……………………………………………………………..
Wanasiasa wameaswa kudumisha amani, upendo na mshikamano wa Tanzania,
ili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza ambazo kwa kiasi kikubwa
zimekuwa zikisababishwa na makundi ya wanasiasa, kwa kutoa ujumbe kwa
wananchi unao chochea kuvurugukika kwa amani ya Tanzania.
Akizungumza na wanamichezo wa vilabu mbalimbali vya kukimbia (Jogging) kutoka Tanzania bara na Zanzibar,
katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, mbunge wa jimbo
la Nzega, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Tawala za mikoa
na seikali za mitaa, Dk. Hamis Kigwangala, amesema wakati bunge maalum
la Katiba lilipokuwa likitunga katiba inayopendekezwa, kuliibuka baadhi
ya wanasiasa, waliokana kushiriki katika bunge hilo na kutofautiana
katika baadhi ya mambo kuingizwa katika katiba hiyo, huku wale waliobaki
ndani ya bunge maalumu la katiba kwa asilimia takriban 85 wakiheshimu
maamuzi ya watanzania na kuhakikisha katiba mpya inapatikana.
Hivyo amewataka
wanasiasa pamoja na kuwa mapendekezo yao hayakuingia ndani ya katiba
wasiwe chanzo cha kutokuridhika kwao kulazimisha na watanzania wengine
wasiridhike na kwamba watanzania waachwe siku ya kuipigia kura katiba
inayopendezwa itakapo tangazwa, watanzania waipigie kura ya ndio au
hapana na kwamba waamue kwa utashi wao bila uchochezi wa wanasiasa.
Katika Tamasha hilo lililopewa jina la Mbio za amani 2014, Dk, Kigwangala pia amehimiza umuhimu wa kufanya michezo
kila wakati, kwani michezo ni Afya, Furaha, Amani, Upendo na Ajira,
huku akivitunuku vyeti baadhi ya vilabu vya Jogging kwa kushiriki katika
tamasha hilo.
Tamasha hilo limeshirikisha wanamichezo wa vilabu vya Jogging kutoka Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam, ambapo limeandaliwa na Faita Jogging & Sports Club ya jijini Dar es Salaam, huu ukiwa ni mwaka wa tatu kuandaliwa.
No comments:
Post a Comment