Mkutano ulifanyika kuanzia saa
1520hrs ukiwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu mh. Joseph Sinde
Warioba. Mkutano ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na
itikadi tofauti za kisiasa. Mkutano ulirushwa moja kwa moja na ITV na
maudhui yake kimtazamo ulilenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya
Katiba ya tume ya Warioba na ile ya Mh. Sitta na tume yake. Baada ya Mh.
Warioba kuelezea kwamba Muungano sio tunu ila ni urithi ndipo
wakereketwa wa upande wa Mh. Sitta walipoinua mabango yasemayo pamoja na
mambo mengine kwamba iweje wajadili mapendekezo ya katiba ya Mh. Sitta
ambayo wao wameshaikubali? Baada ya mabango yale kuinuliwa yakazua
tafrani ambapo walishauriwa kutoyainua kwa sababu haukuwa mkutano wa
kisiasa na wakanyang’anywa na kuyachana ndipo vurugu/kashfa/matusi
yakaanza kutolewa dhidi ya meza kuu. Hali hii ilisababisha kushikana,
kusukumana na kurushiana viti. Katika tafrani hiyo mh. Warioba alipigwa
kibao na Mh. Paulo Makonda- ambaye ni katibu wa UVCCM TAIFA. Mtuhumiwa
huyu pamoja na wengine wanne wamekamatwa kwa mahojiano. Upelelezi
unaendelea na juhudi za kuwapata wengine zinaendelea.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Kidata atembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu NHC Mkinga
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Japan
Kidata akisikiliza maelezo ya Meneja wa miradi wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Subira Gugadi huku Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa
Shirika la Nyumba la Taifa na Mkurugenzi wa Fedha, Felix Maagi
akisikiliza, kulia kabisa ni Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera, Ng’aranga
Magai. Katibu Mkuu Kidata alitembelea mradi huo leo hii ili kuweza
kufahamu utendaji wa NHC katika miradi ya nyumba ya gharama nafuu, jana
alifungua kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la
Taifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Japan Kidata akisikiliza maelezo
ya Meneja wa miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Gugadi
huku Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la
Taifa na Mkurugenzi wa Fedha, Felix Maagi akisikiliza, kulia kabisa ni
Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera, Ng’aranga Magai.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Japan Kidata akifutilia maelezo
ya Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la
Taifa na Mkurugenzi wa Fedha, Felix Maagi katikati yao ni Meneja wa NHC
Mkoa wa Upanga, Nathaniel Malisa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Japan Kidata akisikiliza maelezo
ya Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utawala wa Mikoa wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Raymond Mndolwa, kushoto ni Meneja wa NHC Mkoa wa Dodoma,
Itandula Gambalagi
Baadhi ya nyumba zilizokamilika zinavyoonekana
Sabina Kilato wa NHC Kigoma akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii,
Susan Omari na Margareth Ezekiel, Kaimu Mkuu wa Mkadiriaji Majengo wa
NHC wakati wa ziara hiyo iliyowashirikisha Wajumbe wa Baraza Kuu la
Wafanyakazi, Mameneja na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa.
Baadhi ya Wajumbe waliokuwapo katika ziara hiyo
Baadhi ya nyumba zilizokamilika zinavyoonekana.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji
Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio akijadiliana jambo na Meneja wa NHC mkoa
wa Tanga, Isaya Mshamba na Meneja wa Rasilimali watu wa NHC, Omari
Makalamangi wakati wa ziara hiyo iliyowashirikisha Wajumbe wa Baraza Kuu
la Wafanyakazi, Mameneja na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji
Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio akijadiliana jambo na Meneja wa NHC mkoa
wa Tanga, Isaya Mshamba na Meneja wa Rasilimali watu wa NHC, Omari
Makalamangi wakati wa ziara hiyo iliyowashirikisha Wajumbe wa Baraza Kuu
la Wafanyakazi, Mameneja na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa.
Kulia ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki, Hamad Abdallah.
Meneja wa miradi wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Subira Gugadi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa
Ubunifu, Issack Peter. Katikati ni Mohammed Mneka, Katibu wa TAMICO NHC.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la
Wafanyakazi, Mameneja na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa
waliofika katika ziara hiyo.
Baadhi ya nyumba zilizokamilika zinavyoonekana.
No comments:
Post a Comment