JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI 1. HASSAN ADAMU [84], MKAZI WA ILEMI NA 2. ALPHONCE
MWAKABANA [45] MKAZI WA MWENJELWA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO]
UJAZO WA LITA 10.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
05.11.2014 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO ENEO LA ISANGA,KATA YA
ISANGA,TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI
WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NANI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
MTU MMOJA AMEKAMATWA BAADA YA KUWAUZIA WATU NYAMA YA MBWA.
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA AHADI JESIKAKA [20] MKAZI WA KIJIJI CHA NGYEKYE KWA KOSA LA KUWAUZIA WATU NYAMA YA MBWA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
04.11.2014 MAJIRA YA SAA 13:45HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NGYEKYE,KATA YA
MATEMA,TARAFA YA NTEMBELA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. WATU
WALIOUZIWA NA KUTUMIA KITOWEO HICHO NI 1. ENOCK NSEMWA [52] MKAZI WA
NGYEKYE 2. GEORGE NSEMWA [26],MKAZI WA NGYEKYE NA 3. ANYANDWILE MBWILO
[29] MKAZI WA NGYEKYE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUWA MAKINI HUSUSANI WANAPONUNUA VYAKULA ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA
YA KIAFYA.
Imesainiwa na:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment