Wasanii Luci Marphy Mmarekani (kushoto) na Anna Mwalagho kuoka Kenya wakiimba wimbo wa Taifa.
Bwana na Bibi Rick Tingling wakiwashukuru watu kwa kuja kumuenzi
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambayo hiyo jana siku ya Jumapili
Novemba 2, 2014 ilikua ni kumbukumbu ya 6 tangia bwn. Rick Tingling
alipoanzisha kumbukumbu za Mwalimu Nyerere mwaka 2009 hapa DMV. Yeye
bwn. Tingling ni Mmarekani aliyemjua Mwalimu Nyerere kwa kusoma vitabu
vyake na kuanza kumfuatilia na kutambua kwamba Mwalimu Julius Nyerere
ni kiongozi asiyekua na mfano na ambaye huwezi kumlinganisha na kionozi
yeyeyote hapa Dunia si zama hizo au wakati huu tulio nao sasa. Bwn. Rick
Tingling amesema ataendelea kumenzi Mwalimu Julius Nyerere kila mwaka.
Dr. John Rutayuga ambaye ni CEO wa Ukimwi Orphans Assistance
akielezea kazi ya kikundi hicho inayofanya nchini Tanzania na baadae
kuelezea kuhusu Mwalimu Julius Nyerere.
Msanii wa mashairi Anna Mwalagho kutoka Kenya ambaye ni mkaazi wa
DMV akitoa shairi la I have a dream lililoelezea utajiri wa Africa na
kwamba ndoto yake siku moja ni Africa itakua moja na itaitwa United
State of Africa.
Mama Elvira William ambaye ni mkurugenzi mkuu wa AHEAD wanaosaidia
maswala ya afya na elimu nchini Tanzania tangia mwaka 1974 wakati mume
wake Baba Felton William alipoambwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere kwenda Tanzania kuasaidia maswala ya afya katika hospiali ya
Bugando baada ya miaka 2 na nusu walirudi Marekani na mwaka 1985
walirejea tena Tanzania kwa mwaliko wa aliyekua Waziri wa Afya Mhe.
Chiduo na kufanya kazi za afya Shinyanga.huku mama William akisaidia
kufundisha katika vijiji mkoani Shinyanga. Mwaka 2002 walirudi tena
Tanzania na kwa sasa wapo Kisarawe wakiendelea kuasadia katika nyanja ya
afya na elimu. Mama William baada ya kueleza kazi zake anazofanya
Tanzania alimalizia kw kusoma wasifu wa Mwalimu Julius Nyerere
Bwn. Melvin Deal akifanya tambiko kabla ya kuanza kwa kukmbukumbu
ya Mwalimu Julius Nyerere kulia ni Baba C maarufu kama msimulizi wa
hadithi.
Bwn.
Melvin Deal ambaye ni mpiga ngoma wa siku nyingi akielezea maana ya
tambiko ambalo baadae alilifanya ukumbini hapo kama ilivyokua likifanywa
na mababu zetu enzi hizo.
No comments:
Post a Comment