Mahmoud Ahmad Arusha
Tamasha la upendo kwa mama
lilofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kushindwa kumalizika
sababu ya mvua linatarajiwa kurudiwa mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza kabla ya kuahirishwa
kwa Tamasha hilo mratibu wa tamasha hilo Carlos Mkundi alisema kuwa
tamasha hilo litarudiwa na hakutakuwa na kiingilio tarehe 30 ya mwezi
huu huku akiwataka kuwa na moyo wa uvumilivu kwani kila jambo linahitaji
uwepo wa bwana.
Hata hivyo kabla ya wasanii
Christina Shusho na Upendo Nkone kupanda jukwaani mvua kubwa ilianza
kunyesha hivyo kukatiza kiu ya wauumini mbalimbali waliojitokeza kupata
burudani ya nyimbo za injili iliyokuwa itolewe na wasanii hao.
Iliwabidi waimbaji maarufu wa
nyimbo za injili waliokuwa wakijiandaa kupanda jukwaani ndipo mvua kubwa
iliyoambatana na upepo ilianza kunyesha hali iliyowafanya wasanii hao
kuimba bila ya kutumia vyombo na kipaza sauti huku washiriki wakiimba
pamoja nao na baadae kuahirishwa kwa tamasha hilo.
Awali kabla ya wasanii hao
kuwasili katika uwanja huo makundi mbali mbali yaliwapa burudani waumini
mbali mbali waliofika katika uwanja huo wakisubiri kuona burudani
kutoka kwa wasanii nguli wa nyimbo za injili akiwemo Martha
mwaipaja,Christina Shusho,Carlos Mkundi,Matumaini, na Upendo Nkone.
Hakika tamasha hilo lilijaa
furaha kwa waumini na wakazi mbal;I mbali wa jiji la Arusha kujitokeza
kwa mamia kujakushuhudia burudani hiyo huku wakiimba na kucheza muziki
wa kumtukuza mungu kwa furaha.
Ndipo katika hali isiyo ya
kawaida mvua ilianza kunyesha majira ya saa 11 jioni na kukatiza
burudani hiyo huku wakazi hao wa jiji la Arusha kulazimika kukimbilia
jukwaa kuu kujificha mvua hvyo tamasha kuahirishwa hadi mwishini mwa
mwezi huu.
No comments:
Post a Comment