Pichani
mtuhumiwa Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa aliyekamatwa eneo la
Mianzini jijini Arusha akiwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi
iliyokuwa inasafirishwa toka nchi jirani ya Kenya kuelekea Kondoa mkoani
Dodoma (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
…………………………………………………………………………………………
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Mtu mmoja aitwaye Hamis Mohamed
(47) Mkazi wa Kondoa mkoa wa Dodoma, amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa
wa Arusha baada ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi
aliyekuwa anaisafirisha kwa mtindo wa aina yake.
Akiongea na waandishi wa habari
ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba tukio hilo
lilitokea tarehe 05.11.2014 muda wa saa 11:00 jioni eneo la Mianzini
ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa anasafirisha madawa hayo kwenye gari aina
ya Fusso basi lenye namba za usajili T. 577 BFM ambapo aliihifadhi
kwenye magunia mawili huku juu na pembeni ya magunia hayo akiweka viatu.
‘’Katika magunia yale alikuwa
ameweka viatu na katikati aliweka viroba 36 vya madawa hayo aina ya
mirungi ambayo alikuwa anasafirisha toka nchini Kenya kupeleka Kondoa
mkoani Dodoma hivyo ukiangalia unaweza kusema ni viatu pekee’’.
Alifafanua Kamanda Sabas.
Alisema tukio hilo lilifanikiwa
kutokana na mahusiano mema yaliyopo kati ya Jeshi hilo na raia wema
ambao walitoa taarifa iliyofanyiwa kazi haraka na asakari wa Jeshi hilo.
Baada ya askari hao kupata
taarifa hiyo walianza kulifuatilia gari hilo na lilipofika maeneo ya
Mianzini jijini hapa kwenye maegesho ya basi hilo ndipo walipoanza
kufanya upekuzi na kufanikiwa kukamata magunia hayo yaliyokuwa na viatu
vilivyochanganywa na madawa hayo.
Kamanda Sabas alisema kwamba
mtuhumiwa huyo bado anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani mara
baada ya upelelezi kukamilika.
No comments:
Post a Comment