Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki, akiongea na wajumbe
wa Umoja Wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na
Kusini mwa Afrika (WOMESA) wakati wa kufunga mkutano wa sita wa mwaka wa
umoja huo uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (kushoto), akimkabidhi
cheti Mkurugenzi Msaidizi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia
Mambo ya Bahari (IMO) Pamela Tansey (kulia) katika hafla ya kufunga
mkutano wa sita wa mwaka wa Umoja Wanawake walio katika Sekta ya masuala
ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wajumbe mkutano wa sita wa mwaka wa Umoja Wanawake walio katika
Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA)
wakiwa katika mkutano huo uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam.
Wajumbe
wa mkutano wa mwaka wa WOMESA wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni
Ramsmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (wa tano
kutoka kulia waliokaa) ya mara baada ya kufunga wa mkutano huo.
…………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
WANAWAKE walio katika Sekta ya
masuala ya Bahari wameaswa kupanua wigo wa wanachama walio katika sekta
hiyo ili kuongeza ufanisi na tija katika kutekeleza majukumu yao.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki, alipokuwa akifunga mkutano wa
sita wa mwaka wa wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya
Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) unaomalizika mwishoni mwa
wiki jijini Dar es salaam.
Bi. Kairuki alisema kuwa sekta
hiyo katika nchi wanachama ni muhimu kulingana na unyeti wake licha ya
kukumbwa na changamoto ya kuwa na wataalamu wa kike wachache jambo
ambalo WOMESA imelitambua na wanalifanyia kazi kupitia mikutano na
semina mbalimbali.
“Ni jukumu lenu WOMESA
kushirikiana kwa pamoja ili kuongeza idadi ya wataalamu katika sekta hii
mkianzia na wasichana waliopo shuleni na vyuo mbalimbali vya elimu”
alisema Bi. Kairuki.
Pamoja na mkutano huo, Bi.
Kairuki amewaambia wajumbe hao wa mkutano kuwa anaamini wamepta na
kuboresha ujuzi walionao kwa kuwa wameshirikishana na kubadilishana
uzoefu kutoka nchi wanachama wa WOMESA ambapo maarifa hayo yataendelea
kuwaongezea tija na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao kama akina
mama na watalaam katika masuala ya bahari.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,
Mwenyekiti wa WOMESA kanda ya Afrika kutoka Mauritius Bi. Meenaksi
Bhirugnath-Bhookun amesema kuwa WOMESA inakabiliwa na changamoto ya kuwa
na wanawake wachache katika sekta ya bahari.
Aidha Bi. Meenaksi amesema kuwa
katika mkutano wao wa mwaka wamefikia makubaliano ya kuongeza wanachama
kupitia mamlaka za masuala ya bahari, Idara mbalimbali zinazohusu
masuala ya bandari, shule za sekondari na vyuo mbalimbali katika nchi
wanachama.
Naye Mwenekiti Msaidizi WOMESA
tawi la Tanzania Dkt. Tumain Gurumo ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo
cha Ubaharia cha Dar es salaam (DMI) amesema kuwa sekta ya bahari
inafursa nyingi amewaasa wazazi wawaruhusu watoto wa kike kujiunga
kwenye elimu ya bahari ambapo bado kuna fursa nyingi ili waweze
kuboresha maisha yao na taifa kwa ujumla.
Dkt. Tumain amewato wasiwasi
wazazi na watoto wa kike ambapo amesema kuwa teknolojia imekuwa na
imepanua wigo wa wanawake kwenye masuala ya bahari, hivyo wanawake
wanaweza kama walivyo wanaume katika sekta hiyo.
katika mkutano huo,
WOMESA wamezindua mpango makakati wa miaka mitano unaoanza mwaka 2014
hadi 2019 ikiwa ni mpango wa kuuimarisha umoja huo katika ngazi ya
kitaifa na kanda.
Mkutano wa sita wa WOMESA, mwaka
huu umeongozwa na kauli mbiu inayosema “Wanawake katika sekta ya bahari
baada ya 2014: Wakijenga jukwaa endelevu”.
Nchi zilizoshiriki mkutano huo wa mwaka ni Tanzania, Kenya, Komoro, Mauritius, Namibia na Visiwa vya Shelisheli.
Nchi nyingine ni wanachama
ambazo hazikushiriki mkutano wa mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali
ni Angola, Sudani, Lesotho, Uganda, Somalia, Eritrea, Botswana, Rwanda,
Madagaska, Afrika Kusini, Msumbiji, Burundi, Malawi, Djibout, Zimbabwe, Ethiopia na Zambia.
No comments:
Post a Comment