Mwanafunzi wa shule ya msingi Kawanzige wakicheza baada ya kutoka madarasani wakijiburudisha kwa michezo wakati wa mapumziko hapo shuleni.
……………………………………………………………………………
Na Kibada Kibada -Katavi.
Pamoja na Changamoto lukuki
zinazoikabili Shule ya Msingi Kawanzige iliyoko Halmashauri ya Mji wa
Mpanda Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi nje kidogo ya Mji umbali wa
takribani kilometa 30 kutoka mjini bado shule hiyo imeonekana kufanya
vizuri katika matokeo ya elimu ya Msingi kwa mwaka yalitangazwa na
Baraza la mitihani la taifana kushika nafasi ya kwanza kwenye shule
zilizoko kwenye Halamshauri hiyo.
Shule hiyo ambayo imeshika
nafasi ya kwanza kwa Halmashauri ya mji na kuzigalaghaza shule zilizoko
mjini ambazo zinapata kila aina ya mahitaji yote muhimu.
Shule ya Kawanzige yenye idadi
ya walimu kumi kati yao saba wa kiume na watatu wa kike ina Idadi ya
wanafunzi Wanafunzi 484 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, ambapo
wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa wanafunzi 23
kati yao wanafunzi wa kiume walikuwa na wakike
Shule hiyo ilishika nafasi ya
kwanza katika halamshauri hiyo yenye shule 24 na nafasi ya pili kimkoa
kati ya shule 159 nafasi ya 430 kitaifa kati ya shule 15867 za msingi
nchi hivyo kuwa na wastani wa 174,0000.
Matokeo hayo yanaifanya shule
kuwa moja ya shule bora pamoja na kuwa katika mazingira magumu kwa
kutokuwa na vyumba vya madarasa wanafunzi madarasa tofauti kusomea
kwenye chuma kimoja kwa wakati mmoja darasa la tatu na la tano, na wale
wa darasa la kwanza na pili nao kuwa katika darsa moja huku wakiwa
hawana madawati wakika chini changamoto ambayo inahitaji kupatiwa
ufumbuzi.
Mbali ya changamoto hiyo kwa
wanafunzi vitabu vya kiada na ziada ni shida maji hakuna matundu ya vyo
ni shida,na walimu nao wanakabiliwa na changamoto lukuki kama ukosefu wa
makazi bora, nyumba za kuishi hakuna,motisha kidogo kutoka kwa wakuu
wao wa kazi hali iliyopelekea kutoa malalamiko yao kwa mkuu wa wilaya
aliyetembelea shule hiyo kujionea changamoto zinazowakabili na kuwatia
moyo waskate tama wawe na moyo wa kulipenda Taifa lao wakati Serikali
inaendelea kushughulikia madai yao.
Pamoja na changamoto hizo bado
walimu hao hawajakataa tama waliendelea kuchapa kazi kwa ushirikiano
mkubwa na moyo wa kuipenda nchi yao pamoja na kuelewa changamoto
zilizoko mbele yao hali iliyochangia kfanikisha ufaulu huo na kufanya
vizuri huku wakiziacha mbali shule nyingine ambazo zinapata mahitaji
muhimu na zina pata mahitaji muhimu ya huduma za kielimu na pia watoto
wanasoma masomo ya ziada kwa kuwa hata umeme upuo.
Kutokana na hilo mkuu wa wilaya
ya M,panda Paza Mwamlima amemwagiza mkurugenzi kupitia Idara ya Elimu
Halmashauri ya mji kuona namna ya kuweza kuzipatia changamoto ufumbuzi
na kuhakikisha madai na stahili za walimu wanatimiziwa ili waendelee
kuchapa kazi na kulijenga taifa kwa kuelemisha watoto ambao watakuja
kuwa viongozi wa baadaye wa Taifa hili.
No comments:
Post a Comment