Rais
wa tuzo za TWA Irene Kiwia akizungumza na waandishi wa habari leo
kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam wakati akielezea
maandalizi ya tuzo hizo kwa mwaka huu wa 2014, Katikati ni Mwenyekiti wa
tuzo za TWA mama Sadaka Gandi na kulia ni Hellen Kiwia katibu TWA. Mwenyekiti
wa tuzo za TWA mama Sadaka Gandi akifafanua jambo wakati wa mkutano na
waandishi wa habari alipokuwa akielezea maandalizi ya tuzo za Mwanamke
za TWA,
Kulia ni Rais wa tuzo za TWA Irene Kiwia
……………………………………………………………………………………
Taasisi ya Shirika la
kijamii TanzaniA Women of Achievement (TWA) juzi imezindua
rasmi Tuzo za Wanawake wenye MafanikioTanzania ambazo zitafanyika tarehe 7/3/2015
kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake, likiwa
na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake
ambao wamechangia maendeleo Tanzania katika nyanja tofauti.
Rais wa shirika la Wanawake Wenye Mafanikio Bi. Irene Kiwia alisema “ Lengo la
TWAA ni kusheherekea mafanikio ya wanawake hawa na kazi wanazozifanya
kwenye jamii kupitia nyanja tofauti ndani ya Tanzania.
Vigezo mbalimbali vitatumika katika
kuwachagua kama vile utofauti waliouonyesha katika jamii zao, jinsi gani wameweza
kuwavutia na kuwashawahi watu wengine, na jinsi gani wameweza kuwagusa na kuwafikia
watu tofauti
tofauti.”
Bi
Kiwia alisema kwamba “ Tuzo hizi pia zitaenda sambamba
na na mafunzo ya kujenga uwezo wa wasichana viongozi katika nyanja
tofauti walio kati ya umri wa miaka 18-27 kutoka mikoa yote ya Tanzania ambayo yatachukua
wiki
6. Wasichana hao
watakutanishwa na wanawake wanaofanya vizuri katika biashara, kazi za
jamii na idara tofauti kwa ajili ya kupewa motisha an
kujifunza. Mategemeo yetu ni kuwa baada ya mafunzo haya
wasichana wataenda kuwa chachu ya mabadiliko mikoani
kwao na kuwafundisha wenzao wengi ili kusambaza mori wa maendeleo an
mabadiliko kwa wasichana wadogo nchini kote.
Mwenyekiti wa TWAA, Mrs. Sadaka
Gandhi alisema “suala la uwezeshaji kwa wanawake linapewa
kipaumbele duniani
kote, tuzo hizi zitaonyesha uwezo na ugunduzi wa wanawake katika sehemu tofauti.
Tunaamini kuwa wale wote watakaoshiriki watakuwa chachu ya
mabadiliko kwa wasichana kutoka
vijijijini, wafanyabiashara na wanawake wengi chini Tanzania”.
“Katika kipindi cha miezi mitatu, tunaomba watu mbalimbali
wajitokeze kuchagua wanawake ambao wanafanya vizuri katika
fani zote kuanzia mfanyabishara mwenye jitihada kubwa, mwalimu wa namna
ya kipekee na hata mtu ambaye
ameweza kuleta mabadiliko muhimu katika jamii yake.” Alimalizia Mrs.
Gandi.
Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni sanaa na utamaduni, ujasiriamali, elimu, afya, sayansi
na teknolojia,
kilimo, ustawi wa
jamii, michezo, umma, mshiriki wa mafanikio mwenye umri
mdogo, mwanamke aliefanya vizuri ndani ya mwaka mzima na
mwanamke aliefanya vizuri katika maisha yake.
Washiriki wanaweza kujipendekeza ama kupendekezwa la shirika kupitia www.twa.or.tz,
info@twaa.or.tz kabla
ya tarehe 30 Januari 2015. Washiriki lazima wawe ni wakazi wa Tanzania
ambao kazi zao zimefanyika
Tanzania. Washiriki watatu katika kila kipengele watatangazwa kabla ya siku ya
sherehe ya Tuzo za Wanawake Wenye Mafanikio mwezi Machi mwakani.
Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi
Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania,
Jaji Joaquine De
Mello, Dk. Marcelina Chijoriga – kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Bwana. Innocent Mungy –
Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Sadaka Gandi – Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene
Kiwia
– Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline
Porter Novelli.
Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwa na Baileys, Delloite,
NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, TheAmerican People, DTP, UN
Development Partners Gender Group, UNFPA,
UNESCO,
UN Women,TBL, Multichoice, Africa Life Assurance, Barrick, Twiga Cement,
Vodacom, Farm Equip CompanyRBP, Clouds
FM, Thinline, Costech, Kairuki Hospital, ZARA Tours, Serena Hotel, Tigo,
African Lynx Investment, EATV na EA radio na Frontline Porter Novelli.
No comments:
Post a Comment