Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil akitoa
hotuba ya Ufungaji wa Mkutano wa Wadau uliohusu upokeaji wa maoni ya
Sera ya Taifa ya Magereza. Mkutano huo wa siku mbili umefanyikia katika
Hoteli ya Livingstone Bagamoyo ambapo wadau wamepitia rasimu hiyo na
kutoa maoni kikamilifu Novemba 05, 2014.
Wadau
wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji wa Mkutano wa Wadau uliohusu
upokeaji wa maoni ya Sera ya Taifa ya Magereza Novemba 05, 2014 katika
Hoteli ya Livingstone Bagamoyo .
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi
kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw.
Mbarak Abdulawakil kutoa hotuba ya Ufungaji wa Mkutano wa Wadau
uliohusu upokeaji wa maoni ya Sera ya Taifa ya Magereza.
Mchumi
kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Deonesia Mjema akichangia maoni katika
rasimu ya Sera ya Taifa ya Magereza kabla ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil kutoa hotuba ya Ufungaji wa
Mkutano wa Wadau uliohusu upokeaji wa maoni ya Sera ya Taifa ya
Magereza.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) akipitia
makabrasha wakati wa majadiliano ya rasimu ya Sera ya Taifa ya
Magereza(kulia) ni Mkurugenzi Idara ya Malalamiko Wizara ya Mambo ya
Ndani, Bw. A. Shio(kushoto) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Bw. Mbarak Abdulawaki.
Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma malewa akitolea
ufafanuzi wa Haki za Wafungwa wanazostahili kupatiwa wawapo Magerezani
wakati wa majadiliano Sera ya Taifa ya Magereza Novemba 05, 2014 katika Hoteli ya Livingstone Bagamoyo(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
…………………………………………………………………………
Na Lucas Mboje; Bagamoyo
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja
amepongezwa na Wadau mbalimbali nchini kwa kufanikisha kuandaa na
kukamilisha rasimu ya Sera ya Taifa ya Magereza ambapo Wadau kutoka nje
ya Jeshi la Magereza wamepata fursa ya kujadili kwa siku mbili Wilayani
Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Pongezi hizo wamezitoa kwa nyakati tofauti mjini Bagamoyo
katika Mkutano wa siku mbili wa Wadau wa kupokea maoni juu ya rasimu ya
Sera ya Taifa ya Magereza uliofunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil Novemba 04, 2014 katika
Hoteli ya Livingstone – Bagamoyo.
“Tunampongeza sana Kamishna Jenerali Minja hususani kwa
kufanikisha rasimu hiyo na tunaamini kutokana na kasi yake ya Utendaji
wa kazi rasimu hiyo itawasilishwa mapema Serikali kwa hatua za mwisho,”
Walisikika wakisema.
Aidha, wameongeza kuwa kukamilika kwa Sera ya Taifa ya
Magereza kutaleta ufanisi katika utendaji na uboreshaji huduma
mbalimbali zitolewazo ndani ya Jeshi la hilo.
Awali akitoa maelezo mafupi katika ufunguzi wa Mkutano huo
wa Wadau wa kupokea maoni ya Sera ya Taifa ya Magereza, Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja alisema kuwa
chimbuko la kuwa na Sera hiyo ni kubadili utaratibu wa kuwafunga
wahalifu magerezani ambao ulianza wakati wa Ukoloni na ulilenga zaidi
kuwakomoa na kuwaadabisha.
Jenerali Minja aliongeza kuwa utaratibu huo ulilenga kuwaweka
wahalifu kwenye Ulinzi mkali na kuwafanyisha kazi ngumu zisizo na tija
nazisizozingatia haki za Binadamu.
Alisema kuwa baada ya Uhuru mwaka 1961, Falsafa ya Magereza
ilibadilika kutoka ile ya kukomoa na kuwaadabisha wahalifu na kuwa
Urekebishaji na kuzingatia haki za Binadamu.
“Mabadiliko ya kifalsafa pamoja na kuridhiwa kwa Mikataba
mbalimbali ya Kimataifa yanatulazimu kuwa na Sera ambayo ndiyo itakuwa
dira ya Utekelezaji wa shughuli za kila siku za Jeshi la Magereza,”
alisema Jenerali Minja.
Aidha Jenerali Minja, aliongeza kuwa sera hiyo inalenga pia kubadili mitizamo ya jamii
kuwa magereza ni mahali pa mateso. “Tunataka Magereza ya sasa ionekane
ni chuo cha kubadili tabia za wafungwa ili wamalizapo vifungo vyao wawe
ni raia wema katika jamii.”
Jeshi la Magereza kupitia Wataalam
wake limeandaa Rasimu ya Sera ya Taifa ya Magereza kwa kushirikiana na
Mshauri Mwelekezi toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Dkt. Haji Semboja ambapo tayari wadau wote wa ndani na nje ya Jeshi la
Magereza wamepata fursa ya kuchangia maoni yao kikamilifu tayari
kuwasilishwa rasmi Serikalini kwa hatua za mwisho,
No comments:
Post a Comment