TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Sunday, November 2, 2014
Dk Shein ashuhudia sherehe za KMKM Ushindi Misimu Miwili
SUNDERLAND AFC NA SYMBION POWER WASHEREHEKEA UIDHINISHAJI WA UJENZI WA UWANJA MPYA WA MICHEZO YA UMMA JIJINI DAR-ES-SALAAM.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete
(kulia) akiwaonyesha jezi yenye jina la Tanzania kwa wageni waalikwa
pamoja na wananchi waliohudhuria hafla ya kutoa Kibali kwa ajili ya
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la
Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Biashara wa Chama cha Michezo cha Sunderland, Bi. Gary Hutchinson
akimkabidhi zawadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa
Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutoa Kibali chake kwa ajili
ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya
Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014
eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Biashara wa Chama cha Michezo cha Sunderland, Bi. Gary Hutchinson
akitoa maelezo machache kabla ya kumkaribisha rasmi Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya
kutoa hotuba pamoja na kutoa Kibali chake kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja
wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth
Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo
Chekundu jijini Dar es Salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Symbion Bwana Paul Hinks akitoa maelezo yake juu ya
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la
Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi akitoa maelezo machache
kabla ya kumkaribisha rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya kutoa hotuba pamoja na
kutoa Kibali chake kwa Chuo cha Michezo cha Sunderland kwa ajili ya
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
01 Novemba, 2014.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Prof. Jakaya Kikwete amevitaka Vilabu vya mpira wa miguu nchini
kuwekeza katika timu za vijana wadogo walio chini ya umri wa miaka 18
ili viweze kuwa na mafanikio ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Rais
Prof. Kikwete leo jijini Dar es saam alipokuwa akizindua ujenzi wa kituo
cha michezo cha vijana wadogo waliochini ya miaka 18 kinachojengwa
nchini eneo la Kidongo Chekundu manispaa ya Ilala.
“Katika nchi yetu, timu ya soka
ya taifa haifanyi vizuri na michezo mingine nayo vivyo hivyo, vilabu
mbalimbali vya michezo navyo havifanyi vizuri katika michezo yao ya
ndani na nje” alisema Prof. Kikwete.
Prof. Kikwete aliendelea kusema
“Kiini cha timu yetu ya soka ya taifa na vilabu vyetu kutokufanya vizuri
katika mashindano, haviwekezi katika vijana wadogo”.
Katika kufanikisha adhima ya
kuwa vilabu na timu ya taifa ya mpira wa miguu kuwa na mafanikio, Rais
Kikwete amewaagiza viongozi Shirikisho la Mpira wa Miguu na wa vilabu
vya mpira wa miguu nchini watekeleze majukumu yao ipasavyo ili soka la
Tanzania liwe la mafanikio kwa wachezaji mmoja mmoja na taifa kwa
ujumla.
Aidha, amelishauri Shirikisho la
mpira wa miguu nchini liweke utaratibu ambao utailazimu kila timu kuwa
na timu ya vijana wadogo kama ilivyo katika mataifa mengine duniani
ambapo kwa mataifa hayo, suala la kuwa na timu ya vijana wadogo na
uwanja wao sio la hiyari.
Kwa upande wake Kurugenzi
Mtendaji wa Timu ya soka ya Sanderland ya nchini Uingereza ambao ndiyo
watakaotoa wataalamu wa michezo watakaofundisha katika kituo hicho Bi.
Margaret Byrne amesema kuwa kituo hicho kitakuwa na uwanja wa mpira wa
miguu wa kisasa wenye ukubwa wa mita 100×60, viwanja viwili vya mpira wa
kikapu, sehemu ya kuegesha magari 20 na kituo cha daladala, kiwanja cha
kuchezea watoto.
Bi. Margaret alisisitiza kwa
ndani ya kituo hicho, kutakuwa pia na jingo la utawala, vyumba vine vya
wachezaji kubadilishia nguo vikiwa na vyoo na bafu, vyumba viwili vya
wafanyakazi pamoja na chumba cha chakula ambacho kitaendana na madhari
ya kituo hicho.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Symbion ya nchini Marekani Paul Hinks amesema kuwa kampuni
yake iko mstari wa mbele na wataendelea kushirikiana na Tanzania katika
masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kukuza sekta ya michezo nchini kwa
kujenga kituo cha soka kwa vijana wadogo.
Ujenzi wa kituo hicho
ulizinduliwa na Rais Kikwete kwa kupanda mti wa mnazi ikiwa ni alama ya
kuashiria kuanza ujenzi huo rasmi ambao unatarajiwa kukamilika mapema
mwakani 2015 ambapo alibainisha kuwa kuwa siku ya Oktoba Mosi mwaka huu,
imekuwa ni siku ya aina ya kipekee ambayo inafungua ukurasa mpya katika
historia ya michezo nchini.
WAZIRI WA AFYA MH. SEIF RASHIDI AZINDUA RASMI GHETTO RADIO KATIKA HOSIPITALI YA TEMEKE JIJINI DAR.
Waziri
wa Afya Mh. Seif Rashid akiongea na Wauguzi wa Hospitali teule ya Mkoa
wa Temeke, Wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm pamoja na wadau
mbalimbali wakati wa uzinduzi Rasmi wa Radio hiyo, ambayo lengo lake ni kuwakomboa vijana wa Mtaani pamoja na vipindi vingine vya kuelimisha Jamii
na Burudani, Pia amewashukuru kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali
ambavyo vitasaidia katika Hospitali hiyo Tarehe 1.11.2014
Mkurugenzi
wa Sibuka George Ndagali akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Ghetto Radio ya Sibuka Fm iliyo fanyika katika katika Hosipitali Teule
ya Mkoa wa Temeke Ambapo Ghetto Radio Imeweza kufunguliwa Rasmi Katika
Mkoa huo nakuweza kutoa Msaada Vifaa Mbalimbali pamoja na Madawa Ambavyo
Vyote kwa ujumla vimegharimu kiasi Cha Shilingi Milioni sita na Laki
sita.
Mkurugenzi
wa
Ghetto Radio Matt Brouwer akizungumza neno wakati wa uzinduzi wa Ghetto
Radio ya Sibuka Fm Ambapo Bw.Brouwer Alisema kuwa Ghetto Radio
ilianzishwa nchini Kenya Miaka Sita iliyopita nakuweza kuwasaidia vijana
mbalimbali Hivyo wameweza kuingia Nchini Tanzania Ilikuendeleza kuwapa
vijana Fursa Na elimu INayo Tolewa na Kituo Hicho Kwa Hapa Nchini
Mganga
Mkuu wa Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke Amaani K. Malima akitoa neno
la Shukurani kwa Timu nzima ya Ghetto Radio ya Sibuka Fm kwa kufanya
uzinduzi wa Radio yao katika Hospitali hiyo pia kutoa Msaada wa vitu
mbalimbali vitakavyo saidia katika eneo hilo.
Meneja wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Edward Lukaka akitoa maelezo machache ya malengo ya Radio hiyo pia kueleza mikakati ya kuendelea kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba katika Vituo zaidi vya Afya.
Mkurugenzi
wa kituo cha afya cha Iran Nchini Tanzania Dkt. Farhad Arjomandi
akiwashukuru Ghetto Radio ya Sibuka FM kwa kuanzisha Kituo hicho pia na
wao wametoa vifaa vya matibabu kwa ajili ya kushiriki uzinduzi huo wa
Radio
Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Dar es salaam Leonard Masonu akitoa neno la Shukurani
Hivi
ni Baadhi ya vitu ambavyo vimetolewa na Ghetto Radio ya Sibuka Fm
katika Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke wakati wa uzinduzi Rasmi wa
Radio hiyo
Waziri
wa Afya Mh. Seif Rashid akikabidhiwa Rasmi msaada wa Vifaa na Vitu
mbalimbali vitakavyo tumika katika Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke
kutoka kwa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Baadhi ya Wadau mbalimbali walioshiriki katika Sherehe hiyo ya Uzinduzi Rasmi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Baadhi ya Wauguzi wakiwa katika uzinduzi huo Rasmi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Wafanyakazi
wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm pamoja na wadau mbalimbali wakijiandaa
kuelekea kutoa Msaada wa vitu mbalimbali katika vyumba vya wagonjwa
Wakiwa wanaelekea Wodini
Kulia
ni Mkurugenzi wa Sibuka George Ndagali akiwa katika Wodi ya watoto
kukabidhi zawadi za watoto na mama zao, katikati ni Mwanamuziki Mkongwe
wa Bongo Flava Juma Nature ambaye ni Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Juma Nature akiwa anatandika Shuka moja wapo katika Wodi ya watoto kuashiria kukabidhi mashuka hayo.
Baadhi ya Timu ya wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
SHUTUMA DHIDI YA TFF
Oktoba 31 mwaka
huu kupitia vyombo vya habari Wakili Damas Ndumbaro alitoa shutuma
mbalimbali dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Tunapenda kuuleza umma wa Watanzania yafuatayo;
1.Hukumu dhidi ya Wakili Ndumbaro ilitolewa na chombo halali kwa mujibu wa Katiba ya TFF. Hivyo, TFF inatoa tahadhari kwa wanafamilia wa mpira wa miguu kutomhusisha Wakili Ndumbaro katika masuala ya mpira wa miguu katika kipindi hiki anachotumikia adhabu.
2.Hadi sasa TFF haijapokea rufani yoyote kutoka kwa Wakili Ndumbaro. Hii ni kwa kuwa kupitia barua yake kwa TFF aliagiza asikabidhiwe nyaraka yoyote kutoka TFF hadi Oktoba 30 mwaka huu, hivyo hukumu ya Kamati ya Nidhamu dhidi yake alikabidhiwa Oktoba 30 mwaka huu. Alichokifanya Wakili Ndumbaro ni kuleta TFF barua ya kusudio la kukata rufani.
3.Tuhuma za ubadhirifu wa TFF zilizotolewa na Wakili Ndumbaro si za kweli. TFF inatafakari hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua dhidi ya tuhuma hizi.
4.Mkataba wa TFF na TBL:
TFF inapenda kuwahakikishia wadau wa mpira wa miguu kuwa hakuna ubadhirifu wa aina yoyote katika matumizi ya fedha za mkataba wa TFF/TBL. TFF ingependa itoe kwa umma ufafanuzi wa vipengele vya mkataba huo na jinsi unavyoendeshwa lakini masharti ya mkataba huo (confidentiality clause) yanatuzuia kufanya hivyo.
1.Hukumu dhidi ya Wakili Ndumbaro ilitolewa na chombo halali kwa mujibu wa Katiba ya TFF. Hivyo, TFF inatoa tahadhari kwa wanafamilia wa mpira wa miguu kutomhusisha Wakili Ndumbaro katika masuala ya mpira wa miguu katika kipindi hiki anachotumikia adhabu.
2.Hadi sasa TFF haijapokea rufani yoyote kutoka kwa Wakili Ndumbaro. Hii ni kwa kuwa kupitia barua yake kwa TFF aliagiza asikabidhiwe nyaraka yoyote kutoka TFF hadi Oktoba 30 mwaka huu, hivyo hukumu ya Kamati ya Nidhamu dhidi yake alikabidhiwa Oktoba 30 mwaka huu. Alichokifanya Wakili Ndumbaro ni kuleta TFF barua ya kusudio la kukata rufani.
3.Tuhuma za ubadhirifu wa TFF zilizotolewa na Wakili Ndumbaro si za kweli. TFF inatafakari hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua dhidi ya tuhuma hizi.
4.Mkataba wa TFF na TBL:
TFF inapenda kuwahakikishia wadau wa mpira wa miguu kuwa hakuna ubadhirifu wa aina yoyote katika matumizi ya fedha za mkataba wa TFF/TBL. TFF ingependa itoe kwa umma ufafanuzi wa vipengele vya mkataba huo na jinsi unavyoendeshwa lakini masharti ya mkataba huo (confidentiality clause) yanatuzuia kufanya hivyo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
alikutana na klabu za Ligi Kuu na kuzielekeza zikae na kujadili kanuni
za Ligi, kisha zipendekeze maboresho ili yajadiliwe katika kikao kijacho
cha Kamati ya Utendaji.
TFF inapenda kuchukue fursa hii
kusisitiza umuhimu wa kufuata mifumo tuliyojiwekea katika kutatua
matatizo/kero zetu mbalimbali, utulivu ni muhimu katika kuendeleza mpira
wa miguu.
TANZANIA NA BURUNDI ZA SAINI MKATABA WA MIAKA 50 KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA MRADI WA RUSUMO
Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania , Profesa,
Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi,
Come Manirakiza.
Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania , Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto) na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, Come Manirakiza wakisaini mkataba huo.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto),
akibadilishana hati na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi,
Come Manirakiza, baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka 50 wa
usafirishaji wa umeme kutoka Mradi wa Rusumo kwenda nchini humo katika
hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Mradi huo unazihusisha nchi tatu
za Tanzania, Rwanda na Burundi.
Hapa mkutano wa maofisa wa Tanaznia na Burundi ukiendelea.
Maofisa wa Tanzania wakiwa kwenye hafla hiyo ya
kusaini mkataba huo.
Maofisa wa Burundi na Tanzania wakiwa katika
hafla hiyo.
Maofisa wa Burundi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Maofisa wa Tanzania wakiwa kwenye tukio hilo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania , Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto) na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, Come Manirakiza wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa nchi hizo mbili wanahusika na wizara hiyo.
…………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
SERIKALI
ya Tanzania na Burundi zimesaini mkataba wa miaka 50 wamakubaliano wa
mradi wa pili wa kusafirisha umeme utakaozalishwa kwenye kituo cha
Rusumo.
TANZANIA NA BURUNDI ZA SAINI MKATABA WA MIAKA 50 KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA MRADI WA RUSUMO
Awali
Tanzania, Burundi na Rwanda zilisaini mkataba wa kwanza wa mradi wa
kituo cha kuzalisha umeme cha rusumo chenye mega watt 80, kilichopo
wilayani Ngara, Mkoani Kagera, mwaka 2013 ambacho kiligharimu takribani
dola za kimarekani milioni 340 zilizotolewa na benki ya Dunia.
Akizungumza
Dar es Salaam jana baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa, Sospeter Muhongo, alisema mkataba huo umezihusisha nchi
mbili ambapo alibainisha kuwa kupitia mradi huo ambao umeanza katika
sehemu ya mwisho ya kutekeleza mradi wa kwanza ulioanza mwaka jana yapo
baadhi ya maeneo nchini yatapata umeme.
Alisema kupitia mradi huo nchi itaweza kuimarisha grid ya Taifa na kupunguza tatizo la umeme kwenye maeneo mengi nchini.
Waziri
Muhongo aliongeza kuwa pamoja na hatua hiyo pia kuitia mradi huo
utaajiri wafanyakazi kutoka nchi zote tatu na hata wa mataifa mwengine
ambapo alibainisha kuwa kwa sasa katika kituo cha mto rusumo wapo
walioajiriwa kutoka nchi husika na miradi hiyo na mataifa mengine.
Kuhusu
ujenzi wa mfumo wa usafirishaji umeme alisema kila nchi itajitegemea
katika kusafirisha umeme na kubainisha kuwa Tanzania itajenga mfumo huo
kuanzia miaka michache ijayo.
Hata hivyo Prof. Muhongo hakubainisha kiasi halisi kitakacho tumika kuendeshea mradi huo wa wamu ya pili
WAZIRI MKUU MIZENGIO PINDA KATIKA HAFLA YA KUCHANGIA MADAWATI
PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO, MAELEZO
Subscribe to:
Posts (Atom)