Wanafunzi wakiwa wamekaa chini
darasani kwa kukosa madawati wakati halmashauri ya mji inazunguukwa na
mistu kibao na wanachi wanashindwa kutengeneza madawati ni abu kwan
wazazi kukka chini watoto.
Walimu na wazazi wanafunzi
wanaokaa chini shule ya msingi kawanzige halmashauri ya mji wa Mpanda
wakimsikiliza mkuu wa Wilaya alipokuwa akiwaeleza umuhimu wa kuwahudumia
watoto ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata elimu bora kwa kukaa
kwenye dawati haina maana.
Mkuu wa wilaya akiwa na
wanafunzi wa darasa la tatu na tano kwenye chumba kimoja cha darasani
kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa wanalazimika kutumia chumba
kimoja kusomea kwa wakati mmoja hali ambayo haiendani na taratibu za
miongozo na sera ya elimu madarasa tofauti kusomea darasa moja tena kwa
wakati mmoja.
(Picha na Kibada Kibada -Katavi)
………………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Katavi.
Upungufu wa vyumba vya madarasa
katika shule ya Msingi Kawanzige Halmashauri ya Mji wa Mpanda umechangia
wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kukaa chini na wengine wa
darasa la tatu na la tano kukaa darasa na kuwapa wakati mgumu walimu
kufundisha madarasa mawili tofauti.
Hayo yalibainika wakati Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alipofanya ziara ya kushitukiza
kutembelea shule hiyo na kukuatana sakata hilo la watoto wa shule ya
Msingi Kawanzige kukaa chumba kimoaja madarasa mawili tofauti.
Akizungumzia mbele ya Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Mwalimu Mkuu Msaidizi Masele Kibona na mwalimu wa
Taaluma katika shule hiyo walieleza kuwa shule hiyo yenye wananfunzi
wapatao 484 ina mikondo 12 kuanzia darasa la (I-Vii) inakabiliwa na
upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hali inayofanya wanafunzi wakae
chini na wengine wakae chumba kimoja madarasa tofauti.
Mwalimu Kibona alieleza kuwa
shule hiyo ina vymba vine vya madarasa na upungufu ni vyumba vine , na
hakuna nyumba ya mwalimu hata mmoja katika shule hiyo.
Mbali ya upungufu huo wa vyumba
vya madarsa pia upo upungufu mkubwa wa matundu ya vyuo ambapo shule
inahitaji matundu ya vyoo 14 lakini yaliyopo ni matundu matatu tu amabyo
hayatoshelezi mahitaji kwa wanafunzi hao.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa
Wilaya amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda
Seleman Lukanga aliyewakilishwa na Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Mji wa Mpanda Zena Kapama aliagizwa kuhakikisha
wanashughulikia changamoto ya upungufu wa madarasa katika shule hiyo.
Akatakiwa kuangalia katika
bajeti yao kuona namna ya kushughulikia changamoto inayoikabili shule
hyo ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi kuchangia katika
ufyatuaji wa tofali,kusomba mchanga na serikali inachangia vifaa ya
ujenzi vya dukani mabati,nondo na misumari na rangi nakadhalika hivyo
wajibu wa wananchi kuhakikisha wanachangia katika ujenzi wa shule kwa
kuwa shule ni mali ya wananchi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima ameutupia lawama uongozi wa Halmashauri
ya Mji wa Mpanda kwa kushindwa kuwatembelea wananchi na kubaini
changamoto zinazowakabili badala yake wanakaa ofisini bila kuwatembelea
wananchi na kubaini changamoto wanazokabiliana nazo.
Alilazimika kutoa kauli hizo
baada ya kubaini kuwa zipo kero nyingi kwa wananchi ambazo zingeweza
kupatiwa ufumbuzi na watalaam iwapo wangekuwa wanawatembelea wananchi na
kubainichangamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi kuliko kusubiri
mpaka viongozi wa ngazi ya wilaya au Mkoa kufanya ziara ya kukagua
maendeleo.
Viongozi kama Mkuu wa Wilaya,
Mkoa na Viongozi wa Kitaifa ambapo wananchi wanakuwa na kero ambazo
zingeweza kupatiwa ufumbuzi na watalaamu na siyo kusubiri viongozi wa
ngazi za juu, maana kero zinakuwa nyingi bila kupatiwa majibu.
Kufuatia hali hiyo amewaagiza
watendaji wote kutoka maofisini na kufanya ziara ya kutembelea vijijini
na kupata changamoto na kuzifanyia kazi ili kuzipatia ufumbuzi ili
kuwaondolea kero wananchi na kuwaletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment