Katibu
wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha vitu
alivyokwenda navyo kwenye mdahalo huo ambavyo ni katiba ya sasa na
katiba pendekezwa kwa ajili ya kutumia kujibu hoja mbalimbali wakati wa
mdahalo huo, Makonda amelaani na kukanusha kuwa hakumpiga Mzee Warioba
isipokuwa alikuwa na kazi moja ya kuhakikisha anamsaidia Anold Kayanda
mwandishi wa BBC ambaye aliumizwa katika vurugu hizo na Mzee Warioba
na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba asiyeona Amon Mpanju
wakati wa vurugu zilizotokea katika mdahalo wa kujadili rasimu ya
Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza
jana, ambapo Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph
Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari,
Dar es Salaam. Pia Makonda amesema kuwa hawezi kabisa kudiriki kumpiga
kwani anamheshimu kama babake mzazi. Amesema kuwa hata leo asubuhi
amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye
amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo
No comments:
Post a Comment