TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, September 26, 2013

MTIBWA SUGAR: SARE SASA BASI

 Na Fatuma Rashid 


 Timu ya Mtibwa Sugar imedhamiria kuondoa mdudu wa sare anayeiandama timu hiyo mara kwa mara.Akizungumza kwa simu akiwa Morogoro Katibu Mkuu wa timu hiyo, Salum Kijazi alisema hivi sasa wanajipanga ili waweze kufanya vizuri katika mechi dhidi ya Ashanti United.

   Kijazi alisema katika mechi, lazima kunakuwa na upungufu mbalimbali ambao husababisha wapinzani kutumia kama faida, hivyo timu yake inaendelea kurekebisha makosa yaliyojitokeza."Unajua katika kila mechi kuna upungufu wake na mpinzani wako hutumia kama faida, ila kwa kipindi hiki timu imejipanga vizuri na imefuta makosa yote ambayo kama tusingeyarekebisha tungekuwa katika nafasi mbaya," alisema.  Alisema msimu huu kila timu ipo vizuri, hivyo inasababisha kila mechi wawe wanajiandaa vizuri na kutumia kila mbinu katika mechi."Katika mpira unapoingia uwanjani hautakiwi kukurupuka, 

wachezaji wanatakiwa kujipanga na kujua ni mbinu gani wanazotumia timu pinzani, ili waweze kupambana nao, hivyo vijana wanajipanga ipasavyo kwani ligi inazidi kupamba moto kutokana na kila timu kujiandaa vizuri," alisema.  Akizungumzia waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu msimu huu, Kijazi alisema katika mechi iliyopita dhidi ya Prisons mwamuzi alikuwa akifanya makosa hivyo walichukulia kama makosa ya kawaida."Waamuzi wote wanachezesha vizuri, ila kuna makosa y a k i b i n a d amu amb a y o huwa yanatokea kwani huyo anayechezesha ni binadamu pia hivyo kuna haja ya kukaa na kuongea naye," alisema.   Alisema katika mechi dhidi ya Ashanti wamejipanga kufanya vizuri, licha ya kuwa na majeruhi ambao ni Mussa Hassan 'Mgosi' na Masudi Ally, walioumia wakati wa mazoezi lakini wanaamini katika mechi hiyo wataweza kucheza kutokana na hali zao kuwa nzuri.

MANJI AWATULIZA WACHEZAJI YANGA


 Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewatuliza wachezaji wa timu hiyo na kuwataka wakaze buti katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zinazokuja  Manji aliwatuliza wachezaji hao juzi alipokutana nao katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam kwa ajili ya kula chakula cha usiku pamoja na viongozi wengine wa Yanga.Katika mechi za ligi hiyo, ambazo Jumamosi itafikia mzunguko wake wa sita, Yanga ina pointi sita ikiwa imeachwa na watani wao wa jadi Simba yenye pointi 11 kileleni.

Manji aliwataka wachezaji hao, wasimlaumu mtu kwa matokeo waliyoyapata na badala yake kuelekeza nguvu katika mechi zilizobaki.Akizungumzia suala la baadhi ya wachezaji kudai fedha za usajili, Manji alisema tatizo hilo litashughulikiwa haraka iwezekanavyo ili kila mmoja apate chake.   Katika hatua nyingine, mchezaji aliyesajiliwa kutoka Simba Mrisho Ngassa ametakiwa kulipa deni la faini sh.milioni 45 kwa Simba kwa kosa la kusaini katika timu mbili. Habari kutoka ndani ya Yanga, zimeeleza kuwa mchezaji huyo anatakiwa kulipa fedha hizo kwa kuwa tayari walishamalizana na kama klabu ikilipa atalazimika kuongeza mkataba wa kuichezea timu hiyo miaka mitatu. 

  Chanzo hicho kimeeleza kwamba Yanga inamtaka Ngassa, kulipa fedha hizo kwa kuwa hazikuisaidia klabu bali zilimfaidisha yeye binafsi.
Ngassa alipotafutwa jana kuzungumzia suala hilo simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

