MWAKIBINGA AONDOKA BODI YA LIGI
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga amemaliza mkataba wake tangu Oktoba 31 mwaka huu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga amemaliza mkataba wake tangu Oktoba 31 mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na TPLB wanamshukuru Mwakibinga kwa mchango wake kwa
kipindi ambacho ameitumikia Bodi, na kumtakia kila la kheri katika
majukumu yake mapya huko aendako.
TPLB hivi sasa iko katika
mchakato wa kupata Ofisa Mtendaji Mkuu mpya kwa ajili ya kuziba nafasi
hiyo iliyoachwa wazi na Mwakibinga baada ya muda wa mkataba wake
kumalizika.
KOCHA NOOIJ KUTAJA KIKOSI STARS
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart
Nooij keshokutwa (Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo
kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba 16 mwaka huu.
Nooij atatangaza kikosi hicho
mbele ya waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30
asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower
jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.
No comments:
Post a Comment