Mkurugenzi
wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru, (katikati),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya B Pesa
Novemba 5, 2014 jijini Dar es Salaam wakati akizindua shindano
lijulikanalo Chini ya kizibo ( Tutoke na Serengeti), ikishirikiana na B
Pesa, ambampo washindi watapelekwa Mbuga za wanyama (wakwanza kulia),
Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Allan Chonjo (wapili
kushoto), ni Mkurungezi mkuu wa B. Pesa, Robert Boniface, (wakwanza
kushoto), Meneja wa Mendeleo ya Biashara, Salil Abbas. Meneja
masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Allan Chonjo (kushoto)
akionyesha moja ya zawadi kwa waandishi wa habari zitakazo shindaniwa. Meneja wa Mendeleo ya Biashara,
Salil Abbas, akielezea huduma mpya ya kutuma fedha ambayo inashirikiana
na benki mbalimbali nchini ikiratibiwa na Benki Kuu (BOT) lengo likiwa
ni kurahisisha utoaji na utumaji wa fedha katika maeneo mbalimbali.
………………………………………………………………
KAMPUNI ya bia ya Serengeti
kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager imezundua mpango kabambe
unaoitwa Tutoke na Serengeti na kuwazawadia wateja wake kwakuwapa fursa
ya kufaidi utalii wandani kwakuwapeleka kwenye mbuga za wanyama
.Promosheni hiyo inalenga kuwafikia wateja wapatao milioni 20 ambao
watapata fursa ya kujishindia fedha taslimu na zawadinyingine nyingi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
Novemba 5,2014 wakati akizindua shindano la kuwazawadia watanzania kwa
kuwapa fursa mbalimbali pamoja na zawadi ambazo kwa ujumla zinagharimu
Sh bilioni 1.2. Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,
Ephraim Mafuru. Alisema.
Katika kuendesha shindano hilo,
kampuni hiyo imeshirikiana na wataalam wa teknolojia B-pesa ambapo
washindi watapata fursa ya kulipwa fedha zao kupitia mfumo huo.
Kuhusu hifadhi za taifa, alisema
kupitia shindano hilo watanzania takriban milioni 20, watapata fursa
ya kufaidi utalii wa ndani kwa kupelekwa katika mbuga za wanyama na
kuweza kuitangaza Tanzania na vivutio vilivyomo popote watakapokuwa.
Alisema Tanzania ina maliasili
nyingi ambazo kwa hakika wapo watanzania wasiokuwa na uzalendo wa
kuzitembelea na kujionea fahari ya nchi yao jambo ambalo hubaki
huwafanya wengine kuona kama wanaotakiwa kufanya hivyo ni watalii wan je
ya nchi peke yake.
Kuhusu shindano hilo alisema
linalojulikana kama “tutoke na Serengeti” na washindi watajishindia
zawadi fedha taslimu zenye thamani y ash milioni 100 ambazo zimegawaywa
katika mafungu y ash 5000 na kwa mshindi atakaetembelea mbuga za wanyama
atapata fursa ya kwenda na marafiki watano wakigharamiwa kila kitu.
“Kwa kupitia kinywaji cha
Serengeti washindi watapata babj sita aina ya limo zenye uwezo wa kubeba
abiria saba zikiwa na vifaa vya B-pesa kwa ajili ya kufanya shughuli
mbalimbali,” alisema na kuongeza kuwa kila wiki mshindi atatangazwa
katiak shindano hilo litakalodumu kwa miezi mitatu.
Kuhusu B-Pesa, Meneja wa Mendeleo
ya Biashara, Salil Abbas alisema ni huduma mpya ya kutuma fedha ambayo
inashirikiana na benki mbalimbali nchini ikiratibiwa na Benki Kuu (BOT)
lengo likiwa ni kurahisisha utoaji na utumaji wa fedha katika maeneo
mbalimbali.
Alisema kutokana na kukua kwa
uchumi nchini kunasababisha kukosekana kwa usalama wa fedha hivyo kwa
kutumia huduma hizo kutawezesha kila mwananchi kuwa huru popote awapo
kutumia fedha yake kwa njia iliyo salama kwake.
No comments:
Post a Comment