Kiongozi wa idara ya
utalii Arusha Bi.Anita Temba akiongea na washiriki wa shindano la Model
of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu
ya TANAPA jijini Arusha ambapo waliweza kufahamu shughuli mbalimbali
zinazofanywa na shirika hilo
Meneja Mahusiano wa TANAPA
Pascal Shelutete akizungumza na washiriki wa shindano la Model of
Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya
TANAPA jijini Arusha
Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiteta jambo na mratibu wa shindano hilo Samdia Charles
Mkurugenzi mkuu hifadhi za
Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki
wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao
katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Mkurugenzi wa utalii na masoko Ibrahim Mussa akiwa anawasikiliza washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha (hawapo pichani)ambapo aliwataka washiriki hao kutumia nafasi hiyo kutangaza utalii wa ndani
Mkurugenzi mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akipata utambulisho kutoka kwa washiriki wa shindano hilo
Washiriki wakipata picha ya pamoja nje ya jengo la makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiwa anatoa maelekezo kwa washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania
Na Pamela Mollel wa jamiiblog
Washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania wametakiwa
kutumia fursa hiyo katika kutangaza utalii wa ndani hali itakayopelekea
idadi kubwa ya watanzania kutembelea hifadhi za Taifa
Rai hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa utalii na masoko Ibrahim
Mussa ,jana wakati washiriki wa shindano hilo walipopata fursa ya
kutembelea makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Bw. Mussa aliwataka washiriki hao kutumia fursa hiyo katika
kutangaza utalii wa ndani hali itakayo pelekea idadi ya watanzania
kujitokeza kwa wingi kutembelea hifadhi za Taifa
Alisema kuwa ipo haja kwa watanzania kuona utalii ni sehemu ya
starehe ambayo unaweza kujifunza hata ukiwa na familia yako tofauti na
starehe zingineNaye Maratibu wa shindano hilo Samdia Charles alisema lengo la
kuanzishwa kwa shindano hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza
vivutio vya nchi yetu kimataifa kupitia maonyesho ya mavazai kama vile
new York fashion week,Paris fashion week na Victoria’s secret fashion
show
Aidha alisema kuwa katika shindano hilo washiriki wametoka
katika mikoa mbalimbali ya Dar es saam, Arusha,Iringa,Mbeya,Manyara,Singida,Kilimanjaro,Tanga,Tabora,Dodoma na
Mwanza Shindano hilo lilianzishwa mwaka 2013 ambapo mwaka huu kuna
jumla ya washiriki 19 kati yao 16 ni mabalozi wa hifadhi za taifa na
shindano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 22 novemba 2014katika ukumbi
wa triple A jijini Arusha
No comments:
Post a Comment