Mbio za 13 za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika Moshi tarehe 1 Machi, 2015 zimezinduliwa leo jijini Dar es salaam.
George Kavishe, Meneja wa bia ya
Kilimanjaro Premium Lager alisema “Sasa tumeingia mwaka wa 13 wa
udhamini wa Kilimanjaro Marathon. Tunafurahi kuona Kilimanjaro Marathon
kwa mara nyingine tena ikiwa kivutio kwa makampuni mbalimbali, hii ni
uthibitisho wa jinsi mbio hizi zilivyoendelea kuwa kubwa na kivutio
chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager tangu zilipoanzishwa.”
“Kilimanjaro Premium Lager ina
furaha kuona jinsi ambavyo Kilimanjaro Marathon imepata mvuto na kuleta
shauku kubwa kwa washiriki wa hapa nchini na wa kimataifa kwa mara
nyingine tena mwaka huu. Udhamini wetu kwa Kilimanjaro Marathon umelenga
kuwapa nguvu wanariadha wetu na kuendeleza ari ya ushindi ili kuipeleka
riadha ya Tanzania juu zaidi.”Tangu udhamini wetu wa kwanza kwa
Kilimanjaro Marathon mwaka 2003, tumeshuhudia ukuaji wa mbio hizi na
tuna furaha kubwa kwa fursa ya kuendelea kuwa sehemu ya mbio hizi na
kuweza kuwaletea wanariadha wetu tukio kubwa la kimataifa hapa nyumbani.
Tunatarajia kuwa na tukio la kusisimua na tunayofuraha kutangaza kwamba
Kilimanjaro Marathon 2015 itakuwa ya kuvutia na yenye msisimko zaidi na
tunakaribisha watu wote wajitokeze kushiriki mbio hizi za aina yake
tarehe 1 Machi 2015.
Akitangaza udhamini wa Tigo kwa
mbio hizo, Meneja Chapa waTigo, William Mpinga alisema udhamini huo ni
sehemu ya wajibu wa kampuni hiyo katika maendeleo ya michezo nchini na
pia katika kusaidia jitihada za uhifadhi wa Mlima Kilimanjaro, kivutio
kikubwa cha utalii Tanzania”
“Tuna furaha sana kuwa sehemu ya
mbio hizi za aina yake ambazo zimepata mafanikio makubwa sana katika
kuutangaza Mlima Kilimanjaro kama kivutio cha kipekee cha utalii hapa
nchini na nje. Kama kampuni ya Kitanzania, tunajivunia mbio hizi kwa
kuleta fursa ambayo sio tu uwavutia wanariadha wa kimataifa, lakini pia
ni jukwaa muhimu la kuionyesha dunia vipaji vyetu katika riadha,”
alisemaMpinga.
Meneja Chapa huyo alisema kwamba
mbali na kufurahia mbio za nusu marathon zitakazojulikana kama “Tigo
Kili Half Marathon” zinazodhaminiwa naTigo mashabiki na wakazi wa Moshi
watapewa fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali za dijitali kutoka Tigo na
huduma zitakazoonyeshwa kwenye mbio hizo.
Meneja Utawala wa GAPCO, Jumbe
Onjero alisema: “GAPCO, wadhamini wa mbio za Marathon za Walemavu kwa
kushirikiana na waandaaji Wild Frontiers, Deep Blue Media na Executive
Solutions tutatoa msaada wa viti vya magurudumu 50 kwa wahitaji mkoani
Kilimanjaro ikiwa ni kuonyesha wajibu wetu kwa jamii.”
Kilimanjaro Marathon ilifanyika
kwa mara ya kwanza mwaka 2003 na imekua na kuwa moja kati ya mbio kubwa
zaidi barani Afrika ikiwa na washiriki zaidi ya 6,000 kutoka nchi zaidi
ya 40. “Kilimanjaro Marathon imeendelea kuboreshwa kila mwaka, kwenye
mbio ya kwanza mwaka 2003 tulikuwa na washiriki 750 tu, lakini kwenye
mbio zilizopita tulikuwa na washiriki zaidi ya 6,000 na idadi hii
inatarajiwa kuongezeka ukizingatia hizi ndio mbio zenye mvuto zaidi kwa
watalii barani Afrika,” alisema John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild
Frontiers, waandaaji wa mbio hizo.
Mbio hizi zinadhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Tigo (Nusu Marathon), GAPCO
(Mbio yaWalemavu), pamoja na wadhamini wa vituo vya maji kwenye mbio
hizo ambao ni Kilimanjaro Water, FNB, CMC Automobiles, Simba Cement, TPC
Sugar, KK Security, Kibo Palace, Rwandair na UNFPA.
No comments:
Post a Comment