TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, July 22, 2014

MKOANI MOROGORO MAFUNZO YA TABIA NCHI KWA WATAALAMU YAFUNGULIWA

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akifungua rasmi mafunzo  yanayowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanayoendelea mjini Morogoro. Aliyekaa upande wa kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gidion  Kasege.
 Mmoja wa wawezeshaji Profesa Pius Yanda kutoka Kituo cha Taaluma ya Mabadiliko ya Tabianchi kilichopo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo
 Baadhi  ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na wawezeshaji kwa nyakati tofauti tofauti
 Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira Mhandisi Gidion  Kasege  (kulia) na Afisa Mazingira Mkuu na Mratibu wa Mradi wa EMA-ISP Bw. Theodore Silinge kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa
 Afisa Mazingira Mkuu na Mratibu wa Mradi wa EMA-ISP kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Theodore Silinge akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
 Mtaalamu kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Nyaso Makwaya akisisitiza jambo wakati alipokuwa  akiwasilisha mada kuhusiana na mikakati ya Wizara katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gidion  Kasege  (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava  (aliyekaa kulia kwake) ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo  yanayowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanayoendelea mjini Morogoro.
 Washiriki  wa mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi  yanayoendelea mjini Morogoro wakiwa katika picha  ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto waliosimama mstari wa mbele) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo

DAR ES SALAAM KUMEKUCHA- WATOTO SASA WAIBWA, TAYARI WAMEPOTEA WANNE


Mtoto aliyeibwa, Merryn Reppyson

MTINDO mpya wa kuiba watoto jijini Dar es Salaam, umezusha hofu kwa wazazi na walezi hali inayofanya baadhi yao kuhofia kutoka nyumbani na kuwaacha watoto wao na wasichana wa kazi.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini katika kipindi cha wiki moja, watoto wanne wameibwa na watu wasiojulikana na kutokomea nao katika mazingira ya kutatanisha.
Moja ya tukio ambalo linaendelea kuvuta hisia za watu wengi ni lile lililotokea eneo la Changanyikeni karibu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Katika tukio hilo, Merryn Reppyson (3), alipotea Julai 15, mwaka huu baada ya mtu asiyejulikana kumchukua kutoka nyumbani kwao.
Akizungumza na MTANZANIA jana, mama mzazi wa Merryn, Elida Fundi, alisema mtu aliyemuiba mtoto wake alifika nyumbani kwake na kuomba kwenda msalani.
Elida alisema alipokutana na dada wa kazi mlangoni mtu huyo alimuulizia Merryn na wazazi wake.
Alisema baada ya mtu huyo kufika ndani ya nyumba aligonga mlango akidhani kuwa mtoto yupo peke yake, lakini baada ya kugonga na kusikia sauti ya mtu mzima ikimkaribisha alilazimika kuomba kuingia msalani.
“Huyu mtu alivyokuwa akiingia getini kwangu alipishana na dada mlangoni, alihisi mtoto atakuwa ndani peke yake, baada ya kukuta kuwa ndani kuna mtu mwingine tofauti na dada aliyepishana naye getini, alilazimika kuomba kwenda msalani.
Dada aliyekuwa pale nyumbani alimuelekeza choo cha nje, alivyotoka huko alikuta mtoto akiwa pale nje akamchukua na kuondoka naye, hicho kilikuwa ni kitendo cha kama dakika tano tu.
Nimechanganyikiwa kabisa hapa, mtoto ameibwa na hatujampata mpaka sasa, aliyemuiba anaonekana anatufahamu kwa sababu dada anasema alikuwa anakuja siku moja moja hapa nyumbani na kutuulizia mimi na mume wangu wakati anajua muda huo tunakuwa kazini.
Lakini pia alikuwa anamfahamu mtoto wangu mpaka kwa jina, akija hapo anakuwa anamuita kabisa kwa jina, anamuuliza mama yupo? Baba yupo,” alisema Elida.
Alisema kuwa mtu aliyemuiba mtoto huyo alifika nyumbani kwake kwa siku tatu tofauti na siku ya tatu ndipo alipomuiba.
Alifafanua dada aliyemkaribisha mtu huyo, alishangaa baada ya kuona mtu aliyeomba kujisaidia ameondoka bila kuaga.
Alieleza pia kuwa dada huyo alishangaa kutomuona mtoto nje hata hivyo, akajipa matumaini kuwa atakuwa ameingia chumbani.
“Dada wa kazi ambaye alikuwa amepishana na yule mgeni getini, aliporudi nyumbani alimuulizia Merryn kwa kuwa hakumuona ndipo walipoanza kumtafuta huku wakiwauliza majirani ambao walidai alipita na mjomba wake ambaye alikuwa anaenda kumnunulia ndizi,” alisema.
Alisema wakati wakiendelea kumtafuta mtoto huyo walifika kwenye genge lililo karibu na nyumba yake na kuambiwa kuwa mtoto huyo alifika hapo na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mjomba wake na kumnunulia ndizi kisha wakaondoka.
“Tukio hili limenishangaza kwa kuwa hatujawahi kugombana na mtu, itakuwa tu wamemchukua ili kututisha au tuwape pesa, lakini hatuna ugomvi na mtu,” alisema Elida.
Alisema tangu kutokea kwa tukio hilo ambalo limeripotiwa katika kituo cha polisi cha Changanyikeni, mpaka sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa zinazohusiana na upatikanaji wa mtoto huyo.
Alisema majibu ambayo wamekuwa wakiyapata kutoka polisi ni kuwa uchunguzi bado unaendelea.
Wakati matukio hayo yakiendelea msichana, Islam Yasin (16), amepotea katika mazingira ya kutatanisha uko Mbezi Msakuzi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Islam ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mpigi Majohe, alipotea tangu Julai mosi hadi sasa hajulikani alipo.
Taarifa za kupotea kwake zimeripotiwa katika kituo kidogo cha polisi Mbezi kwa Yusuf na kufunguliwa jalada lenye kumbukumbu ya RB/6451/2014.
Akizungumza na MTANZANIA jana, mama mzazi wa binti huyo, Conses Buberwa, alisema katika kipindi cha wiki mbili wamekuwa wakimtafuta binti yake bila mafanikio.
Alisema yeyote mwenye taarifa za kupotea kwa msichana huyo atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi kilichopo jirani naye au apige simu namba 0657004332.
Siku ya tukio, Islam alikuwa amevaa blauzi nyekundu na kubeba kanga doti moja za aina tofauti ambazo alizihifadhi kwenye mkoba wake.
Kauli ya Polisi
Akizungumza na MTANZANIA, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alithibitisha kutokea kwa matukio hayo huku akisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wake.
“Ni kweli tumepata taarifa hizo tunazifanyia kazi ili tuweze kujua ni kina nani waliowaiba watoto hao, lakini bado ninaendelea kukusanya matukio ya aina hii kutoka katika vituo vyote vya polisi ili tuweze kubaini ukubwa wa hali ya matukio haya,” alisema Wambura.
Waziri Simba
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, aliliambia gazeti hili kuwa wizi huo unatokana na wazazi kutokuwa makini katika masuala ya ulinzi kwa watoto.
“Jukumu la wizara ni kulinda haki za watoto, ulinzi wa mtoto binafsi ni kazi ya mzazi Serikali haiwezi ikaweka polisi kila nyumba yenye watoto kwa ajili ya ulinzi,” alisema Waziri Simba.
Alisema hivi sasa wazazi wamekuwa hawana muda na watoto wao na hata kushindwa kufuatilia taarifa za watoto wao.
“Serikali itaendelea kuwatafuta watu wanaofanya vitendo vya ukatili wa watoto na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Ripoti ya utafiti uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) katika mikoa 18 ya Tanzania Bara na Visiwani, imebaini kuendelea kushamiri kwa vitendo hivyo huku matukio 996 ya udhalilishaji yakiripotiwa kutokea katika wilaya sita za Zanzibar.

Kati ya matukio hayo, 242 yalihusu ubakaji, vipigo vilikuwa 388, ndoa za utotoni 42, kutelekezwa 96, mimba za utotoni 228, ambapo kwa upande wa Tanzania Bara ukionyesha kuwa Wilaya ya Babati mkoani Manyara inaongoza ikiwa na matukio 132.

Ripoti ya Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto Tanzania, iliyotolewa na Serikali pamoja na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) mwaka 2011, ilidhihirisha kuwa msichana mmoja kati ya watatu na mvulana mmoja kati ya saba nchini Tanzania hukumbwa na unyanyasaji wa kijinsia kabla ya kufikisha umri wa miaka

Morogoro Kumpata Miss Kanda Mashariki Agosti 8

Mashindano ya kumsaka mrembo kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014) yatafanyika siku ya sikukuu ya Nanenane kwanue ukumbi wa  Nashera Hotel, mkoani Morogoro.
 
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo  14 kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani, Lindi, Mtwara na mwenyeji, Mkoa wa Morogoro chini ya udhamini wa Redds Original, Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari Lodge, Kitwe General Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC Africa, Sykes Travel, Sasa Saloon, Grand Villa Hotel, Shabibi Line na Clouds FM.
 
Mratibu wa masindano hayo, Alex Nikitas aliwataja warembo watakaoshindana siku hiyo kuwa ni Lucy Julius Diu, Prisca  Mengi, Tarchisia Noback Mtui na Angel  Shio ambao wanatoka Morogoro.Warembo wengine ni Elizabeth Tarimo, Lilian  Andrew na Leila  Abdul  Ally ambao wanatoka mkoa wa Lindi ambapo kutoka Mtwara ni  Nidah Fred Katunzi, Lightness  Mziray na Nelabo  Emmanuel.
 
Pia warembo kutoka Pwani ni Khadija Ramadhan Sihaba, Irene Rajabu Soka, Mary  Mpelo na Arafa Shaban. Nikitas alisema kuwa warembo hao watakuwa kambini kuanzia Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge chini ya Miss Kanda ya mashariki mwaka jana,  Diana Laizer.

TUKIO LA VIUNGO LA BINADAMU,WATU NANE WAKAMATWA JIJINI DAR.

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na Vyombo vya habari mbalimbali mapema leo, makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar kuhusiana na sakata la viungo vya binadamu vilivyokamatwa jana INGIA HAPA KUONA TUKIO HILO.Kamanda Kova amesema kuwa watu wanane wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Kova amesema kuwa jopo la Wataalamu saba limeundwa kuchunguza tukio hilo na amethibitisha kuwa viungo vile vilikuwa ni vya maiti,ambavyo hutumika na madaktari kwa elimu ya matibabu na utafiti. 

SHILOLE NA STAILI YA SERENGETI BOY JUU YA JUKWAA

Shilole akiwa amelaliwa juu na kidume alipokuwa akifanya show na hii ni style yake

GAZA KIMENUKA ANGALIA HALI ILIVYOCHAFUKA

'I want my father, bring me my father!': The boy is thought to be one of four young siblings brought to the Gaza City hospital last week...

Grief: Israeli soldiers of the Paratroopers Brigade mourn over the grave of Sgt. Bnaya Rubel during his funeral
As Israeli airstrikes continued to pound Gaza on Monday, rescue workers near the southern Gaza city of Khan Younis were digging out bodies from a home flattened in one of the strikes overnight, said Ashraf al-Kidra, a Gaza health ministry official.
Al-Kidra said the Palestinian death toll from the two-week offensive stood at 508 as of Monday morning, including 20 bodies that were found at the site in Khan Younis. Two people were pulled alive from the rubble, he added.
Elsewhere in Gaza, Israeli tanks opened fire on the home of the Siyam family west of Rafah in the southern part of the strip, killing 10 people, including four young children and a 9-month-old baby girl, al Kidra said.
 

Monday, July 21, 2014

PPF YAFUTURISHA SIKU YA JANA WAFANYAKAZI WAKE

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akitoa hotuba kwa wafanyakazi wa Mfuko huo baada ya futari iliyoandaliwa na Ofisi yake kwa wafanyakazi wake kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio(Wapili kushoto) na baadhi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Mfuko huo, wakishiriki futari iliyoandaliwa na ofisi yake kwa wafanyakazi wa PPF kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakishiriki futari iliyoandaliwa na Mfuko huo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakishiriki futari iliyoandaliwa na Mfuko huo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wafanyakazi wake, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KOICA/KAAT) yapata uongozi mpya

*Wadhamiria kuitangaza Tanzania kibiashara kimataifa

Na Saidi Mkabakuli
 Rais Mpya wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KAAT), Bw. Stephen Katemba (Kulia) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa. Anayemsikiliza ni Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Kushoto).
 Viongozi wapya KAAT na viongozi wa zamani wakipongezana mara baada ya uchaguzi huo
 Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Katikati) akizungumza machache mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo. Kushoto ni aliyekuwa Muweka Hazina wa KAAT, Bibi Emilia Maingu na kulia ni Bw. Stephen Matee ambaye ni Muweka Hazina mpya.
 Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Wapili Kulia) akikabidhi nyaraka za KAAT kwa uongozi mpya. Kutoka kushoto pichani ni Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara), Bw. Bukheti Juma (Wapili kushoto) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar). Wengine ni Rais Mpya Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Stephen Matee (Kulia)ambaye ni Muweka Hazina mpya.
 Uongozi mpya wa KAAT wakizungumza na Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Wapili kulia).
 Wakiwa katika picha ya pamoja ni uongozi mpya wa KAAT na baadhi ya viongozi wa zamani wa Jumuiya hiyo.
======================================
Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea imefanikiwa kupata uongozi mpya, utaongoza umoja wa Watanzania hao kwa muda wa miaka miwili.
Waliochaguliwa kuongoza KAAT ni pamoja na Bw. Stephen Katemba ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya. Bw. Katemba atasaidiwa na Bw. Bukheti Juma (Makamu wa Rais, Zanzibar) na Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara). Katika nafasi ya Uweka Muweka Hazina, aliyechaguliwa ni Bw. Stephen Matee, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) ulio chini wa Mama Anna Mkapa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa rasmi jukumu la kuiongoza Jumuiya hiyo, Bw. Katemba ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya Uchumi na Biashara za Kimataifa, amesema kuwa Tanzania ina fursa kubwa katika eneo la biashara za kimataifa kuwa kuzingatia rasilimali zilizopo nchini na kuchagiza kuwa fursa hizo zinaweza kutumiwa ipasavyo kwa kujitangaza tu.
Bw. Katemba aliongeza kuwa kama Watanzania tukiwa na uzalendo wa dhati na kuwa mabalozi wazuri, Tanzania itakuwa na uhakika wa kukamata masoko makubwa ikiwemo Korea na Bara la Asia kwa ujumla.
“Kwa mfano kwa mujibu wa hali ya uchumi wa Taifa, kwa mwaka 2013, mwenendo wa biashara ya bidhaa na huduma nje haukuwa wa  kuridhisha ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2012. Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ilipungua kwa asilimia 1.7 kutoka Dola za Kimarekani milioni 8,675.6 mwaka 2012 hadi Dola milioni 8,532.0,” alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Katemba kuwa ili kufikia malengo ya kimkakati ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulio chini ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao umelenga kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi, Tanzania haina budi kufikia malengo ya kikao cha tisa cha Shirikisho la Biashara Ulimwenguni (WTO) ambalo linalenga kuziwezesha kibiashara nchi wanachama kuboresha biashara zao.
“Katika kikao cha tisa cha WTO, Mawaziri wa nchi wanachama 159 wa Shirikisho walikubaliana
kuwa na “Mpango wa Bali” ambao unalenga kuziruhusu nchi zinazoendelea kuwa na fursa zaidi ya kuzalisha chakula cha akiba, kuinua kiwango cha biashara kwa nchi changa na kusaidia maendeleo ya nchi changa kibiashara. Hivyo, tunaweza kufikia malengo haya kwa kutangaza bidhaa zetu hasa za vyakula kwa mataifa yenye uhitaji wa bidhaa hizo,” alifafanua.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim alisema kuwa Tanzania ina bidhaa nyingi ya kuziuza kwenye soko la Korea na kutolea mfano mchele wa Kyela kuwa ni bidhaa nzuri kwenye soko hilo.

viungo vya binadamu vyakamatwa jijini dar (wadau mtuwie radhi kwa picha hiza za kutisha).

 Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika  mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
 Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za miili

Sunday, July 20, 2014

WALIMU WANAOTAKIWA KUJIUNGA NA JKT WATAJWA

Hatimaye jeshi la kujenga taifa limetangaza majina ya walimu ambao wanatakiwa kupitia jkt kwa ajili ya mafunzo MAALUM kama ilivyo kwa kidato cha sita,yajulikanayo kama mafunzo kwa  mujibu wa sheria.


Walimu waliochaguliwa ni wa ngazi ya cheti ambao wamepangiwa vikosi vya kwenda.
Kuangalia majina hayo tafadhali BOFYA hapo chini;

TAIFA STARS NGOMA NZITO NA MSUMBIJI UWANJA WA TAIFA

 Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Msumbiji katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 
Mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akiwa katikati ya mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 


Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wa kuwania tiketi ya Fainali za Afrika zitakazofanyika nchini Morocco mwakani. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2. 
 Thomas Ulimwengu  akichuana na beki wa Msumbiji, Josemar Machaisse.

 Huniwezi...Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior.
 Mshambuliaji wa Stars, Khamis Mcha akiwa katika harakati za kufunga goli.
 Golikipa wa Stars, Deogratius Munishi akishangilia balo la pili la 
Taifa Stars kwa kuonyesha fulana yake iliyokuwa ikisomeka 'Sisi ni Watoto wa Rais Kikwete'.

TANGAZA BIASHARA YAKO SASA KWA BEI NAFUU. KWA MAWASILIANO ZAIDI: -

Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd,
Mpalule Shaban
P.o Box:8017
Dar Es Salaam
+255-767-869133
+255-713-869133
+255-789-167937
www.missdemokrasiatanzania@yahoo.com
www.missdemokrasia.blogspot.com
www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com
www.missdemokrasiatanzania.com
www.facebook.com/mchimati
www.shaabanmpalule.blogspot.com
Thank you very much everyone for your cooperation advanced, God help us obtain power, be more stable, who are all God's blessings, and you who named blessing, ask God to give you strength very intelligent to realize the proper way to enter heaven. networks continue to enjoy our good services and advertising at affordable prices, give us a call or send an email, you can also call.MISS DEMOCRACY TANZANIA, very soon.
  • You like this.

RAIS KIKWETE: TANZANIA HAITATUMIA NGUVU ZA KIJESHI KUMALIZANA NA MALAWI KATIKA MGOGORO WA MPAKA WA ZIWA NYASA.

 
Rais Jakaya Kikwete akisalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Majimaji Songea kuhutubia siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Ruvuma katikati ya wiki. (Picha na Ikulu).

RAIS Jakaya Kikwete amesema kamwe Tanzania haitatumia nguvu kumaliza mvutano kati yake na Malawi kuhusu mpaka kati ya nchi hizo, huku akiongeza kuwa, Tanzania haioni mantiki ama busara yoyote kuingia vitani na nchi yoyote jirani kwa sababu yoyote ile.

Alitoa uhakikisho huo kwa Malawi na nchi nyingine jirani wakati alipohutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa mjini Mbamba Bay, Mji mkuu wa Wilaya mpya ya Nyasa, juzi. Mji huo uko kwenye pwani ya Ziwa Nyasa.

Rais Kikwete ambaye alikuwa anasemea juhudi za kutafuta ufumbuzi wa suala la mpaka kati ya Tanzania na Malawi, alisema: “Nataka kuwatoeni wasiwasi. Hakuna sababu ya vita.Laleni usingizi bila wasiwasi, kuleni samaki wenu kwa sababu Tanzania haioni busara ya vita.”

“Tanzania haiwezi kutumia nguvu kupata suluhisho la mvutano wa mpaka. Tuna uwezo wa kupata jawabu la tatizo hilo bila kutumia njia ya vita. Tanzania haioni busara hiyo ya vita. Tuna uwezo wa kupata ufumbuzi kwa njia ya majadiliano. Na wala msimamo huo siyo kwa mpaka wetu na Malawi pekee bali kwa mipaka yote ya Tanzania,” alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete pia ameelezea juhudi ambazo zimekuwa zinafanywa na Tanzania kutatua tatizo hilo la mpaka ikiwa ni pamoja na kuliomba jopo la Marais wastaafu kusaidia kutafuta jawabu la mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Marais hao Joachim Chissano wa Msumbiji, Festus Mogae wa Botswana na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini wanasaidiwa na jopo la Kimataifa la mabingwa wa Sheria katika kazi yao hiyo.

Rais pia amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Nyasa kuwa ahadi na mpango wa Serikali kununua na kuweka meli mpya katika Ziwa Nyasa uko pale pale na kwamba mipango inafanywa ya kuhamisha chelezo cha kujengea meli kutoka Mwanza kwenye Ziwa Victoria kuipeleka Itungi, Kyela, Mbeya ili kuanza ujenzi wa meli hiyo.

Rais ambaye katika Kampeni ya Uchaguzi Mkuu Mwaka 2010 aliahidi ununuzi wa meli tatu za kutoa huduma katika maziwa makuu ya Tanzania ya Victoria, Tanganyika na Nyasa amesema kuwa kiasi cha Sh bilioni 23 zimetengwa tayari kwa ajili ya kuanza ujenzi wa meli hiyo.

Amesema kuwa michoro ya meli hiyo ya Ziwa Nyasa imelazimika kubadilishwa kidogo kwa sababu ya ukweli kuwa ziwa hilo lina mawimbi makali na huchafuka mara kwa mara tofauti na maziwa Victoria na Tanganyika.

Rais Kikwete pia amewaambia wananchi kuwa Serikali inaendelea na mipango ya kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay ili kuzidi kufungua ukanda wa Mtwara na kuweza kubeba chuma na makaa ya mawe kutoka Liganga na Mchuchuma, maeneo yaliyoko katika Mkoa wa jirani wa Njombe na wilaya jirani za Nyasa na Ludewa katika Mkoa huo wa Njombe.

Kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara, Rais Kikwete ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Ruvuma, Rais Kikwete alikuwa na shughuli nyingi katika Wilaya ya Nyasa ambako amezindua Daraja la Ruhekei lililoko katika Kijiji cha Mkalole, kilomita nane kutoka mjini Mbamba Bay.

Alisema ujenzi wa daraja hilo ambalo lina sehemu tatu limejengwa kisasa kabisa ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mbinga, Wilaya ya Mbinga kwenda Mbamba Bay, Wilaya ya Nyasa.

“Ni kweli Mwaka 2005 wakati wa kampeni ya Uchaguzi Mkuu nilishindwa kuvuka hapa kwa sababu daraja lilivunjika lakini ujenzi huu wa kisasa ni kwa sababu tunajiandaa kujenga barabara ya lami kuunganisha Mbinga na Mbamba Bay,” Rais Kikwete amewaambia wananchi kwenye daraja hilo.

Rais Kikwete pia ameweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Nyasa katika Kijiji cha Kilosa kilichoko karibu na Mbamba Bay na amezindua usambazaji wa umeme katika vijiji vya Wilaya ya Nyasa. Rais Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani Ruvuma.HABARILEO

AROBAINI YA JAMBAZI LILILOKUWA LIKIJIDAI NI NGULI WA TANESCO MIKONONI MWA POLISI-

10500539_819006161445574_7780628803053090260_n
Pichani juu na chini ni Kishoka wa Tanesco aliyekamatwa Mlimani City.

TAPELI lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.

Kwa mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa tapeli huyo alifika asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye GPS yao kuwaUmeme hauendi vema.

“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.

Na kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuitePolisi, basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme, nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.

Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.
10417599_819006198112237_2101442257557265538_n  
Hapa likiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.