Na mwandishi wetu, Zanzibar
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amepongeza
juhudi zinazofanywa na Serikali ya Zanzibar katika kuangalia masuala
muhimu yanayohusu muktadha ujao wa kufanikisha uondoaji wa umaskini
uliotopea (SDGs) baada ya kukamilika kwa programu ya maendeleo ya
milenia (MDGS).
Alisema
kitendo cha serikali kuandaa warsha ya kupashana kuhusu programu hiyo
mpya kabla ya mazungumzo na mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo ni
washirika wa maendeleo kuhusu SDGs kunaonesha dhamira ya dhati kwa
serikali kuendelea kusukuma mbele maendeleo yenye lengo la kunemeesha
wananchi.
Mratibu
huyo alisema hayo hivi karibuni katika warsha iliyofungulia na Katibu
Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee iliyokusanya
wadau mbalimbali wa maendeleo kuangalia malengo ya programu ya maendeleo
endelevu (SDGs),iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii
(ESRF).
Warsha
hiyo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Programu wa ESRF Dk. Tausi Kida warsha
hiyo ni sehemu ya kuelezana kuhusu mkakati huo mpya wa Umoja wa Mataifa
unachukua nafasi ya MDGs na nafasi ya Tanzania katika kutekeleza
malengo hayo ya kimataifa.
Warsha hiyo imefadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNDP, UNAIDS na UNWOMEN.
Mratibu
huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa amesema kwamba agenda
zilizopangwa kujadiliwa zinaonesha ujasiri wa Tanzania katika
kuhakikisha inashiriki kwenye ajenda za dunia kwa kutekeleza nafasi yake
katika mipango ya maendeleo na ustawi wa jamii kwa kuzingatia usawa wa
jinsia.
Alisema
shughuli inayofanywa sasa ya kuwasilisha malengo hayo kwa majadiliano
miongoni mwa wadau mbalimbali kabla ya majadiliano rasmi kati ya
mashirika ya Umoja wa mataifa na serikali ni ya maana katika kuongeza
uelewa na kuimarishwa kwa mawazo muhimu.
Warsha
ya kwanza ya aina hiyo ilifanyika Oktoba 27 jijini Dar es Salaam ambapo
wadau mbalimbali wakiwemo wanazuoni, wawakilishi wa serikali, taasisi
zisizo za kiserikali na wengineo walijadiliana kuhusu SDGs na kama
malengo yake yanawezwa kutekelezwa.
Aidha
warsha hiyo ilijadili kama malengo hayo yanawezwa kutumiwa na watunga
sera na kuleta tofauti inayotakiwa na kama malengo hayo yanahitaji
kuboreshwa zaidi ili kujua kitu cha kufanya na kama umma unaweza
kujipanga kutekeleza malengo hayo.
Alvaro
alisema agenda hizo zinakwenda vyema na mpango wa Msaada wa Maendeleo
wa Umoja wa Mataifa kwa Tanzania (UNDAP) kwa kuwa imejikita katika
maeneo muhimu yanayopambana na kutokomeza umaskini na kuwa na maendeleo
endelevu.
Maeneo
hayo ni pamoja na malengo ya milenia ambayo hayajatekelezwa kwa
ukamilifu, nishati, mabadiliko ya tabia nchi,mazingira na kujenga jamii
yenye amani na kujali maendeleo.
Akizungumza
katika mkutano huo uliofanyika Zanzibar Beach resort, Katibu Mkuu
alisema ni vyema wazanzibari wakatumia nafasi hiyo kutengeneza mkakati
wa Zanzibar wanayoitaka, Zanzibar yenye maendeleo inayojali haki na
yenye amani.
Aliwataka
wana warsha kutumia nafasi hiyo kujipanga vilivyo katika kuhakikisha
wanajua kinachotokea duniani katika sekta ya maendeleo na kutumia nafasi
hiyo kutengeneza muskabali wa wazanzibari unaoendana na malengo ya
dunia ya kutokomeza umaskini na kujenga nchi yenye kujali maslahi ya
jamii yenye maendeleo endelevu na amani.
Alisema
mafanikio ya malengo ya milenia yaliyojikita katika kutokomeza umaskini
na njaa, kufanikisha elimu ya msingi kuyaleta usawa wa kijinsia na
kuwawezesha wanawake na kupunguza vifo vya watoto na wanawake
wajawazito, kukabiliana na Ukimwi, kuhakikisha mazingira endelevu na
kuleta mshikamano wa kimataifa katika maendeleo yanatakiw akuendelezwa.
Alisema
kwa miaka 15 zanzibar imefanya vyema katika programu hizo na kutaka
wadau kufikiria kuimarisha na kuangalia kwenye udhaifu ili kuyakamilisha
kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
No comments:
Post a Comment