Baadhi ya Matrekta ambayo wakulima hao watafaidika nayo |
WENYEVITI wa vijiji vya kata ya
Chumbi Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wamemuomba muwekezaji ambaye amepewa
aridhi kwa ridha yao kuwekeza haraka katika mashamba ya miwa ili wananchi
waanze kufaidi matunda ya uwekezaji.
Matunda wanayotarajia kufaidika nayo ni
pamoja na ajira kwa vijana wao kwa vile ya kulimwa miwa muwekezaji atafugua
kiwanda kikubwa cha sukari na kuwa mkombozi mkubwa kwa ajira katika kata hiyo
hasa kwa vijana wengi wanaomaliza darasa la saba na kulanda mitaani bila ya
shghuli ya kufanya.
Wakiongea juzi mbele ya mratibu wa
mradi anaesimamia shughuli zote za Agro plantation wilayani Rufiji Mkoa wa
Pwani, Kiondo Mahanyu ,walisema ukimia wa kuanza mradi unawatia wasiwasi wakazi
wa eneo hilo kutokana na maamuzi yao ya kutoa aridhi ili baadae waje wafaidi
matunda.
Wakiongea kwa pamoja katika maongenzi
yaliofanyika katika ofisi za serikali Chumbi, juzi ambako wenyeviti wote wa
vijiji nane katika kata hiyo walikusanyika kwa lengo la kuchukua matrekta toka
kwa muwekezaji kama sehemu ya kusaidiwa kulimiwa mashamba kupitia kaya ya
vijiji.
Mwaka jana muwekezaji alitoa matrekta
katika kila kijiji na kufanya baadhi ya kaya kuogeza nafaka maradufu pamoja na
kuwepo kwa mvua zisozoridhisha. Pamoja na kutoa matrekta pia muwekezaji anatoa
misaada ya kijamii katika vijiji hivyo kitu ambacho kimefanya wanavijiji
wavutiwe zaidi na muwekezaji huyo.
Wenyeviti waliokuwepo katika
makabidhiano ya matrekta juzi ni pamoja na kijiji cha Nyamwage, Ibrahimi
Mboweto,Said Makangu mwenyekiti wa kijiji cha Muhoro Magharibi,Rashid kisomo,
mwenyekiti wa Muhoro Mashariki,Ali Nguyu mwenyekiti wa Chumbi A.
Wengine ni pamoja na Abdalahamani
Ngongwe kaimu mwenyekiti wa kijiji cha Chumbi B na mwenyekiti wa kijiji cha
Chumbi C. Salum Mtimbuko, wwenyeviti wa vijiji vya Roma , Tawi,Roma na Muyuyu
hawakuweza kufika kutokana na udhuru, lakini trekta zao zipo kwa ajili ya
kuchukua na kukodisha wananchi katika vijiji hivyo.
Akiongea wakati wa kukabidhi matrekta
kwa niaba ya muwekezaji,Mratibu wa kampuni Mahanyu,alisema sehemu kubwa ya
uwekezaji katika kata hiyo ni kuakikisha wananchi wananufaika na mradi huyo
ikiwemo ajira kwa vijana na kwenye taaluma mbalimbali za elimu.
Amesema kuchelewa kwa kuanza mradi
kumetokana na mchakato wa kupimiwa aridhi kama unavyoelekezwa na Serikali na si
Muwekezaji, hatahivyo amesema hatua iliofikiwa inaridhisha na wakatai wowote
wanakijiji watatagaziwa kupatikana kwa hati rasmi ya umilikaji halali wa
mashamba hayo.
"Nawataka wanavijiji watulie na
kutafakari masuala ya mbele kutokana na mchakato kuelekea mwisho wa kufanikiwa
kupata hati ili shughuli ziianze rasmi",alisema Mahanyu na kuongeza kuwa
faida nyingine watakazopata wanakijiji hao ni pamoja na kushilikishwa katika
kilimo cha miwa ambapo kila mwanakijiji atalima miwa na kuuzia kiwanda.
Faida zingine ni pamoja na kupewa
ushauri toka kwa mabwanashamba watakaotoa elimu juu ya mashamba ya miwa na
nafaka zingine zitakazolimwa katika kata hiyo.Tayari
Akiongea kwa niaba ya wenyeviti
wezake nane wa vijiji hivyo katika kata hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kijiji
cha Chumbi A, Ali Nguyu,alisema kusuasua kwa mradi huo kumewatia wasiwasi
wanavijiji wa maeneo hayo ambapo waliwakilisha suala hilo kwa Mkurungenzi wa
Wilaya ambaye pia aliwasiliana na mwakilishi wa na kwa pamoja waliwekena sawa
kwa ajili ya kuendelea na mradi huo.
Hatahivyo wenyeviti walimtaka muwekezaji kupuguza ghrama za
kulima kwa kutumia matrekta hayo ambapo wametaka heka moja kulimiwa kwa
shilingi 35,000 badala ya 45,000/= kama ilivyokuwa mwaka jana ambapo kutokana
na maombi hayo mwakilishi wa Kampuni ya Agro Forest plantation alikubali ombi
hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mama Mwantumu
Mahiza alimpogeza muwekezaji huyo kwa kujitolea na kuwawezesha wakulima katika
kata hiyo kulimiwa mashamba ili kuondoa hali ya njaa katika kata hiyo
kutakokoenda sambamba na ukulima wa kisasa.
Akiongea kwa njia ya simu , Mahiza
alisema muwekezaji huyo anatarajia kuleta mabadiliko makubwa ya kilimo na
kiuchumi kwa jumla pindi atakapoaanza shughuli zake za kutayarisha mashamba ya
miwa na hatimaye kufugua kiwanda cha sukari Wilayani humo.
Mwishoooo
No comments:
Post a Comment