“Dovutwa amesema vyama hivyo vimeamua kushirikiana kwa sababu vipo
vyama vilivyounda kundi lisilokuwa la kisheria linaitwa Ukawa, lakini
hakuna sheria inayoturuhusu kuunganisha vyama ila tunaweza kushirikiana
tu ndiyo maana tunasema tumekubaliana kushirikiana”. vyama
vilivyokubaliana kushirikiana ni SAUT, DEMOKRASIA MAKINI, JAHAZI ASILIA,
UMD, UMD, UPDP NA AFP , Katika picha wanaofuatia ni Dominic Lyamchai
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini, Rashid Lai Katibu Mkuu AFP na
baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Chama cha SAUT Yusuf Manyanga akifungua mkutano huo kabla ya Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa kutoa tamko.
Rashid Lai Katibu Mkuu AFP akifafanua
jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Sinza jijini Dar es salaam
kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha SAUT Yusuf Manyanga ,
Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa na Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini
No comments:
Post a Comment