UGAIDI KENYA : NGOMA NZITO


  • ESHI LASISITIZA HAKUNA KURUDI NYUMA HADI MWISHO

  • MAGAIDI SITA WAUAWA,10 WAKAMATWA AIRPORT
NAIROBI, Kenya
  Hali si shwari, unaweza kusema hivyo kutokana na mapambano yanayoendelea ndani ya Jengo la Westgate, nchini Kenya, kati ya majeshi ya Serikali nchini humo na magaidi wenye silaha tangu Septemba 21 mwaka huu .  Jengo hilo lilivamiwa na wapiganaji wa Al Shabaab ambao wanadaiwa kufikia 10 hadi 15, kusababisha mauaji ya watu 62, wengine 175 kujeruhiwa na kuwateka baadhi ya watu ambao hadi sasa wanawashikilia ndani ya jengo hilo.  
Taarifa iliyotolewa na Kituo cha Televisheni cha Citizen nchini humo, kilisema magaidi sita wameuawa katika mapambano hayo na wengine waliobaki ndani ya jengo hilo, wanaweza kujisalimisha baada ya kuwazidi nguvu.  Kituo hicho kimeongeza kuwa, wanajeshi watatu wa Kenya kati ya 11 waliojeruhiwa katika mashambulizi yanayoendelea ndani ya jengo hilo, wamefariki dunia na kubaki wanane.Mkuu wa Majeshi nchini humo, Jenerali Julius Karangi, alisema katika mapambano hayo hakuna kurudi nyuma hadi magaidi hao wajisalimishe wenyewe.
Raia wa nchi nyingine wahusishwa
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje nchini Kenya, Bi. Amina Mohamed, amesema mwanamke mmoja raia wa Uingereza anadhaniwa kuhusika na tulio hilo.Bi. Mohamed alisema, mbali ya mwanamke huyo pia kuna raia wawili au watatu Wamarekani ambao inasemekana ni miongoni mwa magaidi hao wa mtandao wa Al Shabaab.   Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), lilisema raia sita wa Uingereza wamethibitishwa kufa katika shambulio hilo.Ofisi inayohusika na Mambo ya Nje nchini Uingereza, ilisema ndugu wa karibu wa raia hao ambao wamepoteza maisha katika shambulio hilo, tayari wamepewa taarifa.
  Pia ofisi hiyo ilifafanua kuwa, haina taarifa zozote juu ya raia wao kuhusika na shambulio hilo, lakini bado wanaendelea kushirikiana na mamlaka za Kenya ili kuwasaidia katika uchunguzi kutokana na shambulio hilo la kinyama.   Akizungumza na waandishi wa habari nchini Pakistan, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Theresa May, alisema "Nimepata taarifa kuwa mwanamke raia wa Uingereza amehusishwa na tukio hili."Tutathibitisha taarifa hizi kama uchunguzi utakamilika, si rahisi kukubali au kukanusha kwa sasa," alisema May. 
Jeshi la Kenya
   Hadi jana mchana, Jeshi la Kenya lilikuwa katika hatua za mwisho kukamilisha msako wa kulikomboa jengo hilo mikononi mwa magaidi.Shirika la Habari nchini Ufaransa (AFP), lilisema majeshi ya Kenya yalikuwa yakikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa magaidi wawili walioosalia ndani ya jengo hilo kila mmoja akiwa amejificha eneo lake.    Milio ya risasi na milipuko ilisikika jana asubuhi katika jengo hilo, lakini Serikali ya Kenya, haijatoa idadi kamili ya mateka waliookolewa katika shambulio hilo.Kwa mujibu wa Kituo cha Televisheni cha K24 nchini Kenya, jana kilitangaza majina sita ambayo ni miongoni mwa magaidi wanaodaiwa kuhusika na shambulizi hilo. 
   Washukiwa hao ni Sayd Nuh (25), anayetoka Kismayu, Isamil Galed (23), Finland, Mustafa Noordiin (24) na Abdifatah Osman (24) wote raia wa Marekani, Kassim Musa (22), Garissa na Mohammed Badr (24), ambaye ni raia wa Syria.
Al Shabaab ni nani?
   Jina Al-Shabab linamaanisha kijana kwa lugha ya Kiarabu. Kundi hilo liliibuka kama tawi la vijana la muungano wa mahakama za Kiislamu ambao baadaye ulivunjika mwaka 2006 baada ya kupigana na wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini Somalia kuyaunga mkono majeshi ya Serikali. Kundi hilo limeweka sheria kali za Kiislamu katika maeneo wanayoyadhibiti ikiwemo ya kupigwa mawe hadi kufa wanawake wanaodaiwa kufanya uasherati na kuwakata wezi mikono.Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti katika baadhi ya miji mikubwa nchini Somalia, liliondoka Mji Mkuu Mogadishu Agosti 2011 na Mji wa Kismayo Septemba mwaka 2012.
    Kismayo ulikuwa mji muhimu wa kundi hilo na uliwawezesha kufikiwa na bidhaa pamoja na kuwatoza watu ushuru kwa shughuli zao.Kundi hilo lilianza kufanya mashambulizi ya kuvizia baada ya kushindwa na Majeshi ya Muungano wa Afrika wanaotumia nguvu dhidi yao ambapo Kenya ilianza harakati za kulimaliza kundi hilo mwaaka 2011 Kenyailiwatuhumu wapiganaji wa Al Shabaab kwa kuwateka nyara wanajeshi wake pamoja na watalii.
Nani kiongozi wa Al-Shabaab?
   Ahmed Abdi Godane ndiye kiongozi wa kundi hilo ambaye anajulikana kama Mukhtar Abu Zubair, akitokea katika Jimbo la Somaliland. Kumekuwa na taarifa za mgawanyiko katika kundi hilo, ambazo hata hivyo, zinapingwa vikali na kundi lenyewe.    Kiongozi wa kundi hilo Godane huwa haonekani hadharani, ambapo mtangulizi wake, Moalim Aden Hashi Ayro, aliuawa katika shambulizi lililofanywa na Marekani mwaka 2008.Al Shabaab walijiunga na al Qaeda, Februari mwaka 2012, ambapo kiongozi wa Al Shabaab (Godane), aliahidi kumuunga mkono kingozi wa al Qaeda, Ayman al-Zawahiri. Makundi hayo mawili yamekuwa yakifanya kazi kwa pamoja na baadhi ya raia wa kigeni wamekuwa wakiweaunga mkono na kuwasaidia katika harakati zao za mapigano 



MAAJABU YA MAITI DAR,, YAKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA PIPI 33


  •  Na Frank Monyo


   Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewashikilia watu wawili wakazi wa Tabata, kwa tuhuma za kukutwa na maiti ambayo tumboni ilikuwa na dawa za kulevya aina ya heroine.Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema maiti hiyo ilikuwa na dawa hizo pipi 33 na kuwataja watuhumiwa kuwa ni Nasri Omari 'Roboti' (36) na Mwanaisha Salim (36), wote wakazi wa Kigogo Luhanga, wakiwa na mwili wa marehemu Rajabu Kadunda. "Tulipata taarifa kuwa kuna mtu amefariki ghafla muda mfupi baada ya kutoka bafuni kuoga... tulikwenda eneo la tukio nyumbani kwa Omari na kuhoji hatimaye tuligundua uwepo wa maiti sebuleni ikiwa imelazwa chali katika godoro sakafuni. 


"Omari ambaye ndiye mmiliki wa chumba kilichokutwa maiti, alisema marehemu ambaye kwa jina lingine anafahamika kama Mashaka Mabruki (43) ni mfanyabiashara," alisema.



   Aliongeza kuwa, uchunguzi unaonesha kuwa marehemu alifika Dar es Salaam akitokea mkoani Mtwara Septemba 21 mwaka huu, kwa maelezo kuwa ni mgonjwa na alikwenda kuchukuliwa na watuhumiwa hao ambapo muda mfupi kabla ya kifo chake, alikwenda bafuni kuoga na hatimaye kufariki dunia.



   Kamishna Kova aliongeza kuwa, mazingira ya kifo hicho yalisababisha polisi kufika eneo la tukio, kuchukua maiti na kuipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi. "Uchunguzi uliofanywa na jopo la madaktari wawili pamoja na Maofisa wa Juu wa Polisi na ndugu wa karibu wa marehemu, zilikutwa pipi 33 za dawa za kulevya tumboni kwake.



"Pia marehemu alikutwa na hati ya dharura ya kusafiria nchi za nje ambazo hazikuonesha anasafiri kwenda nchi gani hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini mtandao mzima wa usafirishaji dawa hizi uliomhusisha marehemu," alisema.



     Alisema zipo taarifa zinazoonesha marehemu alikuwa mhalifu mzoefu wa kusafirisha dawa hizo kwani kabla ya kurudi Tanzania alikuwa akitumikia kifungo nje ya nchi Barani Asia.Wakati huo huo, jeshi hilo l ime f a n i k iwa k umk ama t a Dismas Chacha (33), ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Tabata kwa kujifanya mtumishi wa umma (daktari).



      Kamishna Kova alisema, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa mtuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kuchukua fedha zao akiwa na kawaida ya kuvaa mavazi ya kidaktari ambapo baada ya kupekuliwa, alikutwa na nyaraka mbalimbali zenye nembo ya Hospitali ya Muhimbili "Tulipata taarifa kuwa kuna mtu amefariki ghafla muda mfupi baada ya kutoka bafuni kuoga... tulikwenda eneo la tukio nyumbani kwa Omari na kuhoji hatimaye tuligundua uwepo wa maiti sebuleni ikiwa imelazwa chali katika godoro sakafuni."Omari ambaye ndiye mmiliki wa chumba kilichokutwa maiti, alisema marehemu ambaye kwa jina lingine anafahamika kama Mashaka Mabruki (43) ni mfanyabiashara," alisema.

   Aliongeza kuwa, uchunguzi unaonesha kuwa marehemu alifika Dar es Salaam akitokea mkoani Mtwara Septemba 21 mwaka huu, kwa maelezo kuwa ni mgonjwa na alikwenda kuchukuliwa na watuhumiwa hao ambapo muda mfupi kabla ya kifo chake, alikwenda bafuni kuoga na hatimaye kufariki dunia.

   Kamishna Kova aliongeza kuwa, mazingira ya kifo hicho yalisababisha polisi kufika eneo la tukio, kuchukua maiti na kuipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi. "Uchunguzi uliofanywa na jopo la madaktari wawili pamoja na Maofisa wa Juu wa Polisi na ndugu wa karibu wa marehemu, zilikutwa pipi 33 za dawa za kulevya tumboni kwake.

"Pia marehemu alikutwa na hati ya dharura ya kusafiria nchi za nje ambazo hazikuonesha anasafiri kwenda nchi gani hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini mtandao mzima wa usafirishaji dawa hizi uliomhusisha marehemu," alisema.

     Alisema zipo taarifa zinazoonesha marehemu alikuwa mhalifu mzoefu wa kusafirisha dawa hizo kwani kabla ya kurudi Tanzania alikuwa akitumikia kifungo nje ya nchi Barani Asia.Wakati huo huo, jeshi hilo l ime f a n i k iwa k umk ama t a Dismas Chacha (33), ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Tabata kwa kujifanya mtumishi wa umma (daktari).

      Kamishna Kova alisema, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa  tuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kuchukua fedha zao akiwa na kawaida ya kuvaa mavazi ya kidaktari ambapo baada ya kupekuliwa, alikutwa na nyaraka mbalimbali zenye nembo ya Hospitali ya Muhimbili "Omari ambaye ndiye mmiliki wa chumba kilichokutwa maiti, alisema marehemu ambaye kwa jina lingine anafahamika kama Mashaka Mabruki (43) ni  mfanyabiashara," alisema.

   Aliongeza kuwa, uchunguzi unaonesha kuwa marehemu alifika Dar es Salaam akitokea mkoani Mtwara Septemba 21 mwaka huu, kwa maelezo kuwa ni mgonjwa na alikwenda kuchukuliwa na watuhumiwa hao ambapo muda mfupi kabla ya kifo chake, alikwenda bafuni kuoga na hatimaye kufariki dunia.    Kamishna Kova aliongeza kuwa, mazingira ya kifo hicho yalisababisha polisi kufika eneo la tukio, kuchukua maiti na kuipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi. "Uchunguzi uliofanywa na jopo la madaktari wawili pamoja na Maofisa wa Juu wa Polisi na ndugu wa karibu wa marehemu, zilikutwa pipi 33 za dawa za kulevya tumboni kwake.

"Pia marehemu alikutwa na hati ya dharura ya kusafiria nchi za nje ambazo hazikuonesha anasafiri kwenda nchi gani hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini mtandao mzima wa usafirishaji dawa hizi uliomhusisha marehemu," alisema.  Alisema zipo taarifa zinazoonesha marehemu alikuwa mhalifu mzoefu wa kusafirisha dawa hizo kwani kabla ya kurudi Tanzania alikuwa akitumikia kifungo nje ya nchi Barani Asia.Wakati huo huo, jeshi hilo l ime f a n i k iwa k umk ama t a Dismas Chacha (33), ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Tabata kwa kujifanya mtumishi wa umma (daktari).

      Kamishna Kova alisema, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa  tuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kuchukua fedha zao akiwa na kawaida ya kuvaa mavazi ya kidaktari ambapo baada ya kupekuliwa, alikutwa na nyaraka mbalimbali zenye nembo ya Hospitali ya Muhimbili    Aliongeza kuwa, uchunguzi unaonesha kuwa marehemu alifika Dar es Salaam akitokea mkoani Mtwara Septemba 21 mwaka huu, kwa maelezo kuwa ni mgonjwa na alikwenda kuchukuliwa na watuhumiwa hao ambapo muda mfupi kabla ya kifo chake, alikwenda bafuni kuoga na hatimaye kufariki dunia.    Kamishna Kova aliongeza kuwa, mazingira ya kifo hicho yalisababisha polisi kufika eneo la tukio, kuchukua maiti na kuipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi. "Uchunguzi uliofanywa na jopo la madaktari wawili pamoja na Maofisa wa Juu wa Polisi na ndugu wa karibu wa marehemu, zilikutwa pipi 33 za dawa za kulevya tumboni kwake.

"Pia marehemu alikutwa na hati ya dharura ya kusafiria nchi za nje ambazo hazikuonesha anasafiri kwenda nchi gani hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini mtandao mzima wa usafirishaji dawa hizi uliomhusisha marehemu," alisema.       Alisema zipo taarifa zinazoonesha marehemu alikuwa mhalifu mzoefu wa kusafirisha dawa hizo kwani kabla ya kurudi Tanzania alikuwa akitumikia kifungo nje ya nchi Barani Asia.Wakati huo huo, jeshi hilo l ime f a n i k iwa k umk ama t a Dismas Chacha (33), ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Tabata kwa kujifanya mtumishi wa umma (daktari).

      Kamishna Kova alisema, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa  tuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kuchukua fedha zao akiwa na kawaida ya kuvaa mavazi ya kidaktari ambapo baada ya kupekuliwa, alikutwa na nyaraka mbalimbali zenye nembo ya Hospitali ya Muhimbili    Kamishna Kova aliongeza kuwa, mazingira ya kifo hicho  yalisababisha polisi kufika eneo la tukio, kuchukua maiti na kuipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi. "Uchunguzi uliofanywa na jopo la madaktari wawili pamoja na Maofisa wa Juu wa Polisi na ndugu wa karibu wa marehemu, zilikutwa pipi 33 za dawa za kulevya tumboni kwake. "Pia marehemu alikutwa na hati ya dharura ya kusafiria nchi za nje ambazo hazikuonesha anasafiri kwenda nchi gani hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini mtandao mzima wa usafirishaji dawa hizi uliomhusisha marehemu," alisema.

     Alisema zipo taarifa zinazoonesha marehemu alikuwa mhalifu mzoefu wa kusafirisha dawa hizo kwani kabla ya kurudi Tanzania alikuwa akitumikia kifungo nje ya nchi Barani Asia.Wakati huo huo, jeshi hilo l ime f a n i k iwa k umk ama t a Dismas Chacha (33), ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Tabata kwa kujifanya mtumishi wa umma (daktari).       Kamishna Kova alisema, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa mtuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kuchukua fedha zao akiwa na kawaida ya kuvaa mavazi ya kidaktari ambapo baada ya kupekuliwa, alikutwa na nyaraka mbalimbali zenye nembo ya Hospitali ya Muhimbili "Pia marehemu alikutwa na hati ya dharura ya kusafiria nchi za nje ambazo hazikuonesha anasafiri kwenda nchi gani hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini mtandao mzima wa usafirishaji dawa hizi uliomhusisha marehemu," alisema.

     Alisema zipo taarifa zinazoonesha marehemu alikuwa mhalifu mzoefu wa kusafirisha dawa hizo kwani kabla ya kurudi Tanzania alikuwa akitumikia kifungo nje ya nchi Barani Asia.Wakati huo huo, jeshi hilo l ime f a n i k iwa k umk ama t a Dismas Chacha (33), ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Tabata kwa kujifanya mtumishi wa umma (daktari).   Kamishna Kova alisema, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa mtuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kuchukua fedha zao akiwa na kawaida ya kuvaa mavazi ya kidaktari ambapo baada ya kupekuliwa, alikutwa na nyaraka mbalimbali zenye nembo ya Hospitali ya Muhimbili

     Alisema zipo taarifa zinazoonesha marehemu alikuwa mhalifu mzoefu wa kusafirisha dawa hizo kwani kabla ya kurudi Tanzania alikuwa akitumikia kifungo nje ya nchi Barani Asia.Wakati huo huo, jeshi hilo l ime f a n i k iwa k umk ama t a Dismas Chacha (33), ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Tabata kwa kujifanya mtumishi wa umma (daktari).  Kamishna Kova alisema, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa mtuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kuchukua fedha zao akiwa na kawaida ya kuvaa mavazi ya kidaktari ambapo baada ya kupekuliwa, alikutwa na nyaraka mbalimbali zenye nembo ya Hospitali ya Muhimbili

      Kamishna Kova alisema, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa  tuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kuchukua fedha zao akiwa na kawaida ya kuvaa mavazi ya kidaktari ambapo baada ya kupekuliwa, alikutwa na nyaraka mbalimbali zenye nembo ya Hospitali ya Muhimbili

CAG KUKAGUA OFISI YA MEYA BUKOBA

 Mariam Mziwanda na Stella Aron 

   Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utouh, amesema ofisi yake ipo mbioni kwenda mjini Bukoba, mkoani Kagera, ili kufanya ukaguzi wa mahesabu katika Ofisi ya Meya na kutoa ripoti yenye uhakika.   Bw. Utouh aliyasema hayo Dar es Salaam  katika mafunzo yaliyoshirikisha Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ili kuwajengea uwezo wa kuripoti taarifa za ofisi hiyo. 

  Alisema ukaguzi wanaokwenda kuufanya mjini Bukoba, hautokani na matakwa ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye; bali ni ombi maalumu lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.    Aliongeza kuwa, kumekuwa na taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikifanywa na baadhi ya makundi ambayo hayana nia njema na ofisi hiyo, hivyo ni vyema ikaeleweka kuwa, ukaguzi huo umezingatia agizo la Waziri Mkuu. 

 "Ofisi yangu inafanya kazi kikatiba si kwa matakwa ya chama chochote cha siasa, ukaguzi maalumu ambao utafanyika mjini Bukoba, utaanza wiki ijayo...ni jukumu la vyombo vya habari kuwa waangalifu wanaporipoti taarifa hizi.   "Wananchi wa Bukoba wasiwe na wasiwasi, tunakwenda huko lakini hatutaki chai ya mtu labda usafiri ambao upo kisheria kwa ajili ya ukaguzi wa miradi yenye utata iweze kufikiwa na kupatikana taarifa sahihi," alisema. 
  Bw. Utouh alisema uwajibikaji na uwazi ni mambo yasiyoweza kupatikana katika mfumo wa kuficha taarifa za utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali. 

  Alisema mahali ambapo habari inafichwa, lazima patatokea mvutano, kutoaminiana na hatimaye wananchi kuona Serikali yao ndiyo chanzo cha matatizo hivyo ni muhimu haki ya kikatiba kwa wananchi kupashwa habari ikazingatiwa.   Alitumia fursa hiyo kuvitaka vyombo vya habari nchini k u p u n g u z a u p o t o s h a j i n a kuelimisha jamii ipasavyo ili kusaidia makundi mbalimbali kuzielewa vizuri ripoti za CAG ili kuzuia machafuko yasiyo na lazima nchini. 

 "Madhara ya kuripoti taarifa za upotoshaji na mipaka ambayo inahitajika ni makubwa kwa jamii ...tunahitaji kufikiria masuala mazito yanayokwamisha kufikia malengo yetu, hivyo ni muhimu kuacha kutoa taarifa zisizo sahihi," alisema 

NCHIMBI: MSIWAHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU

Na Penina Malundo


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi,amesema Serikali itahakikisha wahamiaji haramu hawarudi nchini bila kufuata taratibu za kisheria zinazostahili kufuatwa. Dkt. Nchimbi aliyasema hayo Dar es Salam jana wakatiakizungumza na waandishi wahabari na kutoa matokeo ya awali juu ya utekelezaji Operesheni Kimbunga iliyolenga kuwaondoa wahamiaji haramu nchini

  Alisema kupitia operesheni hiyo awamu ya kwanza, wahamiaji haramu 12,604 wamerejeshwa katika nchi zao kutokana na agizo la kiongozi wa nchi, Rais Jakaya Kikwete. "Kati ya wahamiaji hawa,Wanyarwanda ni 3,448, Warundi 6,125, Waganda 2,496, Wakongo 589, Wasomalia 44, raia wa Yemeni mmoja na India mmoja," alisema Dkt. Nchimbi na kuongeza;"Ni vyema wahamiaji haramu wakafuata utaratibu wa kisheria,hata Watanzania wanaokwenda nchi nyingine nao wanapaswa kufuata utaratibu na si vinginevyo,"alisema.

   Alitoa wito kwa Watanzania,kuacha utamaduni wa kuwapokea na kuwahifadhi wahamiaji haramu jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao na nchi kwa ujumla. Alisema Watanzania wanapaswa kuwa macho na wageni wanaoingia nchini kutoka nchi nyingine bila kufuata taratibu za kuishi nchini kwani wengi wao wanauwezo wakufanya uhalifu hasa katika kipindi hiki cha usalama wa dunia kuwa hatarini.   

   Aliongeza kuwa, katika operesheni hiyo watuhumiwa 212 wa unyang'anyi wa kutumia silaha walikamatwa pamoja na mabomu 10 ya kutupwa kwa mkono, silaha 61, risasi 662 na mitambo miwili ya kutengeza silaha aina ya magobori

PUSH MOBILE KUTOA GARI KWA MSHINDI WA FIESTA

Na Mwandishi Wetu


   Kampuni ya Push Mobile Media, itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz kwa mshindi wa promosheni ya tamasha la Serengeti Fiesta litakalofanyika mkoani Mwanza leo    Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema watatoa gari aina ya Vitz kwa mpenzi wa Fiesta atakayeshiriki katika tamasha hilo kwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 na kuingia katika bahati nasibu hiyo.

Rodney alisema mbali ya kushinda gari, mshiriki pia anaweza kushinda fedha taslimu sh. 100,000 kwa siku. Pia mpenzi wa Fiesta anaweza kushinda pikipiki.Mshindi wa Mkoa wa Mwanza atakuwa wa pili kupata gari ambapo mshindi wa kwanza wa gari alikuwa Abdallah Ngagari (51) aliyeshinda kupitia tamasha la Fiesta la Kigoma.

  "Tumepania kutoa zawadi katika mikoa yote ambayo Fiesta itafanyika, tumetenga zaidi ya sh. milioni 80 ili kufanikisha jambo hili ambapo magari aina ya Vitz yapo nane kwa ajili ya kuwapa mashabiki, tunawaomba mashabiki kushiriki kwa nguvu zote," alisema Rodney. Wakati huo huo, mkazi wa Shinyanga, Rose Mahenda amafanikiwa kushinda pikipiki baada ya kushiriki katika bahati nasibu hiyo.

WAKAZI WA DAR ES SALAAM WANUFAIKA NA TAMASHA LA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA, UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI KWA WOTE

 Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika Mafunzo ya Biashara, na mafunzo jinsi ya kujiendeleza kiuchumi
  Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika Mafunzo ya Biashara, na mafunzo jinsi ya kujiendeleza kiuchumi
  Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika Mafunzo ya Biashara, na mafunzo jinsi ya kujiendeleza kiuchumi
  Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika Mafunzo ya Biashara, na mafunzo jinsi ya kujiendeleza kiuchumi
  Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika Mafunzo ya Biashara, na mafunzo jinsi ya kujiendeleza kiuchumi
 Semina hii ya mafunzo kwa watu wote inaendelea kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja. Dar Es Salaam
Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakipata Mafunzo hayo.(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania)

WAKULIMA RUFIKI KUFAIDIKA NA MATREKTA KUTOKA KWA MWEKEZAJI.

Mratibu wa mradi wa kilimo cha miwa wa Kampuni ya Agro Foresty Plantation Ltd, Bw. Kiondo Mahanyu, akikabidhi funguo za Trekta kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Chumbi B, Wilayani Rufiji, Bw. Abdulrahiman Ngongwe, kusaidia wakulima wa kijiji hicho kwa gharama nafuu. Kulia ni Afisa kilimo, Bi. Rose Mbezi na Bi. Mwanaidi Singano
Mratibu wa mradi wa kilimo cha miwa wa Kampuni ya Agro Foresty Plantation Ltd, Bw. Kiondo Mahanyu, akikabidhi funguo za Trekta kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Chumbi B, Wilayani Rufiji, Bw. Abdulrahiman Ngongwe, kusaidia wakulima wa kijiji hicho kwa gharama nafuu. Kulia ni Afisa kilimo, Bi. Rose Mbezi na Bi. Mwanaidi Singano
Baadhi ya Matrekta ambayo wakulima hao watafaidika nayo
 WENYEVITI wa vijiji vya kata ya Chumbi Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wamemuomba muwekezaji ambaye amepewa aridhi kwa ridha yao kuwekeza haraka katika mashamba ya miwa ili wananchi waanze kufaidi matunda ya uwekezaji.

Matunda wanayotarajia kufaidika nayo ni pamoja na ajira kwa vijana wao kwa vile ya kulimwa miwa muwekezaji atafugua kiwanda kikubwa cha sukari na kuwa mkombozi mkubwa kwa ajira katika kata hiyo hasa kwa vijana wengi wanaomaliza darasa la saba na kulanda mitaani bila ya shghuli ya kufanya.

Wakiongea juzi mbele ya mratibu wa mradi anaesimamia shughuli zote za Agro plantation wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani, Kiondo Mahanyu ,walisema ukimia wa kuanza mradi unawatia wasiwasi wakazi wa eneo hilo kutokana na maamuzi yao ya kutoa aridhi ili baadae waje wafaidi matunda.

Wakiongea kwa pamoja katika maongenzi yaliofanyika katika ofisi za serikali Chumbi, juzi ambako wenyeviti wote wa vijiji nane katika kata hiyo walikusanyika kwa lengo la kuchukua matrekta toka kwa muwekezaji kama sehemu ya kusaidiwa kulimiwa mashamba kupitia kaya ya vijiji.

Mwaka jana muwekezaji alitoa matrekta katika kila kijiji na kufanya baadhi ya kaya kuogeza nafaka maradufu pamoja na kuwepo kwa mvua zisozoridhisha. Pamoja na kutoa matrekta pia muwekezaji anatoa misaada ya kijamii katika vijiji hivyo kitu ambacho kimefanya wanavijiji wavutiwe zaidi na muwekezaji huyo.

Wenyeviti waliokuwepo katika makabidhiano ya matrekta juzi ni pamoja na kijiji cha Nyamwage, Ibrahimi Mboweto,Said Makangu mwenyekiti wa kijiji cha Muhoro Magharibi,Rashid kisomo, mwenyekiti wa Muhoro Mashariki,Ali Nguyu mwenyekiti wa Chumbi A.

Wengine ni pamoja na Abdalahamani Ngongwe kaimu mwenyekiti wa kijiji cha Chumbi B na mwenyekiti wa kijiji cha Chumbi C. Salum Mtimbuko, wwenyeviti wa vijiji vya Roma , Tawi,Roma na Muyuyu hawakuweza kufika kutokana na udhuru, lakini trekta zao zipo kwa ajili ya kuchukua na kukodisha wananchi katika vijiji hivyo.

Akiongea wakati wa kukabidhi matrekta kwa niaba ya muwekezaji,Mratibu wa kampuni Mahanyu,alisema sehemu kubwa ya uwekezaji katika kata hiyo ni kuakikisha wananchi wananufaika na mradi huyo ikiwemo ajira kwa vijana na kwenye taaluma mbalimbali za elimu.

Amesema kuchelewa kwa kuanza mradi kumetokana na mchakato wa kupimiwa aridhi kama unavyoelekezwa na Serikali na si Muwekezaji, hatahivyo amesema hatua iliofikiwa inaridhisha na wakatai wowote wanakijiji watatagaziwa kupatikana kwa hati rasmi ya umilikaji halali wa mashamba hayo.

"Nawataka wanavijiji watulie na kutafakari masuala ya mbele kutokana na mchakato kuelekea mwisho wa kufanikiwa kupata hati ili shughuli ziianze rasmi",alisema Mahanyu na kuongeza kuwa faida nyingine watakazopata wanakijiji hao ni pamoja na kushilikishwa katika kilimo cha miwa ambapo kila mwanakijiji atalima miwa na kuuzia kiwanda.

Faida zingine ni pamoja na kupewa ushauri toka kwa mabwanashamba watakaotoa elimu juu ya mashamba ya miwa na nafaka zingine zitakazolimwa katika kata hiyo.Tayari

Akiongea kwa niaba ya wenyeviti wezake nane wa vijiji hivyo katika kata hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kijiji cha Chumbi A, Ali Nguyu,alisema kusuasua kwa mradi huo kumewatia wasiwasi wanavijiji wa maeneo hayo ambapo waliwakilisha suala hilo kwa Mkurungenzi wa Wilaya ambaye pia aliwasiliana na mwakilishi wa na kwa pamoja waliwekena sawa kwa ajili ya kuendelea na mradi huo.

Hatahivyo wenyeviti  walimtaka muwekezaji kupuguza ghrama za kulima kwa kutumia matrekta hayo ambapo wametaka heka moja kulimiwa kwa shilingi 35,000 badala ya 45,000/= kama ilivyokuwa mwaka jana ambapo kutokana na maombi hayo mwakilishi wa Kampuni ya Agro Forest plantation alikubali ombi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani mama Mwantumu Mahiza alimpogeza muwekezaji huyo kwa kujitolea na kuwawezesha wakulima katika kata hiyo kulimiwa mashamba ili kuondoa hali ya njaa katika kata hiyo kutakokoenda sambamba na ukulima wa kisasa.

Akiongea kwa njia ya simu , Mahiza alisema muwekezaji huyo anatarajia kuleta mabadiliko makubwa ya kilimo na kiuchumi kwa jumla pindi atakapoaanza shughuli zake za kutayarisha mashamba ya miwa na hatimaye kufugua kiwanda cha sukari Wilayani humo.
Mwishoooo

Monday, September 23, 2013

SIMANZI nchini KENYA


Posted: 23 Sep 2013 04:04 AM PDT
  • WALIOUWAWA NA AL-SHABAAB KENYA WAFIKA 60
  • MWANADIPLOMASIA WA CANADA NAYE AUWAWA
  • MAKOMANDOO ISRAEL WATUA NAIROBI KUWASAKA
    Mmoja wa majeruhi (kushoto) akiwa na jeraha la risasi mgongoni akikimbia kuondoka eneo la tukio.
    Watu wakikimbia kuokoa maisha yao baada ya wavamizi kuanza kumiminia watu risasi.

    Majeruhi akiwa amebebwa kuondolewa eneo la tukio baada ya kushambuliwa na risasi.
    Na Goodluck Hongo
     Idadi ya watu waliokufa katika shambulio lililofanyika katika jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi nchini Kenya imefikia zaidi ya watu 60 na wengine 162 kujeruhiwa baada ya kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Al-Shabaab kuvamia na kuwamiminia risasi ovyo.

    Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha The Citizen cha nchini Kenya, kundi hilo lilivamia jengo hilo saa saba kasoro dakika 10 mchana juzi na kuanza kuwapiga risasi watu hao. Vikosi vya usalama vya nchi hiyo vikitumia mbwa na helikopta, vimeendelea kuzingira jengo hilo ambapo hadi jana mchana kundi hilo la watekaji lilikuwa bado linawashikilia watu ndani ya jengo hilo la ghorofa nne.

    Jengo hilo ambalo ni lenye maduka na migahawa mingi hutumiwa na watu wengi ambapo mara nyingi siku kama ya Jumamosi hujumuika na familia zao kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali.

    Televisheni hiyo ilionesha jinsi vikosi vya usalama vya nchi hiyo vilivyokuwa vikiokoa watu ambao walikuwa ndani ya jengo, huku helikopta za kijeshi zikizunguka jengo hiloTelevisheni hiyo ilisema wanamgambo hao ambao idadi yao haijafahamika bado wamejificha ndani ya jengo hilo wakiwa wamewateka idadi ya watu wasiojulikana wakati juhudi za kuwaokoa zikiendelea.

    Mitandao ya kijamii

    Katika baadhi ya mitandao ya kijamii ilimnukuu Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akielezea shambulizi hilo kuwa ni la kigaidi na kwamba kitendo hicho kamwe hakikubaliki.Alisema waliohusika watakumbana na mkono wa sheria. 
    Aliongeza kuwa Wakenya hawatagawanyika kutokana na shambulizi hilo na jeshi lake litaendelea kukabiliana na magaidi wa nje na ndani ya taifa hilo. Rais Kenyatta alisema baadhi ya waliofariki ni jamaa zake na miongoni mwa waliofariki ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa.

    Taarifa kutoka Ikulu ya Rais wa Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na majeraha yake.

    Mashuhuda

       Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema kuwa waliwaona watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao wakianza kumshambulia kila mtu waliyekutana naye ndani ya jengo hilo.Inadaiwa kwamba walikuwa wakiuliza waliyekutana naye maswali na aliyeshindwa kujibu alipigwa risasi.

    Uingereza yatoa tamko

       Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague, alisema Serikali yake inashirikiana na Kenya kuhakikisha magaidi na wanamgambo hao wanapatikana.Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kuikumba Kenya tangu shambulizi la bomu lililotokea mwaka 1998 lililotekelezwa na Al-Qaeda.

       Vikosi vya usalama vikishirikiana na vikosi maalumu kutoka jeshi la nchi hiyo wameendelea kuweka ulinzi mkali ili kuwaokoa watu walioshikwa mateka na watekaji hao wenye silaha nzito kwa majibu wa mashuhuda.

       Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), lilimnukuu Waziri wa Usalama Joseph Ole Lenku, akisema watu 59 wamefariki katika shambulizi hilo lililofanywa na wanamgambo wa Al-Shabaab na wengine 175 kujeruhiwa.Waziri Ole Lenku alisema kuwa idadi ya magaidi walio ndani ya jengo hilo ni kati ya 10 na haijulikani wamejificha sehemu gani katika jumba hilo la Westgate.

    Red Cross wanena

       Shirika la Msalaba Mwekundu la nchini Kenya awali katika taarifa yake, lilisema kuwa watu 43 ndiyo waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa katika shambulizi hilo.
     Habari zinaeleza kuwa hadi jana jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi yamepelekwa katika eneo hilo, huku polisi na wanajeshi wakijaribu kuokoa mateka.

       Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo, zinasema wanamgambo hao wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo.

    Al-Shabaab watamba kuhusika

        Kwa mujibu wa BBC, ofisa mmoja mkuu wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab, aliliambia shirika hilo kuwa kundi hilo ndilo limehusika na shambulio hilo.Kwa mujibu wa ofisa huyo mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na vita ndani ya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi hilo.

      Wanamgambo wa Al Shabaab kupitia kwa mtandao wao wa Twitter , wanasema kuwa Kenya haikuchukulia kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka wanajeshi wake nchini humo kupambana dhidi yao.

      Kundi hilo limesema limekuwa likitoa onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa vikosi vyake nchini Somalia, athari zitakuwa mbaya mno.Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al-Shabaab limesema kuwa Kenya haikusikia onyo hilo na kuendelea kuwaua Waislamu wasio na hatia nchini Somalia.

      Taarifa hiyo ya Twitter ilisema kuwa Shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba Wasomali nchini Somalia.

    Makomando wa Israel wajitosa

      Katika hatua nyingine makomandoo wa Israel jana waliwazidi nguvu wanamgambo wa Somalia na kufanikiwa kuwakomboa mateka waliokuwa wakishikiliwa na manamgambo hao.Milio ya risasi ya hapa na pale ilisikika huku maofisa usalama wa Kenya wakisema walikuwa wakijaribu kuwaua au kuwateka washambuliaji waliobakia na kumaliza umwagaji damu uliodumu kwa saa 28 katika ukumbi wa soko wa Westgate.

      “Makomandoo wa Israel wamekwisha wasili na sasa w a n a w a o k o a ma t e k a n a waliojeruhiwa,” chanzo cha habari cha usalama cha Kenya kiliiambia Shirika la Habari la Ufaransa- AFP. Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ilikataa kuthibitisha au kukanusha kwamba vikosi vyake vilihusishwa 

    WAFANYAKAZI TANAPA WADAIWA KUHUSIKA KWENYE UJANGILI

    Posted: 23 Sep 2013 01:46 AM PDT

    Na Said Njuki, Arusha
      Wakati ujangili wa meno ya tembo na faru ukiinyima usingizi Serikali, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewashtukia baadhi ya watumishi wake kutokana na kujihusisha na mtandao wa ujangili kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa vyombo mbalimbali vya dola.
    Kutokana na hali hiyo TANAPA inakusudia kubadili mfumo wake wa kiutendaji kutoka wa kiraia na kuwa mfumo kamili wa kijeshi kwa watumishi wote ili kujiimarisha katika kukabiliana na janga la ujangili nchini.

    Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete, aliwaambia waandishi wa habari jana mjini hapa kuwa Serikali haiwezi kuona maliasili ambazo ni urithi wa Watanzania na dunia kwa ujumla, zikiteketezwa na majangili na kuikosesha mapato Serikali.   Alisema lazima juhudi za makusudi zichukuliwe licha ya majangili hao kuwa na mtandao. Alisema ujangili hasa wa meno ya tembo na faru ni mtandao wa kimataifa unaohusisha watu wa kada mbalimbali, huku majangili hao wakitumia fedha nyingi na vifaa vya kisasa zikiwemo silaha za kivita, hali inayokwamisha jitihada za Serikali za kupambana na uhalifu huo.

      Shelutete alisema Shirika kwa kutumia vyombo vyake vya kiintelejensia vinawachunguza baadhi ya watumishi wake wanaojihusisha na mtandao huo na watakapogundulika na kujiridhisha watachukuliwa hatua kali za kisheria.  "Shirika linaendelea kuchunguza na kuchukua hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria kwa wafanyakazi wanaobainika kujihusisha na vitendo vya ujangili kwa kushirikiana na vyombo vya dola...uchunguzi unaendelea kufanyika kwa baadhi ya wafanyakazi na ushahidi wa kisheria utakapokamilika kwa wanaojihusisha na mtandao huo hatua za kisheria zitachukuliwa," alisema Shelutete
      "Tumepokea tuhuma dhidi ya baadhi ya watumishi wetu kujihusisha na ujangili, huo ni mwanzo mzuri kwetu katika kuchunguza tuhuma hizo kwa kutumia vyombo mbalimbali... hatukatai kuwa Shirika linaweza kuwa na watumishi wa aina hiyo, bali uchunguzi wa kina utafanyika ili tusimwonee mtu," alisema. 

       Alisema shirika linajua ukubwa wa tatizo, hivyo linajiandaa kwa mikakati mbalimbali ili kukabiliana na ujangili na tayari uimarishaji wa doria za magari, miguu na matumizi ya mbwa hifadhini kote nchini hali inayodhihirisha kupunguza kwa kiwango cha vitendo hivyo.  Alitoa mfano wa hifadhi za Tarangire na Ziwa Manyara akieleza kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita ujangili ulikuwa umeshika kasi umedhibitiwa kwa asilimia 100 kwa maana hakuna tembo hata mmoja aliyeuawa.

      Alitaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na kuanzishwa kwa kikosi maalumu cha kupambana na ujangili na matukio ya dharura, kutoa mafunzo maalumu ya awali kwa askari 100 ambao wataingia katika mafunzo ya awamu ya pili hivi karibuni.  Aliyataja baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na kunasa majangili 1,116 ndani ya hifadhi za taifa nchini, wakiwemo majangili 248 walioshikwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pekee katika kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu, kukamata silaha za moto 85 na waya zinazotumika kutega wanyama 25,422, mbao 3,275' mbao 1030 na mifugo 6,650.