Pichani (Katikati) ni Mwanaafa Mwinzagu ambae ni Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wafanyakazi na Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions ambao
ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya
kutangazwa mshindi wa Kitita cha Milioni 50 za Kitanzania katika fainali
ya shindano la TMT lililomalizika Mnamo tarehe 30 Aug 2014 katika
Ukumbi wa Mlimani City na Kumtangaza Mwanaafa Kuwa Mshindi kwa Mwaka
2014.
Mwanaafa Mwinzagu
ambae alishiriki Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) huku akiwa
ni Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Tandika iliyopo
Mjini Mtwara katika Manispaa ya Mtwara amefaulu mitihani yake ya
kumaliza elimu ya Msingi Kwa Kupata daraja C huku Masomo ya Hesabu na
Sayansi akiwa kafanya vizuri sana kwa Kupata Daraja B.
Wakati
Shindano la TMT lilipofika Mtwara kwaajili ya kusaka vipaji vya kuigiza
Ndipo Mwanaafa alipojiunga na Kuja kushiriki Katika SHindano hilo Kubwa
na lenye mvuto wa Pekee Afrika Mashariki na Kati. Wakati akihojiwa mara
baada ya Kutoka katika hatua ya Kwanza ya Shindano hilo lililofanyika
Mtwara na kuhojiwa Mwanaafa Mwinzago alisema “Hiki ni Kipaji kwahiyo
sina haja ya kuficha na pia naweza Kukosa kwenye Shule nikapata Kwenye
Kuigiza na ndio maana nimekuja Kushiriki” Vilevile alipoulizwa Je
Ikitokea Ukashinda itakuwaje Shule na Sanaa? Alijibu kuwa “Ikitokea
nikashinda katika ngazi ya Kanda ya Kusini Nitaenda Kambini Dar Es
Salaam na kuacha Shule kwanza, Maana Shule Ipo ila Shindano hili
linapita tu Kwahiyo Naweza kupata kwenye Sanaa na nikishinda basi
nitarudia Darasa”.
Mara
baada ya Kuibuka MShindi katika Kinyanganyiro Hiko Katika Ngazi ya
Kanda ya Kusini, Timu nzima ya TMT iliweza kumuhoji Mwalimu wake Mkuu
ambapo alisema yafuatayo “Huyu Ni mwanafunzi wa Darasa la Saba Kwa
Sahivi na Hiki pia ni kipaji lakini Sisi kama Wazazi hatuwezi kuzuia
Mtoto kuonyesha Kipaji chake yeye alichofanya alishiriki Mashindano na
ameshinda kwahiyo sisi kama walimu wake tutajadiliana jinsi ya kulitatua
hili kwa maana hatuwezi kujua labda mshindi wa Milioni 50 hatakuwa
yeye”
Mara
baada ya Shindano la TMT kumalizika tarehe 30 August 2014 wiki moja
baadae Mwanaafa aliweza Kurejea Mjini Mtwara kwaajili ya Kufanya
mitihani yake ya Kuhitimu Elimu ya Msingi na Hatimae mara baada ya
kuwasili nyumbani kwao Mwanaafa aliweza kwenda shule kwao kwaajili ya
kukamilisha taratibu za kufanya mtihani na kesho Mwanaafa akaweza
kufanya Mitihani yake vizuri kwa muda wa siku mbili na alipomaliza
Alirejea Jijini Dar Es Salaam ambapo Aliendelea na zoezi la Kurekodi
filamu ya Pamoja Ya Washindi wa TMT waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi
Bora huku yeye akiwa ni kinara katika filamu hiyo ambayo inatarajiwa
kuzinduliwa Mapema Mwezi wa Kumi na Mbili katika Mikoa yote ambayo TMT
ilipita kwaajili ya kusaka Vipaji.
Hapo
Majuzi kupitia Vyombo mbalimbali vya habari kupitia Baraza la Mitihani
la Taifa (NECTA) lilitangaza matokeo ya Mitihani ya Elimu ya Msingi na
Ndipo tulipofahamu kuwa Mwanaafa ameweza kujitahidi sana katika Mitihani
huku akiwa kafanya Vizuri sana katika Masomo ya Hesabu na Sayansi
ambapo amepata daraja B huku masomo mengine akiwa amepata daraja C na
Kupelekea kupata wastani wa daraja C.
Kwa
Matokeo hayo tunapenda kumpongeza Mwanaafa kwa kuonyesha uwezo wake
katika Masomo na hatimaye kufanya vizuri katika Mitihani yake ya Mwisho
ya Kumaliza Elimu ya Msingi
Ikumbukwe
kuwa hapo awali Mwanaafa alisema kuwa endapo atashinda Milioni 50
katika fainali ya Shindano la TMT lililomalizika tarehe 30 August 2014
basi atatumia Kiasi hiko cha pesa kwaajili ya kujiendelea kielimu lakini
Wakati wa Fainali hiyo Kampuni ya Proin Promotions Ltd iliahidi
kumsomesha Mwanaafa hata Kama asingeshinda katika Shindano hilo.
Kwasasa
Mwanaafa yupo chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions ambapo
kampuni hiyo itamsomesha Kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Cha Nne.
Kampuni
ya Proin Promotions Ltd inapenda kumpongeza Mwanaafa kwa kufanya Vizuri
katika Mitihani yake ya Kumaliza Elimu ya Msingi na kuonyesha Kuwa
Kumbe Bado ni Mshindi hadi Darasani.
No comments:
Post a Comment