Mahmoud Ahmad Arusha
Wanajumuiya ya Afrika ya Mashariki wametakiwa
kuwa na mashirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo viongozi kuangalia
utangamano wa kisiasa badala ya utengamano wa kiuchumii pekee.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi dkt Richard Sezibera wakati akifungua Tamasha la pili la zinduka linalowashirika Wadau wa Maendeleo kutoka nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki linalofanyika kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Dkt Sezibera alisema kuwa Maendeleo ya kudumu kwenye jumuiya hiyo hayaewezi kuja kwenye utangamano wa kiuchumi pekee bila ya wanasiasa kuingiza jumuiya kwenye sula la utangamano wa kisiasa kwani itapelekea kuwa na maendeleo ya kudumu na yenye tija kwa jumuiya hiyo
Akawata wakazi wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki kujenga utengamano kwenye nyanja mbalimbali za kimaendeleo kwani hatua hiyo itasaidia kwa watunga sera kufanya maamuzi kwa haraka na kuisaidia jumuiya kupata maendeleo endelevu.
“Suala hapa si nani wakujiuliza ila tunatakiwa kujenga utangamano wenye nguvu utakaopelekea kukua kwa uchumi wa nchi zetu na jumuiya kwa ujumla wake”Alisema balozi Sezibera.
Alisema kuwa nchi ya Kenya haiwezi kuimeza jumuiya ya Afrika Mashariki kwani haina Tumbo la kuimeza jumuiya hiyo kwanini imekuwa ikihofiwa kuwa itaweza kuimeza jumuiya hiyo kutumiza Malengo yetu bila ya kuangalia mipaka ya nchi zetu.
Kwa Upande wake Diwani wa Ngarenaro Isaya Doita kwa niaba ya Meya wa jiji la Arusha alisema kuwa suala la utangamano wa Afrika Mashariki si wa viongozi wa jumuiya pekee bali ni la wanajumuiya wote katika dhana nzima ya kujiletea Maendeleo ya kudumu.
Akawataka viongozi kuangalia suala zima la utangamano wa kisiasa kwa maendeleo ya jumuiya na wanajumuiya mmoja mmoja kwani tuangalie utaifa wetu kama waafrika bila ya kujali nchi zetu pekee.
“Tuunganishe Afrika kwa vitendo tuache siasa ili kupata Maendeleo Endelevu kwani utambulisho wetu nje ya bara la afrika ni uafrika wetu na jumuiya yetu ya Afrika ya Mashariki kama inataka Maendeleo suala la utangamano wa kisiasa halikwepeki”alisema Doita
Naye Muhadhiri wa chuo kikuu cha Suza Amour Abdalla Khamis Alisema kuwa suala la lugha ya kiswahili kupewa kipaumbele kwenye matamasha mbali mbali limekuwa ni kwa watu wa chini ila viongozi wanajukumu la kukipa umuhimu mkubwa kiswahili kokote wanapohutubia.
Alisema kuwa suala la lugha yetu ya kiswahili kutopewa umuhimu katika masomo si kwamba haliwezi kufundishika kwenye mitaala ya masomo yetu bali ni kutokana na kutopewa umuhimu wa kipekee kwa ajili ya maendeleo yetu.
Aidha mhadhiri msaidizi wa SUZA Omary Suleiman alisema kuwa Kiswahili ni muhimu kwa Mtangamano wa Afrika ya Mashariki kwa Maendeleo Endelevu ya wanajumuiya ya Arfrika ya Mashariki.
Suleiman alisema kuwa kama tunataka kuiangausha mipaka ya Afrika Mashariki ni lazima kuzinagalia na kuziweka pembeni tofauti zetu za mipaka kwa maendeleo yetu kama jumuiya.
“Wote ni waafrika matatizo yetu yanafanana ila bila ya kuondoa fikra za kikoloni za utengano na kuamua kuungana basi tutafika kwenye maendeleo yetu”alisema Suleiman
Tamasha la Zinduka limekuwa likiwashirikisha wadau mbali mbali kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wanasheria,wasanii,na sekta nyinginezo wakizungumzia mtangamano wa Maendeleo ya kudumu ya Afrika Mashariki.

No comments:
Post a Comment