Uongozi waeleza ushirikiano na Facebook ni hatua ya kwanza
OLX, moja ya jukwaa linaloongoza
majukwaa yatoayo habari kwa njia ya mitandao Duniani leo limetangaza
kuingia kwenye soko la Tanzania kwa kupitia mtandao wa kijamii wa
Facebook.
Bw. Thomas Plateng
a, kiongozi wa OLX Kusini mwa
Jangwa la Sahara ameelezea furaha ya kampuni yake kuaza mradi huo. “OLX
imekuwa na mafanikio makubwa kwenye nchi ambazo inapatikana. Kenya
tumefanikiwa kuwaelemisha watu kuhusu ya mtandao wetu kwa asilimia 98
(98%). Hii ina maana kuwa kila mtu anaijua OLX na anaweza kukuambia
inahusika na vitu gani. Tuna tumaini tutapata muamko wa aina hii kutoka
Tanzania,” alisema Bw. Platenga.
Takwimu zinaonyesha kuwa,
inakadiriwa ni asilimia 4.4 (4.4%) ya Watanzania wanapata huduma ya
mtandao (internet) huku Facebook ikiwa ni moja ya huduma inayotumiwa
zaidi. Hii inaashiria kuwa ni fursa ya kuwaunganisha watu wengi na OLX.
“Ushirikiano wa baina ya Facebook
na OLX ni muhimu sana kwetu. Mtandao wetu una mambo mengi ya kutoa, na
tunaamini kwa kutumia njia na taarifa sahihi tutafanya mapinduzi ya
biashara ya mtandaoni Barani Afrika,’’ aliongeza Bw. Platenga.
OLX inapatikana kwenye nchi zaidi
ya 100 Duniani na inatumia lugha 50 tofauti. Hii inasaidia kutafsiri
lugha kwa mamilioni ya watu Ulimwenguni kote kila siku wanaotumia OLX
kununua na kuuza bidhaa, kutafuta kazi au kupangisha nyumba. Zaidi ya
watumiaji tofauti milioni 200 kwa mwezi wanatimiza jumla ya wasomaji wa
ukurasa wa OLX zaidi ya bilioni 11 kwa mwezi au wasomaji wasiopungua
milioni 360 kwa siku hivyo OLX ina matumaini ya kuzidi kukua na kupanua
huduma zake Afrika.
Bw. Platenga alihitimisha kwa
kusema kuwa kuingia Tanzania ilikuwa ni moja ya mkakati muhimu. “Tovuti
yetu Tanzania imeshaanza kufanya kazi na sasa kupitia ushirikiano na
Facebook hasa ukizingatia OLX ni moja ya huduma za bure ndani ya huduma
za mtandaoni hivyo Watanzania watafanya biashara,” alisisitiza Platenga
Huduma ya Facebook inafanya
matumizi ya mtandao kuwa rahisi kupitia huduma za bure ambazo
zinawawezesha watu kuperuzi mambo mbalambali kwenye tovuti bila kulipia.
Wateja wa mtandao wa tigo nchini Tanzania wanaweza kupata huduma ya internet kupita Google Play kwa kutembelea tuvuti ya www.internet.org
kwa kutumia simu ya mkononi kupitia Opera Mini. Huduma hii inapatikana
kwa watumiaji wa smart phones na simu za kawaida zenye uwezo wa
internet.
Kampuni ya OLX ina wafanyakazi
600 kwenye ofisi zake zilizoko Buenos Aires, Cape Town, Delhi, Sao
Paulo, Rio de Janeiro, Lisbon, New York na Kenya.
No comments:
Post a Comment