Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MDAU wa muziki wa dansi Tanzania
ambaye pia ni Mchumi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Kata ya Makumbusho,
Yusuphed Mhandeni, amesema kuna haja kubwa wadau kuliunga mkono tamasha
la Handeni Kwetu linalotarajiwa kufanyika Desemba 13, wilayani Handeni,
mkoani Tanga ili kuchochea kasi ya maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Mdau wa muziki wa dansi Tanzania, Yusuphed Mhandeni, pichani.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Mhandeni alisema kitendo cha
kufanyika tamasha hilo na mengineyo makubwa Tanzania,si tu kinachangia
kwa kiasi kikubwa kuitangaza sanaa na utamaduni wa Mtanzania, bali pia kunaleta maendeleo makubwa.
Alisema
tamasha la Handeni linafanyika katika eneo ambalo wananchi wake na
viongozi kwa kiasi kikubwa wanapambania maendeleo, hivyo ni jambo la busara kuendelea kubuni matukio makubwa, sanjari na kushirikiana kwa kiasi kikubwa.
Mhandeni
alisema nyumba za wageni, hoteli, migahawa na vyombo vya usafiri
vinafanya biadhara kubwa kutoka kwa wananchi wanaohudhuria tamasha hilo,
wakiwamo wasanii na vikundi vingi vinavyonufaika kwa uwapo wa tamasha
hilo.
“Naungana na Watanzania wazalendo wakiwamo waandaaji wa tamasha kubwa la Handeni Kwetu, linaloandaliwa chini ya mratibu wake mkuu Kambi Mbwana, huku likipangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu wilayani Handeni mkoani Tanga kwasababu napenda maendeleo ya nchi yetu.
“Wengine
waliunge mkono wakiwamo wafanyabiashara wakubwa, mashirika na kampuni
mbalimbali za Tanzania kwa ajili ya kufaninisha maendeleo ya Taifa letu,
ukizingatia kuwa ili tusonge mbele tunapaswa kuunga mkono juhudi kama
hizi,” alisema Mhandeni.
Mhandeni
ni miongoni mwa wadau wanaolipigia chapuo tamasha la Handeni Kwetu kwa
kupitia mabasi yake ya Phed Trans yanayokwenda Mkata, wilayan Handeni,
bila kusahau SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd
kwa kupitia kitabu chao cha Ni Wakati wako wa Kung’aa, Handeni Kwetu
Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd.
Tamasha
la Handeni Kwetu ni miongoni mwa matukio makubwa ya kiburudani mkoani
Tanga, ambako zaidi ya watu 500 walihudhuria tamasha hilo ambalo kwa
mwaka huu mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa linafanyika kwa mafanikio.
No comments:
Post a Comment