Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwahutubia wageni waalikwa, wafanyakazi mbalimbali wa Kampuni ya
Symbion pamoja na wananchi wakati wa hafla ya kutoa Kibali chake kwa
Chuo cha Michezo cha Sunderland kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo
wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio
hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete
(kulia) akiwaonyesha jezi yenye jina la Tanzania kwa wageni waalikwa
pamoja na wananchi waliohudhuria hafla ya kutoa Kibali kwa ajili ya
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la
Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
wa Biashara wa Chama cha Michezo cha Sunderland, Bi. Gary Hutchinson
akimkabidhi zawadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa
Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutoa Kibali chake kwa ajili
ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya
Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014
eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
wa Biashara wa Chama cha Michezo cha Sunderland, Bi. Gary Hutchinson
akitoa maelezo machache kabla ya kumkaribisha rasmi Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya
kutoa hotuba pamoja na kutoa Kibali chake kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja
wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth
Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo
Chekundu jijini Dar es Salaam. Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Symbion Bwana Paul Hinks akitoa maelezo yake juu ya
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la
Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi akitoa maelezo machache
kabla ya kumkaribisha rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya kutoa hotuba pamoja na
kutoa Kibali chake kwa Chuo cha Michezo cha Sunderland kwa ajili ya
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
01 Novemba, 2014.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Prof. Jakaya Kikwete amevitaka Vilabu vya mpira wa miguu nchini
kuwekeza katika timu za vijana wadogo walio chini ya umri wa miaka 18
ili viweze kuwa na mafanikio ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Rais
Prof. Kikwete leo jijini Dar es saam alipokuwa akizindua ujenzi wa kituo
cha michezo cha vijana wadogo waliochini ya miaka 18 kinachojengwa
nchini eneo la Kidongo Chekundu manispaa ya Ilala.
“Katika nchi yetu, timu ya soka
ya taifa haifanyi vizuri na michezo mingine nayo vivyo hivyo, vilabu
mbalimbali vya michezo navyo havifanyi vizuri katika michezo yao ya
ndani na nje” alisema Prof. Kikwete.
Prof. Kikwete aliendelea kusema
“Kiini cha timu yetu ya soka ya taifa na vilabu vyetu kutokufanya vizuri
katika mashindano, haviwekezi katika vijana wadogo”.
Katika kufanikisha adhima ya
kuwa vilabu na timu ya taifa ya mpira wa miguu kuwa na mafanikio, Rais
Kikwete amewaagiza viongozi Shirikisho la Mpira wa Miguu na wa vilabu
vya mpira wa miguu nchini watekeleze majukumu yao ipasavyo ili soka la
Tanzania liwe la mafanikio kwa wachezaji mmoja mmoja na taifa kwa
ujumla.
Aidha, amelishauri Shirikisho la
mpira wa miguu nchini liweke utaratibu ambao utailazimu kila timu kuwa
na timu ya vijana wadogo kama ilivyo katika mataifa mengine duniani
ambapo kwa mataifa hayo, suala la kuwa na timu ya vijana wadogo na
uwanja wao sio la hiyari.
Kwa upande wake Kurugenzi
Mtendaji wa Timu ya soka ya Sanderland ya nchini Uingereza ambao ndiyo
watakaotoa wataalamu wa michezo watakaofundisha katika kituo hicho Bi.
Margaret Byrne amesema kuwa kituo hicho kitakuwa na uwanja wa mpira wa
miguu wa kisasa wenye ukubwa wa mita 100×60, viwanja viwili vya mpira wa
kikapu, sehemu ya kuegesha magari 20 na kituo cha daladala, kiwanja cha
kuchezea watoto.
Bi. Margaret alisisitiza kwa
ndani ya kituo hicho, kutakuwa pia na jingo la utawala, vyumba vine vya
wachezaji kubadilishia nguo vikiwa na vyoo na bafu, vyumba viwili vya
wafanyakazi pamoja na chumba cha chakula ambacho kitaendana na madhari
ya kituo hicho.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Symbion ya nchini Marekani Paul Hinks amesema kuwa kampuni
yake iko mstari wa mbele na wataendelea kushirikiana na Tanzania katika
masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kukuza sekta ya michezo nchini kwa
kujenga kituo cha soka kwa vijana wadogo.
Ujenzi wa kituo hicho
ulizinduliwa na Rais Kikwete kwa kupanda mti wa mnazi ikiwa ni alama ya
kuashiria kuanza ujenzi huo rasmi ambao unatarajiwa kukamilika mapema
mwakani 2015 ambapo alibainisha kuwa kuwa siku ya Oktoba Mosi mwaka huu,
imekuwa ni siku ya aina ya kipekee ambayo inafungua ukurasa mpya katika
historia ya michezo nchini.
No comments:
Post a Comment