Na Mwandishi Wetu
Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazopatikana katika kisiwa cha Anjouan nchini Comoro ili kukuza na kuendeleza ushirikiano uliopo kwa maslahi ya kijamii na kiuchumi kati ya pande hizo mbili.
Gavana wa Anjouan, Anissi Chamsidine,al ielezah ayoalipotembel eaKituo cha Uwe kezaji Ta nz ania(TIC) janajijini Dar es Salaam."Tuna fursa nyingi za uwekezaji katika kisiwa cha Anjouan na tunaamini Watanzania wako katika nafasi nzuri ya kuzitumia," alisema na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili ni wadamu na wa kihistoria.
Alisema kuna umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika eneo la uwekezaji na kutaja maeneo ambayo yan ahitaji uwekezaji kuwa ni elimu,utalii,nishati na katika sekta ya afya."Tuna hospitali kubwa zinajengwa lakini tatizo ni kukosekana kwa wataalamu wa afya ikiwemo wauguzi na madaktari hivyo tunaomba Watanzania waje kutusaidia
katika eneo hilo," alisema. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Juliet Kairuki amesema kuwa ujio wa Gavana huyo na ujumbe wa wawekezaji utasaidia kufungua fursa za uwekezaji na ushirikiano mzuri kiuchumi kati ya nchi hizo. "TIC na Serikali inathamini ziara ya Gavana na ujumbe wake, uhusiano wetu ni wa siku nyingi na tungependa kuimarisha," alisema na kuongeza kuwa ziara hiyo itasaidia kuvutia uwekezaji kutoka katika kisiwa hicho.
No comments:
Post a Comment