Kushoto ni Dkt. Frank Forka ambaye ni
mkurugenzi PGCEDC Africa Trade Office akielezea njia za kufuata kwa
mwekezaji kutoka Tanzania anapokuja kutafuta au kufanya mazungumuzo na
wawekezaji wa Kimarekani kwa ajili ya kuingia nao ubia kwa ajili ya
kuwekeza Tanzania. Dkt. Frank Furka alisema jambo la kwanza muhimu ni
kujifunza utamaduni wa wafanyabishara wa Kimarekani hasa inapokuja
kwenye swala la muda, Mambo mengine ya kuzingatia ni ufafanuzi wa kina
na uwazi wa fulsa unayoitafutia mwekezaji na itakapokuja swali uwe na
uwezo wa kulijibu kwa ufasaha.
Caroline Chang kutoka Maryland Center
For Foreign Investment akielezea sheria ya EB-5 Invester’s Program
inavyoweza kumnufaisha mwekezaji kutoka Tanzania anayewekeza nchini
Marekani.
Jessca Mushala Mkurugenzi wa SHINA
akielezea wawekezaji kutoka Tanzania wanahitaji mafunzo kwanza jinsi ya
kujieleza, kuandika poropozo na kujifunza utamaduni wa wafanyabishara wa
Kimarekani kabla hajakuja nchini Marekani. Jessca Mushala aliongezea
kwamba anampango wa kumtuma mmoja ya mwakilishi wa SHINA kwenda Tanzania
kufanya semina na wawekezaji wa Tanzania na kuwapa mafunzo ya nini cha
kufanya wanapokuja Marekani kutafuta wawekezaji wanaotaka kuingia nao
ubia.
Kutoka kushoto ni Mzee Zuberi,
Stanslaus Munyaraga Malima na Awadhi Zuberi Athman wa kampuni ya Urban
and Rural Engineering Services Ltd. Awadhi na Malima wapo nchini
Marekani wakijaribu kujinadi kwa wawekezaji wa Kimarekani watakaoingia
nao ubia kwenye fulsa ya uwekezaji ya umeme wa jua ikiwemo vifaa vya
ujenzi.
Kulia kwa Jessca Mushala ni Mujuni
Joseph Kataraia akielezea kampuni ya Urban and Rural Engineering
Services Ltd na aina gani ya mwekezaji wanaemtafuta kuingia nae ubia wa
uwekezaji wa umeme wa jua na vifaa vya ujenzi.
Dr..Loleta Robinson anayejihusiha na bishara ya vifaa vya
hospitali na maabara akielezea uzowefu wake na Tanzania na kuchangia
utamaduni wa swala la muda akijitolea mfano yeye mwenyewe alipokua
Tanzania iibidi ajifunze utamaduni wao muda. Tanzania ukitaka kufanikiwa
kilichokupeleka inakubidi uvumilie swala la muda kwani kuchelewa kwenye
vikao ni jambo la kawaida. Dr. Loleta aliongezea alisema baada ya
kufahamu hilo alichokua akifanya ni kuwahi huku akiwa na kitabu chake
alichokua akikisoma huku akiendelea kuwasubili wahusika. Kulia ni Shaban
Mseba aliyekuja kwenye semina hiyo kutoka New York.
wawakilishi kutoka SHINA wakifuatilia semina
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment