Mkurugenzi wa Kampuni inayojishughulisha na uboreshaji wa kuku Zanzibar(Zanchick) Bw.Issa Khasim Issa akikabidhi chanjo 600,000 zenye thamani ya Tshs 9,000,000 kwa Naibu katibu katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Omar Ali Amir kwa ajili ya kuwalinda kuku na ugonjwa wa Mdondo, anayeshuhudia kulia Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis
………………………………………………………………………………….
Kampuni inayojishughulisha na
uboreshaji wa kuku Zanzibar, Zanchick, leo imetoa chanjo 600,000 zilizo
na thamani ya Tshs 9,000,000 kwa wafugaji kuku kwa ajili ya kuwalinda
kuku wao na ugonjwa wa Mdondo.
Utoaji wa chanjo hizo ulifanyika kwa msaada wa wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar ambao wata ratibu na kusimamia zoezi zima.
Meneja wa Uendeshaji, kutoka Zanchick, Bwana Christopher
Kontonasios alisema: “Tunashukuru Wizara ya Ufugaji na Uvuvi kwa kuwa
washiriki wakubwa katika kuratibu zoezi hili na tunataraji serikali
itazidi kuwasaidia wazalishaji kuku wa kawaida, kwa kuondoa kodi ya
kuagiza chakula cha kuku, jambo
ambalo litawaruhusu wazalishaji wa kawaida kupata chakula bora cha kuku
chenye bei nafuu. Hii ndio njia pekee ya kuwawezesha wakulima wa
kawaida kuendeleza ufugaji wa kuku, kwa kiwango cha hali ya juu, na pia
kuwaruhusu kukidhi biashara zenye faida.
Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka
Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis alisema,
“Tunafarijika na juhudi za Zanchick katika kuboresha uzalishaji wa kuku
Zanzibar, hii ni hatua kubwa kwa wafugaji wa kawaida. Tunatarajia
kuongeza juhudi katika kushirikiana kukuza viwango na jitihada za
ufugaji kuku kisiwani hapa.”
Kirusi cha ugonjwa wa Mdondo kwa
ujumla hakisababishi madhara yoyote kwa afya ya binadamu, lakini kina
uwezo wa kuleta maafa makubwa kwa wafugaji wa kawaida, kwa kumaliza
kiasi kikubwa cha kuku na hatimaye kuangamiza biashara yao.
Msaada huu mkubwa na muhimu ni katika juhudi za Zanchick
kufanya kazi na wafugaji wa kawaida ili kuongeza, kuboresha na kunadi
uzalishaji wa kuku Zanzibar.
No comments:
Post a Comment