Mratibu
wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu
inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha akitoa maelezo
kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(kulia) alipotembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la
UNDP wilayani Longido mkoani Arusha katika ziara yake ya siku mbili mara
baada ya kuwasili wilayani humo. Katikati ni Mtaalam wa Mahusiano na
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu aliyeambatana
na Mwakilishi huyo.
Na Mwandishi wetu,
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amewataka
wadau wa mazingira nchini kuwasaidia wananchi wa vijijini hasa wafugaji
kutumia nguvu na rasilimali walizonazo kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuendelea kuhifadhi mazingira na viumbe
vilivyopo wakiwemo wanyamapori
Bw,
Rodriguez aliyasema hayo wilayani Longido mkoani Arusha katika ziara
yake ya siku mbili ya kutembelea baadhi ya miradi inayofadhiliwa na
shirika hilo .
Akizungumza
baada ya kutembelea na kuzindua mradi wa kuwawezesha wafugaji wa wilaya
ya Longido kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kujenga uzio wa
kulinda mifugo yao na wanyama wakali Bw, Rodriguez, amesema kutokana na
uelewa mdogo wa mabadiliko yanayoendelea kutokea wananchi wengi wa
vijijini wanahitaji msaada wa namna ya kuyadhibiti.
Mratibu
wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu
inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha akiendelea
kutoa maelezo kwa Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez (katikati), wa
pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya.
Aidha
alisema kwa sasa wananchi wengi wanatumia muda na nguvu nyingi
kushughulikia matokeo ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na maeneo
mengi wamekuwa wakijikuta wanagombana wenyewe kwa wenyewe badala ya
kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya msingi.
“mara
nyingi wananchi wa vijijini kama hawa wafugaji mmekuwa wamekuwa
wakilaumiwa kwa matokeo ya yale wanayoyafanya kwa kusukumwa na
mabadiliko haya na mengine wangeweza kuyajua wala wasingeyafanya
“alisema Rodriguez.
Aidha
Bw. Rodriguez ambaye pia ni Mkuu wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa
na shirika hilo hapa nchini amewataka viongozi na watendaji wakiwemo
watalaam kutumia muda na uwezo wao kuwasaidia wananchi wa vijijini hasa
wafugaji na kwamba UNDP itaongeza nguvu kusaidia makundi hayo.
Mratibu
wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu
inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha akimwoonyesha
eneo maalum lililowekwa uzio kwa ajili ya kulinda mifugo na wanyama wa
kali Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez aliyefika wilani hapo kukagua
miradi hiyo.
Mratibu
wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu
inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha ambaye pia ni
mtafiti mkuu wa wanyama katika taasisi ya utafiti wa wanyamapori TAWIRI
amesema mradi huo umeonyesha mafanikio makubwa kwa kuanza kupunguza
uhasama kati ya wafugaji na wanyama pori wanaokula mifugo yao wakiwemo
Simba na Fisi.
Kwa
upande wao viongozi na wananchi akiwemo Mkuu wa wilaya ya Longido Bw
James Ole Milya wamesema pamoja na changamoto zinazowakabili wanaendelea
kutilia mkazo suala la utunzaji wa mazingira na wanyamapori kwani licha
ya kuwa ni asili yao ndio msingi wa maisha yao.
Mkuu
wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya (kulia) akifafanua
jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez (wa pili kushoto) wakati alipotembelea wilaya hiyo kukagua
maendelo ya miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP. Kushoto ni
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez
akisalimiana na na wanawake wa kimasai mara baada ya kuwasili wilayani
Longido kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa
Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya kwa pamoja wakizundua
uzio wa kuhifadhia mifugo ya jamii ya wafugaji wilayani Longido wakati
alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika la
UNDP.
Muonekano wa uzio utakaotumika kuhifadhia wanyama wasidhurike na wanyama wakali mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akitoa
nasaha zake kwa jamii ya wafugaji wa wilaya ya Longido mkoani Arusha
alipofanya ziara ya siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika
la UNDP.
Baadhi
ya wakazi wa Longido ambao shughuli zao kubwa ni ufugaji wakimsikiliza
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo
pichani).
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akivishwa
zawadi ya shuka la kimasai na mmoja wa wafugaji wa wilaya hiyo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
akisikiliza maelezo ya zawadi za asali za Nyuki wadogo na wakubwa kutoka
kwa jamii za wafugaji wanaofadhiliwa na shirika la UNDP wakati
alipofanya ziara ya kukagua miradi hiyo wilayani humo.
No comments:
Post a Comment