Na Mwandishi wetu, Arusha
TANZANIA
imesema ipo tayari kuendeleza juhudi za kimataifa za kupunguza
kuendelea kuliwa kwa tabaka la ozone kwa kuhakikisha kwamba inatunza
misitu na kuwaelimisha wananchi juu ya menejimenti ya misitu hiyo.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge wakati wa kufungua
kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja
wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha.
Alisema
ingawa Tanzania kwa sasa ina hekta milioni 48.1 za misitu na mapori
ambayo sawa ni asilimia 55 ya eneo lake, Tanzania kupitia misitu hiyo
inanyonya zaidi ya tani milioni 76 za hewa ya ukaa ingawa yenyewe inatoa
chini ya tani hizo.
Hata
hivyo alisema kwamba pamoja na juhudi za serikali kuna changamoto kubwa
katika kutunza misitu hiyo ambapo kiwango cha ukataji wa misitu kwa sasa
ni kiasi hekta 372,000 kwa mwaka sawa na asilimia 1.1 ya eneo la ardhi
la nchi.
Katika
hali ya kawaida na endelevu eneo linaloruhusiwa kuvuna kwa mwaka
linaweza kutoa mita za ujazo milioni 42.8 kwa mwaka wakati mahitaji
halisi ni mita za ujazo Milioni 62.3 kwa mwaka.
“Asilimia
92 za mahitaji ni kwa ajili ya nishati kama kuni na mkaa.” Alisema
akionesha changamoto zinazokabili serikali ya Tanzania pamoja na ukweli
kuwa mabadiliko ya tabia nchi tayari yameonesha ukali wake nchini.
Mabadiliko
ya tabia nchi yanayotokana na kuzidi kwa joto katika tabaka la ozone
kumesababisha kupanda kwa bahari wka sentimeta 19 na kusababisha baadhi
ya visiwa katika pwani ya Tanzania kuzama kama cha Maziwe kilichopo
wilaya ya Pangani.
Aidha
alisema keundelea kuyeyuka kwa barafu ni dalili nyingine ya Tanzania
kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi kwa hiyo taifa la Tanzania
linajikita pamoja na mataifa mengine kuhakikisha kwamba programu ya
Umoja wa mataifa ya kuhifadhi misitu inafanikiwa.
Aidha
alisema kwa mazingira ya sasa ambapo tani milioni 1 ya mkaa huzalishwa
nchini kwa mwaka huu nusu yake ikitumika jiji la Dar es salaam na majiji
ya Arusha na Mwanza yakitumia kiasi kinachobaki kunahitaji juhudi za
ziada kuongeza kasi ya upandaji miti kiasi cha hekta 185,00 kwa mwaka
katika kipindi cha miaka 16 ijayo.
Waziri
Binilith alisema pamoja na Tanzania na mataifa mengine ni laizma
kushirikiana katika kupunguza kasi ya ukataji miti katika misitu huku
wananchi wake wakisaidiwa njia nyingine ya kuendesha maisha yao.
Alisema
mikakati ya kutunza misitu ili kupunguza kiwango cha joto duniani pia
itasaidia kunyanyua uchumi wa wananchi, kuondoa umaskini na kutengeneza
mtengamano wa mazingira na ekolojia hasa kwa jamii ambayo inategemea
misitu kuwezesha maisha.
Waziri
huyo aliwataka wadau waliopo katika mkutano huo wa siku mbili kujadili
na kubadilishana uzoefu na kuhakikisha kwamba mkakati wa Umoja wa
mataifa wa kukabiliana na mseleleko wa joto kwa kuwekeza katika
kuhifadhi misitu unafanikiwa.
Umoja
wa Mataifa una mpango wa kuhifadhi misitu unaojulikana kama Reduce
Emissions from Deforestation and Forest Degradation (REDD+) unatarajia
kuanza 2016-2020.
Wakati
huo huo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez, akizungumza awali alishukuru mchango wa Norway katika
kuwezesha utekelezaji wa programu ya UN REDD+ nchini Tanzania na maeneo
mbalimbali duniani.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizotolewa mkutanoni hapo Norway imechangia dola za
Marekani milioni 11 kuwezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Umoja wa
Mataifa katika kufanikisha programu hiyo katika nchi mbalimbali.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akisalimiani na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge alipowasili kwenye
ukumbi wa mikutano. Katikati ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD
Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi
Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la
Chakula na Kilimo Duniani (FAO).
Utoaji
wa hela hizo umeelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kitengo cha kimataifa cha
mabadiliko ya hali ya hewa katika Wizara ya hali ya hewa na mazingira ya
Norway.
Akizungumza
wakati wa kumkaribisha Waziri Dk Binilith Mahenge, wawakilishi
mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa mataifa (– UNDP, UNEP, na
FAO),Sekretarieti ya UN REDD, wajumbe wa bodi ya sera ya UN REDD,
Mashirika yasiyo ya kiserikali, Mwakilishi huyo wa UN alisema mafanikio
yanayopatikana kwa sasa na duniani ni matokeo ya uwezeshaji wa Norway na
wadau wengine katika mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
kwa kuhifadhi misitu.
Alisema
kazi ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha wanatoa msaada wa
kitaalamu na misaada mingine kuiwezesha serikali kutimiza wajibu wake.
Alisema
Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na nchi nyingine 56 duniani wanaounda
UN-REDD wamefanya vyema kuziwezesha nchi hizo kuwa tayari katika
kutekeleza programu husika kwa manufaa ya nchi zao na dunia kwa ujumla.
Alisema
Tanzania kama nchi nyingine duniani zinazoendelea inakumbana na
changamoto kubwa ya kuhifadhi misitu hasa kutokana na wananchi wake
wengi kutegemea sana misitu kwa mambo mbalimbali yanayohusu maisha yao.
Aidha alisema kama taifa lina uwezo mdogo wa kusimamia sera na sheria zinazohusu hifadhi ya misitu.
REDD+
ambayo imeanza kutekelezwa nchini Tanzania mwaka 2008, mikakati ya
utekelezaji wa mkakati huo imefanywa na kupitishwa na Bunge la Tanzania
mwaka 2013.
Kukiwa
na kikosi kazi cha kuwezesha kutekeleza UN REDD+ Tanzania pia
imepongezwa kwa kuanzisha miradi tisa yenye lengo la kuwezesha
utekelezaji wa malengo ya REDD+
Aidha
katika utekelezaji wake serikali imejikita katika vipato vingine kwa
jamii inayoishi karibu au ndani ya misitu kwa kuwa na kilimo
kinacholinda mazingira na ufugaji nyuki.
Alvaro
alisema kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwa sasa UN na serikali ya
Tanzania wanakamilisha awamu ya pili ya UN REDD+ kwa kuangalia uzoefu
uliopatikana katika awamu ya kwanza.
Utekelezaji wa awamu ya pili utafanyika mara tu fedha zitakapopatikana.
Naye
Abbas Kitogo ambaye ni Meneja wa miradi ya nishati na mabadiliko ya
tabia nchi (UNDP) alisema kwamba mkutano huo wa 13 utawezesha
kubadilishana uzoefu wa sekta mbalimbali katika kutunza misitu huku
wananchi wakiendelea kuneemeka.
Alisema
nchini Tanzania kumekuwepo na miradi ya kujenga uelewa, kutengeneza
mpango wa kutekeleza yanayotakiwa kufanywa na kujenga uwezo kwa wadau
ili kujua REDD na kufuatilia athari za utekelezaji wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment