Na Owen Mwandumbya, Victoria Falls, Zimbabwe
Mkutano wa 36 wa Jukwaa la
Mabunge ya Nchi wanachama wa SADC (SADC PF) ulioanza wiki hii mjini
Victoria Falls nchini Zimbabwe na unatarajiwa kumalizika tarehe 3
Novemba, 2014, ikiwa ni baada ya kukamilika kwa ajenda ya Mkutano huu
pamoja na kufanyika kwa uchaguzi wa Rais wa chama hicho atakayeongoza
jukwaa hilo kwa miaka miwili ijayo.
Kauli mbiu ya mkutano huu ni
“Bunge la kikanda la SADC – Wakati ni huu” ama kwa lugha ya kimombo
inasema “ SADC Regional Parliament – the Future is Now”.
Maneno yaliyo katika kauli mbiu
ya Mkutano huu yamebeba ujumbe mzito sana wa Mabunge ya Nchi za SADC
ikiwa ni dhamira ya dhati waliyokuwa nayo wanachama hawa ya kuundwa kwa
Bunge la kikanda litakalokuwa na nguvu si tu ya kuzisimamia Serikali za
Nchi Wanachama bali pia kuwa na uhalali wa kuhakikisha kuwa maamuzi na
hata mikataba mbalimbali itakayofikiwa na chombo hiki katika ukanda huu
vinatekelezwa katika nchi wanachama.
Pamoja na kwamba yapo mengi
yaliyojadiliwa katika Mkutano huu wa Umoja wa Mabunge ya SADC hapa
Zimbabwe, muhimu limekuwa ni uchaguzi wa Rais wa Jukwaa hili ambaye
ataongoza jitihada za kufanikisha malengo ya chama hiki ya kufikia kuwa
Bunge kamili ndani ya Miaka miwili ijayo yanafanikiwa.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.
Anne Makinda amekuwa akipigiwa chapuo na Wajumbe wengi wa Mkutano ili
aweze kukamata usukani wa kukiongoza chama hiki kwa miaka miwili ijayo
baada ya Rais wa sasa ambaye pia ni Spika wa Mauritius Mhe. Abdool
Razack Mahomed Ameen Peeroo, kumaliza muda wake. Kutokana na uungwaji
mkono mkubwa alionao Mhe. Makinda ameibuka kuwa mgombea pekee na hivyo
ni dhahiri atapitishwa na kukabidhiwa jukumu la kuongoza Jukwaa hili.
Msukumo wa Wajumbe wa Mkutano
huu wa 36 kutaka Spika Makinda aweze kuongoza Bunge hili unatokana na
heshima na ushawishi mkubwa ilivyonayo nchi ya Tanzania katika nchi
wanachama wa SADC swala ambalo linafanya wajumbe wengi wa Umoja huu
waamini kuwa Mtanzania Makinda atasaidia sana kusukuma masuala ya Jukwaa
hili kwa Wakuu wa nchi wanachama, kazi ambayo inahitaji mtu kutoka nchi
inayokubalika na yenye sifa za kidemokrasia ya kweli kwa na hivyo
kuweza kupenyeza na kufanikisha matakwa ya Bunge hili.
Kukubalika kwa Tanzania katika
Ukanda wa huu wa Afrika Kusini na chapuo anayopigiwa Makinda ya kuongoza
Bunge la SADC vinatokana na historia iliyoandikwa na Tanzania kupitia
harakati za Ukombozi
wa Bara la Afrika kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1960. Kuanzia wakati
huo nchi ya Tanzania chini ya Uongozi wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, iliongoza mapambano ya ukombozi Barani Afrika
na kutoa msaada mkubwa kwa Vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile, Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).
Continue reading →
No comments:
Post a Comment