Na Mwandishi Wetu
MWANAMICHEZO maarufu nchini, Azim Dewji amewataka wanachama na wapenzi wa timu ya soka ya Simba kuamini timu yao bado ni bora, isipokuwa ipo katika kipindi cha mpito kuelekea katika mafanikio yatakayowashangaza wengi.
MWANAMICHEZO maarufu nchini, Azim Dewji amewataka wanachama na wapenzi wa timu ya soka ya Simba kuamini timu yao bado ni bora, isipokuwa ipo katika kipindi cha mpito kuelekea katika mafanikio yatakayowashangaza wengi.
Kutokana na imani yake hiyo, ameshauri ni vyema wakatoa ushirikiano wa kila aina kwa viongozi, wachezaji na benchi lote la ufundi, vivyo hivyo akiwataka viongozi kushikamana na wachezaji na benchi la ufundi,badala ya kuanza kunyoosheana vidole.
Aliyasema hayo jana alipokuwa anazungumzia mwenendo wa klabu hiyo
aliyowahi kuifadhili na kuipa mafanikio makubwa katika miaka ya 1990,lakini msimu huu ukionekana kuyumba, kwani tangu kuanza kwa ligi,imetoka sare katika mecho zake zote sita, hali inayowasonesha `wanazi’ wa klabu hiyo.
Alisema Simba inapitia mapito kama ya Manchester United ya England
ambayo tangu kuondoka kwa kocha wake wa zaidi ya robo karne, Sir Alex Ferguson iliyumba na hata kutemeshwa ubingwa kwa aibu, lakini sasa imeanza kurejesha makali.
“Sasa ukiangalia hata Simba si timu mbaya ndiyo maana ingawa
haijashinda, haijapoteza mchezo pia. Haya yanatokana na mabadiliko
mengi kwa wakati mmoja, kuanzia safu ya uongozi, benchi la ufundi na
hata wachezaji…hawa watu wanahitaji kupewa muda. Nakuhakikishia Simba hii itakuwa tishio.
“Lakini wakati nikiwasihi wanachama na wapenzi kuwaunga mkono
viongozi, wachezaji na kocha, naamini viongozi nao watumie busara ya
kufanya kila linalowezekana kuwafanya wachezaji na makocha kujiamini
na kujiona wana deni, lakini si kutishiana kila kukicha.
“Hii si sahihi na kwa mazingira ya vitisho, siku zote watabaki kuwa
watu wa wasiwasi na kushindwa kuisaidia timu…tuwape nafasi, hakika
mapinduzi ya kisoka yataonekana kwa sababu nimeona timu ina wachezaji wengi wenye vipaji,” alisisitiza Dewji.
Katika msimu huu wa ligi, Simba ilianza ligi kwa kutoka sare ya 2-2 na Coastal Union ya Tanga kabla ya kupata sare mbili za matokeo ya 1-1 mbele ya Polisi Moro na Wakuja katika ligi hiyo, Stand United ya
Shinyanga. Haikufungana na Yanga iliyokuwa inaaminika ni mara zaidi
tangu ilipomnasa kocha Mbrazil Marcio Maximo katikati ya mwaka huu,
ikatoka pia sare ya 1-1 na Prisons ya Mbeya na pia na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
No comments:
Post a Comment