Baraza
la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), limelaani
vikali vurugu alizofanyiwa aliyekuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, katika mdahalo wa kujadili
Katiba inayopendekezwa jijini Dar es Salaam.
Pia, limewataka vijana wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha)
kutowavumilia watu wanaosadikiwa kumfanyia Warioba vurugu hizo
wanaodaiwa kutoka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).
Akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Maswa katika
mkutano wa hadhara juzi, Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee, alisema
kitendo alichofanyiwa Jaji Warioba na wenzake kinatakiwa kulaaniwa na
Watanzania wote.
Alisema ni jambo la kusikitisha na kufedhehesha sana kuona
nchi inafikia hapo, kwa kumfanyia kitendo cha ajabu kiongozi mkubwa na
mwadilifu kama yule ambaye amelitumikia taifa kwa moyo na nguvu zake
zote.
“Jaji Warioba ambaye amefanya kazi nzuri katika taifa hili,
leo hii anafanyiwa vitendo kama hivi, nchi hii inakwenda wapi jamanii,
hatuwezi kuvumilia nchi iendeshwe namna hii, lazima hatua zichukuliwe,”
alisema Mdee.
No comments:
Post a Comment