Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwahutubia wageni waalikwa, wafanyakazi mbalimbali wa Kampuni ya
Symbion pamoja na wananchi wakati wa hafla ya kutoa Kibali chake kwa
Chuo cha Michezo cha Sunderland kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo
wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio
hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete
(kulia) akiwaonyesha jezi yenye jina la Tanzania kwa wageni waalikwa
pamoja na wananchi waliohudhuria hafla ya kutoa Kibali kwa ajili ya
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la
Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi
wa Biashara wa Chama cha Michezo cha Sunderland, Bi. Gary Hutchinson
akimkabidhi zawadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa
Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutoa Kibali chake kwa ajili
ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya
Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014
eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi
wa Biashara wa Chama cha Michezo cha Sunderland, Bi. Gary Hutchinson
akitoa maelezo machache kabla ya kumkaribisha rasmi Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya
kutoa hotuba pamoja na kutoa Kibali chake kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja
wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth
Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo
Chekundu jijini Dar es Salaam.Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Symbion Bwana Paul Hinks akitoa maelezo yake juu ya
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la
Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi akitoa maelezo machache
kabla ya kumkaribisha rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya kutoa hotuba pamoja na
kutoa Kibali chake kwa Chuo cha Michezo cha Sunderland kwa ajili ya
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
01 Novemba, 2014.
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Kikwete amevitaka
Vilabu vya mpira wa miguu nchini kuwekeza katika timu za vijana wadogo
walio chini ya umri wa miaka 18 ili viweze kuwa na mafanikio ndani na
nje ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa na Rais Prof. Kikwete leo jijini Dar es saam alipokuwa
akizindua ujenzi wa kituo cha michezo cha vijana wadogo waliochini ya
miaka 18 kinachojengwa nchini eneo la Kidongo Chekundu manispaa ya
Ilala.
“Katika
nchi yetu, timu ya soka ya taifa haifanyi vizuri na michezo mingine
nayo vivyo hivyo, vilabu mbalimbali vya michezo navyo havifanyi vizuri
katika michezo yao ya ndani na nje” alisema Prof. Kikwete.
Prof.
Kikwete aliendelea kusema “Kiini cha timu yetu ya soka ya taifa na
vilabu vyetu kutokufanya vizuri katika mashindano, haviwekezi katika
vijana wadogo”.
Katika
kufanikisha adhima ya kuwa vilabu na timu ya taifa ya mpira wa miguu
kuwa na mafanikio, Rais Kikwete amewaagiza viongozi Shirikisho la Mpira
wa Miguu na wa vilabu vya mpira wa miguu nchini watekeleze majukumu yao
ipasavyo ili soka la Tanzania liwe la mafanikio kwa wachezaji mmoja
mmoja na taifa kwa ujumla.
Aidha,
amelishauri Shirikisho la mpira wa miguu nchini liweke utaratibu ambao
utailazimu kila timu kuwa na timu ya vijana wadogo kama ilivyo katika
mataifa mengine duniani ambapo kwa mataifa hayo, suala la kuwa na timu
ya vijana wadogo na uwanja wao sio la hiyari.
Kwa
upande wake Kurugenzi Mtendaji wa Timu ya soka ya Sanderland ya nchini
Uingereza ambao ndiyo watakaotoa wataalamu wa michezo watakaofundisha
katika kituo hicho Bi. Margaret Byrne amesema kuwa kituo hicho kitakuwa
na uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa wenye ukubwa wa mita 100×60,
viwanja viwili vya mpira wa kikapu, sehemu ya kuegesha magari 20 na
kituo cha daladala, kiwanja cha kuchezea watoto.
Bi.
Margaret alisisitiza kwa ndani ya kituo hicho, kutakuwa pia na jingo
la utawala, vyumba vine vya wachezaji kubadilishia nguo vikiwa na vyoo
na bafu, vyumba viwili vya wafanyakazi pamoja na chumba cha chakula
ambacho kitaendana na madhari ya kituo hicho.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Symbion ya nchini Marekani Paul Hinks
amesema kuwa kampuni yake iko mstari wa mbele na wataendelea
kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo
kukuza sekta ya michezo nchini kwa kujenga kituo cha soka kwa vijana
wadogo.
Ujenzi
wa kituo hicho ulizinduliwa na Rais Kikwete kwa kupanda mti wa mnazi
ikiwa ni alama ya kuashiria kuanza ujenzi huo rasmi ambao unatarajiwa
kukamilika mapema mwakani 2015 ambapo alibainisha kuwa kuwa siku ya
Oktoba Mosi mwaka huu, imekuwa ni siku ya aina ya kipekee ambayo
inafungua ukurasa mpya katika historia ya michezo nchini.
No comments:
Post a Comment