TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, November 2, 2014

VIJANA WANAODHANIWA KUWA CCM WAANZISHA VURUGU HADI NGUMI ZAPIGWA WAKATI WA MDAHALO KUHUSU KATIBA MPYA

Jaji Warioba.
VURUGU zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea hivi punde katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.
Vurugu hizo zimezuka baada ya watu waliokuwa na mabango kuvamia ukumbuni hapo na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wanafuatilia mdahalo huo kuwakabili na kuwapa kichapo.
 Baada ya vurugu hizo, mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa moja kwa moja na ITV umesimamishwa kwa muda. 
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambao wapo kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza kabla ya Vurugu kuanza.
  • 2 people like this.
  • Goodluck Haule It is pathetic Ole Ngeeyan
  • Mpalule Shaaban Kwani imekuwaje jamani huko wengine hatujapata yaliyojili UBUNGO PLAZA
  • Goodluck Haule Warioba alikuwa anatoa ufafanuzi kama KATIBA iliyopendekezwa inaendana na maoni ya wananchi, Mara kuna kikundi cha vijana wa baadhi Yao wakiwa na skafu Za CCM waka Toa mabango Yao ya kusifia KATIBA Inayopendekezwa walipo ona haitoshi wakaanza kupiga Kelele ndio chanzo cha vurugu !!Mpalule Shaaban
  • Mpalule Shaaban duh, kwa hiyo baada ya hapo hakuna klichoendelea tena, ama nini kimeendelea baada ya hilo tifu ukizingatia watu wametoka mbali na kuacha shuguli zao, lakini pia kwa mtazamo wako hapo unadhani CCM wanahusika kwa namna yoyote au ni vurugu za hao Vijana tu wasiokuwa na wazazi, wanaitwa Ngunguru afugiki, nini mtazamo wako katika hilo Goodluck Haule
  • Goodluck Haule Wame tumwa hao mkuu sio bure cauz nikama walikuwa wanapewa directives!!Mpalule Shaaban
  • Mpalule Shaaban kwa maana ingine wanataka kuipitisha hiyo KATIBA kwa nguvu za Rangi za Chama chao au kwa nguvu ya Majina ya Erufi za jina la Chama chao? Katiba ni Suala linalohusu Nchi na si jambo la Rangi ya Vyama kwenye Nguo zao ama siyo suala la Kuamua na kupitishwa kirahisi kwa nguvu ya Maamuzi ya Chama Cha Mapinduzi bila kutambua kwamba Suala la KATIBA, bila kuangalia Chama, Dini na Imani ya Mtu itabaki kuwa ndani ya DEMOKRASIA YETU TANZANIA, au hawajasikia yaliyowakuta wengine wa Burkinafasso? hali ndivyo inavyoanza kidoo kidogo ubadilika mwisho wa siku inakuwa ni hatari kubwa, na hii inaweza kutokea kwa Awamu hii maana hali inazidi kuwa mbaya sana kwa TANZANIA. Usikose pia kutembelea. www.shaabanmpalule.blogspot.com
    shaabanmpalule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment