Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii ambapo tiketi za
elektroniki hazitauzwa tena kwenye magari, hivyo washabiki wanunue
tiketi hizo kwenye mtandao aukwenye maduka ya CRDB Fahari Huduma.
Kesho (Novemba
8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutakuwa na mechi
kati ya Yanga na Mgambo Shooting wakati Uwanja wa Chamazi kutakuwa na
mechi kati ya Azam na Coastal Union. Jumapili ni mechi kati ya Simba na
Ruvu Shooting.
Viingilio kwenye mechi za Uwanja
wa Taifa ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000
(viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 (VIP B na C) wakati VIP A
itakuwa sh. 20,000. Mechi za Uwanja wa Chamazi kiingilio ni sh. 3,000
kwa sh. 10,000.
Mechi nyingine za VPL kesho ni
kati ya Stand United na Mbeya City (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga),
Mtibwa Sugar na Kagera Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo ya saba itakamilika Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Ndanda kutoka Mtwara.
Wakati huo huo, mchezaji bora wa
VPL kwa mwezi Oktoba, Salum Abubakar wa Azam atakabidhiwa zawadi yake
kesho (Novemba 8 mwaka huu) kabla ya mechi kati ya Azam na Coastal
Union.
No comments:
Post a Comment