amani ni ishara ya mchakato wa Katiba Mpya kuwa njia panda na kuanza kukosa maelewano, uvumilivu na mwafaka ambayo ni misingi mikuu ya kuongoza mchakato huo,"alisema Kibamba.

Alibainisha kwamba kwa tukio hilo la bungeni, tathmini ya Jukwaa la Katiba inaonesha kuwa masilahi ya vyama vya siasa yametangulizwa badala ya hoja za wananchi. Kibamba, alisema Naibu Spika, Job Ndugai, alikuwa na nafasi ya kuahirisha mjadala mzima wa mswada huo baada ya vyama vya siasa kuususia hadi pale mambo yaliyokuwa yakigombewa yatatuliwe

OPERESHENI KIMBUNGA YAIBUA MAPYA

Na Mwandishi Wetu

  Operesheni Kimbunga ya kuwaondoa wahamiaji haramu nchini imezidi kuibua mambo mapya kutokana na kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha 55, mabomu ya kurusha kwa mkono manane, bunduki 47 Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Kiongozi wa Timu ya Habari na Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Zamaradi Kawawa, juzi ilieleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kuanzia Septemba 6, 2013 hadi kufikia Septemba 17, 2013. 

Alisema miongoni mwa silaha zilizokamatwa katika operesheni hiyo ni bunduki aina ya SMG (4) Shotgun (4) Riffle (2) Mark IV (1) na Gobori 37.Alisema risasi 602 zilikamatwa zikiwemo risasi 500 za bunduki ya aina ya SMG na SAR, risasi (20) za bunduki aina ya Mark IV na risasi (82) za bunduki aina ya Gobori, fataki (8), mitambo ya kutengeneza magobori (2), misumeno ya kukata miti (9), mbao (1,516), magogo (86), na mkaa magunia (111). 

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo tangu kuanza kwa Operesheni hiyo ya kuwaondoa kwa lazima imefanikiwa kuwahamisha nchini wahamiaji haramu 7,819.Aliongeza kuwa watendaji wa Operesheni Kimbunga pia wamefanikiwa kukamata majangili Watanzania watatu, vipande vya meno ya tembo (2), pamoja na ngozi za wanyama mbalimbali..   Wakati huo huo, ng'ombe 3,436 wamekamatwa baada ya wafugaji haramu kutelekeza mifugo hiyo wakati walipozingirwa na timu ya operesheni kimbunga katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita."Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki wa mifugo kutoka nchi jirani ambao wengi wao ni matajiri na viongozi Serikalini kuwatuma watumishi wao kuingiza mifugo katika ardhi ya Tanzania hususan kwenye hifadhi ya Taifa kwa ajili ya malisho na watumishi hao hupewa silaha kwa ajili ya kujihami wakiwa kazini," alisema Zamaradi na kuongeza; 

  "Operesheni Kimbunga itahakikisha inawakamata wahalifu wote wanaotishia amani hususan katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita."Alisema wananchi ambao ni raia pamoja na raia wenye asili ya nchi jirani wanaowakaribisha na kuwahifadhi wahalifu na wahamiaji haramu watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.   Operesheni Kimbunga inayoongozwa na Brigedia Jenerali Mathew Sukambi imeanza rasmi Septemba 6, 2013 baada ya kutoa muda wa wiki mbili kwa wahamiaji wanaoishi nchini bila kufuata sheria kuondoka kwa hiari.

MSAJILI MPYA AISHUKIA CCM. ASEMA NI KINYUME CHA SHERIA, ATOA ONYO KALI NI KWA KUMTUMIA BALOZI WA CHINA KUFANYA SIASA


 Na Leah Daudi
MSAJILI mpya wa Vyama vya Siasa Nchini, jaji Francis Mutungi amekemea vikali kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumshirikisha balozi wa China nchini, Lu Younqing, katika shughuli za kisiasa.Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam na kusainiwa na Jaji Mtungi, ilisema kuwa amesikitishwa na suala la ushiriki wa raia wa kigeni katika mambo ya kisiasa hapa nchini.

Alisisitiza kuwa jambo hilo lipo kinyume na taratibu za kisheria.“Nimechukizwa na kitendo cha CCM kumruhusu raia wa kigeni kutumia jukwaa lake kufanya siasa, jambo hili si jema na limeweza kuzua hali ya taharuki kwa wananchi,” alisema jaji Mutungi na kuongeza; “Nachukua fursa hii kama mlezi wa vyama vya siasa kwa ujumla kuzingatia na kufuata sheria na taratibu stahiki katika utekelezaji wa shughuli zao za kisiasa.”Hivi karibuni Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahaman Kinana, akiwa mkoani Shinyanga, alimpandisha Balozi huyo wa China, Lu Younqing, akiwa amevaa kofia ya chama hicho na kumtaka aeleze miradi ambayo nchi yake inakusudia kutekeleza kwa Tanzania.

Kitendo hicho tayari kimelalamikiwa vikali na chama kikuu cha upinzani, CHADEMA ambapo kimetishia kuuandikia barua Umoja wa Mataifa (UN) kuhusiana na kitendo hicho kwani kinaenda kinyume na mikataba ya kimataifa.Pia Serikali tayari imeingilia kati suala hilo na kuwataka mabalozi wote wanaowakilisha nchi zao nchini kutambua kuwa wanawajibika kuheshimu mkataba wa kimataifa wa Vienna unaoainisha taratibu za kidiplomasia. Tayari Serikali imesema kuwa inajiandaa kumwandikia barua balozi huyo ili kumkumbusha wajibu wake baada ya kukusanya taarifa zote za tukio hilo.Hata hivyo, CCM kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Nape Nnauye, amekuwa akitetea kitendo hicho cha chama hicho kumsimamisha balozi huyo jukwaani.

Katika hatua nyingine, jaji Mutungi, alisema ofisi yake ipo kwenye mchakato wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa kutokana na iliyopo sasa kubainika kuwa na upungufu.Alisema lengo la hatua hiyo ni kukabiliana na changamoto zilizopo. Alisema ofisi yake inaendelea kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwa ni jitihada ya kufanikisha marekebisho hayo ya sheria.



WANASIASA WAJIBU MAPIGO YA KIKWETE


  • KUNDECHA ATANGAZA KUJIUNGA NA WAPINZANI
 Na Mariam Mziwanda
Viongozi wa vyama vilivyoingia ushirikiano vya CHADEMA, CUF na NCCR -Mageuzi, wamesema, mchakato wa kupata katiba mpya lazima ufanyike kwa maridhiano, vinginevyo vitisho, dharau na kupuuza baadhi ya maoni hakutasaidia kupatikana kwa mwafaka.

Viongozi wa vyama hivyo wametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuelezea kushangazwa na uongo wa baadhi ya wanasiasa hasa madai kwamba aliteua wajumbe wa Tume ya Katiba bila kuongozwa na mapendekezo ya wadau mbalimbali waliopendekeza majina hayo.

Wakizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam  ,viongozi hao ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema mchakato huo unahitaji maridhiano. Mbowe alisema ikiwa Rais atachukulia kwa mzaha suala hilo na kuamua kusaini mswada huo bila kutafakari kwa mapana yake nchi itaingia kwenye machafuko.“Tunarudia kumshauri na kumsihi Rais Kikwete kwamba katiba ni haki ya Watanzania wote, hivyo inahitaji busara, ushirikiano, uvumilivu, staa, kuangalia maslahi, kuaminiana na vitu vingine kama hivyo,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Kamwe hatuwezi kupiga magoti kwa kuomba katiba mpya, katiba sio zawadi kwa wanasiasa na hatupiganii kupatikana kwa katiba nzuri kwa maslahi yetu wenyewe, bali kwa maslahi ya Watanzania wote.”Kwa upande wake Profesa Lipumba, alisema Rais Kikwete ameanza kuonesha dharau kwa mambo yenye maslahi makubwa kwa taifa.“Kwanza naomba niseme kwamba Rais Kikwete ndiye hajaeleza  ukweli kwa Watanzania wanaoishi California, nchini Marekani,” alisema.Naye Mbatia alisema kama Rais Kikwete anadai ametumia mapendekezo ya wadau kuteua wajumbe, anapaswa kuweka wazi anayewakilisha kundi la walemavu.

Mbatia alisema Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) lilipendekeza majina matatu ili achaguliwe mmojawapo, lakini wote walitupwa nje na kufanya kundi hilo kujiona halina umuhimu ndani ya jamii.“Kama kweli anajua ameongozwa na mapendekezo hayo atueleze kila kundi limewakilishwa na nani, yapo mambo mengi tunayolalamikiwa tunataka haki itendeke kwa kila Mtanzania,” alisema. Kwa upande wa Amiri Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Mussa Yusuph Kundecha, alisema wameungana na upinzani kudai katiba inayokidhi matakwa ya Watanzania.“Tumejadiliana na kuafikiana kuungana ili katiba ipatikane yenye mawazo ya makundi yote, kwa bahati nzuri malalamiko yetu waislamu yamekuwa na uwiano sawa na malalamiko ya wapinzani. “Sasa kama wote tumekutana na wazo au shida moja lazima tuamue tufanye nini ili tupate jibu, sasa tunataka mswada urudi bungeni ujadiliwe upya ili kuondoa upungufu uliopo na vipengele vilichomekwa kinyemela.”

HUKUMU WAFUASI WA PONDA KUTOLEWA LEO

  Na: Rachel Balama.
Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam leo inatarajia kutoa hukumu dhidi ya wafuasi 52 wa Shekhe Ponda Issa Ponda, waliokata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela, waliyohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  

  Katika rufaa yao hiyo, wafungwa hao, kupitia kwa wakili wao, Mohamed Tibanyendela, wanapinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu, ambapo pamoja na mambo mengine, wanadai kuwa hakimu alikosea kisheria kuchambua ushahidi wa pande zote uliowasilishwa mahakamani hapo. 

Pia wanadai kuwa katika hukumu hiyo, hakimu alijikanganya kwa kumwachia huru mmoja wa washtakiwa na kuwatia hatiani washtakiwa wengine.Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa leo na Jaji Salvatory Bongole.    Machi, mwaka huu, Hakimu Sundi Fimbo wa Mahakama ya Kisutu aliwahukumu washtakiwa hao wa kesi ya kula njama na kufanya maandamano isivyo halali kwenda jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia katika makosa yaliyokuwa yakiwakabili.

  Washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa hayo Februari 15, mwaka huu.Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Salum Makame, Said Idd na Ally Nandumbi, Makame, Idd na Nandumbi, Hussein Athumani, Seif Rwambo, Abdull Ally, Waziri Swed, Naziru Waziri, Ahmad Rashid, Jumanne Kayogola, Hamis Tita, Amri Diyaga, Salum Said, Rajabu Mpita na Haji Sheluhenda, Abdul Ahmed, Bakari Mwambele, Ramadhani Fadhili na Awadh Juma.

  Wengine ni Omari Mkwau, Kassim Chobo, Abubakari Bakari, Ramadhani Milambo, Hamis Ndeka, Athuman Juma, Abdallah Salum, Juma Makoti, Bashir Kakatu, Imam Omari, Rashid Lukuta na Bakari Athumani, Mbwana Kassim, Nurdin Ahmed, Mustapha Mide, Rajabu Kifumbo, Zuberi Juma.   Wengine ni Omari Mkandi, Idrisa Katulimo, Sawali Mola, Said Dudu, Ramadhani Juma, Mussa Sinde, Issa Sobo, Yahaya Salum, Jabil Twahil, Shomari Tarimo, Hashim Bendera, Waziri Toy, Athuman Yahaya, Yasin Seleman, Shaban Malenda, Yasin Mohamed, Khatib Abdallah na Rajabu Rashid wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.

  Awali, ilidaiwa kuwa katika siku ya tukio, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama za kufanya maandamano isivyo halali.Shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kusababisha uvunjifu wa amani.   Shtaka la tatu ilidaiwa kuwa washtakiwa wote kwa pamoja walikiuka amri ya Jeshi la Polisi ya kutoa zuio la kufanya maandamano, n a k u f a n y a mk u s a n y i k o uliosababisha vurugu na uvunjifu wa amani.Katika shtaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Makame, Idd na Nandumbi, waliwashawishi wananchi kwa kuwasambazia vipeperushi vya kuhamasisha kufanya maandamano yasiyo halali.

MATEKA NCHINI KENYA WAOKOLEWA KUTOKA MIKONONI MWA MAGAIDI

37        Kama taarifa imekupita ni kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekiri kuwa idadi ya waliofariki inafikia 39 na zaidi ya 150 kujeruhiwa.. hizi picha zimetoka bbcswahili.com
36
35
34
33
38
32
31
30

Wasanii wa Kisasa Sanaa Group, wakiwa katika harakati za kukamilisha Filamu mpya ya (ACTION MOVIE), inatazamiwa kuingizwa sokoni baada ya Mwezi mmoja.


 Mzee Simba (ambaye amerekodi kama Mwizi wa Kuku, akiburutwa na Wananchi wenye Asira Kali baada ya Kuitiwa Kelele za Mwizi, pichani wananchi wakijadiliana kuhusu hukumu yake.
 Mwizi  wa Kuku Mzee Shaaban  Simba (Pichani akiigiza kama mtu aliyeitiwa kuuba kuku kisha kupigwa na wananchi wenye Asira Kali
 Wananchi wakimpeleka Mwizi wa KUKU katika Kituo cha Polisi
 Msanii wa Filamu hiyo, Marry Williums Mihayo, Happy Mashagal, Allan Kisandura,  Washiriki wa Kundi hilo wakipozi baada ya kumaliza kurekodi baadhi ya Sehemu ya Filamu hiyo
Wasanii Angel Pasical(kushoto), Silver  Williums, Haeshi Musa,   wakiwa katika harakati za maisha kila siku, ni baadhi ya wasanii wa kundi hilo katika kuonyesha maisha wanayoishi baadhi ya wakazi wa Tanzania, Hapa inaonekana jinsi maji yalivyo na taabu kupatikana.
 Mwongozaji wa Filamu Fredy Libaba, akitoa maelekezo kabla ya kuanza kurekodi
 Mzee Simba akiwa kakalishwa chini ya Ulinzi baada ya kukamatwa kwa Tuhuma za Kuiba Kuku
 Hapa Mzee Simba akipewa kipigo na wananchi wenye asira kali
 Wasanii Edwini Basi, Marry Williums, Silver Williams, Baadhi ya Wasanii wa Kisasa wakimfukuza Mwizi wa Kuku
 Msanii wa Kundi hilo Marry Mtipura wa pili kulia, na Baadhi ya Waigizaji wa Filamu hiyo wakiwa katika harakati za kurekodi
 Msanii wa kundi hilo Shaaban Simba, akipigwa na wakazi wa Maeneo hao wakimpiga baada ya kuiba kuku katika moja ya Sehemu zilizopo katika Mkanda huo wa Kusisimua.
 Mkufunzi wa na Mtunzi wa Filamu hiyo, Nyakasagani Masenza, akitoa Maelekezo kuhusu sehemu zinazorekodiwa.
 Washiriki wa Filamu hiyo wakiwa katika Mazungumzo
 Washiriki wa Filamu hiyo wakimfukuza Mwizi(Hayupo pichani)
 Msanii Shaaban Simba, akiwa Chini ya Ulinzi baada ya kukamatwa kwa kuiba kuku.
Kikundi cha Sanaa (Waigizaji wa Filamu) wa kundi la Kisasa Arts Group cha Keko Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika harakati za Kufanikisha Filamu ambayo imerekodiwa hapa hapa Tanzania, katika Maeneo mbalimbali. hapa ni kati ya Vipande Vilivyopo katika Mkanda huo, Baadhi ya Washiriki wakimwadabisha Mtu ambaye anasadikiwa kuiba Kuku katika Maeneo ya Mbagala Kokoto. kwa habari zaidi tembelea mtandao huu. www.shaabanmpalule.blogspot.com.
(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).