Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Panza
Mwamlima akiongea na uongozi wa Kata ya Kakese katika kikao chake na
uongozi huo kuzungumzia shughuli za maendeleo katika kata hiyo,kushoto
kwa mkuu wa Wilaya ni Afisa mtendaji wa Kata ya Kakese Rebeni Kasomo
aliyeshika kichwa,kulia kwa mkuu wa wilaya ni Kaimu Mkurugenzi wa Mji
Zena Kapama na mwisho ni Kaimu Afisa Katibu Tawala wilaya Reginal
Mhango.
…………………………………………………………………
Na Kiada Kibada- Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza
Mwamlima amewapa changamoto watumishi wa umma kuwa wabunifu kwa kubuni
mbinu zitakazo wasaidia kupambana na changamoto za kimaisha kukabiliana
na mazingira wanayofanyia kazi.
Changamoto za kimazingira
katika utendaji wa kazi kukikabiliana nazo na zitakufanya kuwa mbunifu
na kuweza kukabiliana nazo na mazingira hayo ambapo utapata fikra mpya
na akili itakayo saidia kuwaletea Maendeleo wananchi wanaowatumikia na
wewe mwenyewe.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa
changamoto hiyo wakati akizungumza na watumishi wa Idara ya Elimu,
Afya, kilimo na mifugo Utawala pamoja na vikundi vya kuweka na kukopa wa
Kijiji cha kawanzinge,kakese na mbugani wa kata ya Kakese kwa nyakati
tofauti alipokutana nao katika ziara ya kutembelea,kukagua na kuhimiza
shughuli za maendeleo Kata ya Kakese Halmashauri ya Mji wa Mpanda kisha
kuzungumza na watumishi hao.
Mwamlima akiwa katika Kijiji cha
Kawanzige alikutana na walimu,watumishi wa Idara ya Kilimo, Mifugo na
utawala ambapo katika mazungumzo yao alipokea changamoto mbalimbali
zinazowakabili watumishi hao wa umma katika mazingira yao ya Kazi ya
kila siku hasa kwa wale walioko nje ya makao makuu ya Halmashauri.
Wakiongea katika kikao hicho kwa
nyakati tofauti kwenye ofisi ya Walimu Shule ya Msingi Kawazinge
watumishi hao walimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali za kiutendaji katika kutekeleza majukumu yao ya
kila siku kulingana na mazingira magumu ya kiutendaji wanayotendea kazi.
Baadhi ya changamoto
walizibainisha kuwa ni kuwa kwa upande wa walimu ni upungufu wa
Madawati,Nyumba za Walimu,upungufu wa vitabu vya kiada na ziada,huduma
ya maji safi na salama pamoja na kutosikilizwa na wakuu wao wa elimu
pale wanapoenda kufuatilia stahili zao mbalimbali kwenye ofisi wanapewa
majibu yasiyostahili.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji
wa Kijiji cha Kawanzige Koletha Nyambi alieleza kuwa changamoto katika
kijiji hicho zipo za aina mbalimbali kama walivyoeleza watumishi wenzake
ambapo kubwa ni ukosefu wa nyumba wa watumishi.
Nyambi alitaja changamoto
nyingine kuwa ni upungufu wa vyumba vya madarasa,madawati na huduma ya
maji.akaomba serikali kusaidia kuondoa changamoto hicho hasa kuwajengea
nyumba watumishi ili waweze kuishi jirani na vituo vya kazi kuweza
kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.
Amesema Mtumishi wa umma ambaye
ni mtalaam au kiongozi anapokuwa eneo la kiutendaji akiwahudumia
wananchi hatakiwa kulalamikia mazingira magumu bali anakabilaiana na
changamoto hizon na kutafuta njia ya kutatua changamoto hizo kulingana
na Mazingira anayoishi nayo atumikie kila rasilimali zilizopo kuwasaidia
wananchi kuleta maendeleao.
Awali Afisa Mtendaji wa Kata ya
Kakese Reuben Kasomo alimweleza mkuu wa Wilaya kuwa changamoto
mbalimbali zinazoikabili Kata yake ikiwa ni pamoja na upungufu wa
watumishi hasa katika sekta ya utwala ,walimu,nyumba za kuishi watumishi
, vyumba vya madarasa kwa kwa shule zilizoko kwenye kata yake pamoja na
upungufu wa vitabu vya ziada na kiada,
Mbali ya hilo walieleza hali ya
maandalizi ya upatikaji wa pembejeo za kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo
umekaribia kuanza lakini hadi sasa hawakulima hawajui hatma yao ya
kupata pembejeo watazipataje kwa kuwa hawajaelezwa lolote kulingana na
hali hiyo.
No comments:
Post a Comment