Shughuli
za kuaga mwili wa aliyekuwa golikipa na kapteni wa timu ya taifa ya
Afrika Kusini, Senzo Meyiwa zimefanyika mchana wa leo Novemba 1 Durban.
Mchezaji
huyo alifariki baada ya kupigwa risasi siku ya jumapili majira ya saa 2
usiku, Oktoba 26 akienda kumuokoa mpenzi wake aliyekuwa amevamiwa na
majambazi nyumbani kwake, tayari mtuhumiwa wa kwanza amepandishwa
kizimbani jana Oktoba 31.Maelfu
ya watu wamefurika uwanja wa Moses Mabhida, Durban mchana wa leo kwa
ajili ya kuaga mwili wa golikipa huyo wakiwa wamevalia t-shirt zenye
picha ya Meyiwa .
No comments:
Post a Comment