TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, January 18, 2015

KINANA AUNGURUMA WILAYA YA DIMANI MKOA WA MJINI MAGHARIBI ZANZIBAR LEO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd mara baada ya kupokelewa katika Ofisi kuu ya CCM mkoa wa Mjini Magharibi  wilaya ya Dimani Zanzibar akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba, Katibu Mkuu Kinana anaongozana na Nape Nauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama, Katika mkutano wa ndani akiongea na wajumbe wa mkutano mkuu wa Halmashauri ya mkoa wa  mjini Magharibi  Kinana amesema katika mambo muhimu ambayo kamati za siasa zinatakiwa kuzingatia wakati wa kuteua wagombea mbalimbali ni Maadili ya viongozi, Ameongeza kwamba kama kuna kamati ya siasa itakiuka utaratibu huo na ikaonekana kubeba baadhi ya wagombea basi Kamati Kuu  haitasitakufuata utaratibu wa kikatiba na  kuteua kamati ya siasa nyingine ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea wote walioomba uongozi.
 Nape Nauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongozana na Vuai Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu Zanzibar mara baada ya kuwasili ofisi kuu ya CCM Kiembesamaki mkoa wa Mjini Magharibi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wajumbe mbalimbali na wa wana CCM wakati alipowasili wilaya ya Kiembesamaki wilaya ya Dimani mkoa wa Mjini Magharibi leo.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Yusuf Mohamed Yusuf akimkaribisha Ndugu Abdulrahman Kinana ili kuongea na wajumbe wa halmashauri ya wilaya ya Dimani.
  Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, kulia Vuai Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na kushoto ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Bi. Khadija Abood wakiwa katika mkutano huo.
 Mjumbe wa Kamati kuu wa CCM Mh. Balozi Seif Ali Idd akizungumza katika mkutano huo wa ndani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe hao hawapo pichani.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Kirtkumar Dave Meneja wa Kiwanda cha maziwa cha Azam kilichopo Fumba Unguja wakati alipotembelea kiwanda hicho na kukagua shughuliza uzalishaji kiwandani hapo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya Meneja wa kiwanda cha maziwa cha Azam Bw.Kirtkumar Dave
 
 SEhemu ya mitambo ya uzalishaji wa kiwanda hicho
 Meneja wa kiwanda hicho Kirtimar Kumar akimueleza jambo Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uzalishaji wa kiwanda hicho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia baadhi ya maziwa yaliyozalishwa kiwandani hapo.
 
 Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akishiriki kupatkia katoni za maziwa kwenye kiwanda hicho.
 Meneja wa kiwanda hicho Kirtimar Kumar akimzawadia  katoni ya maziwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.akipokelewa na Profesa David Mfinaga Naibu wa Makamu Mkuu wa chuo cha UDSM wakati alipotembelea chuo Sayansi ya Bahari Shakani
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. akizungumza na baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusafisha eneo la chuo hicho kinachoendelea kupanuliwa , kulia ni Profesa David Mfinaga Naibu wa Makamu Mkuu wa chuo cha UDSM na kushoto ni Ndugu Vuai Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua majengo ya chuo hicho huku akiongozwa na Profesa David Mfinaga Naibu wa Makamu Mkuu wa chuo cha UDSM katikati ni Desiderius Masalu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka chuoni hao.
 Msafara wa Katibu Mkuu ukikatiza katika msitu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mikoko huko Fumba kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Yusuf Mohamed Yusuf.
 Hapa akishiriki zoezi la uhifadhi wa Kaa
 Akizindua Gari la wagonjwa Ambulance
 Wananchi na wana CCM wakinyanyua mikono yao juu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Magereza..
 Balozi Ali Karume akiwahutubia wananchi katika mkutano huo
 Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kwenye viwanja vya  Magereza.
 Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Magereza Zanzibar
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaongoza wana CCM wapya kula kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi zao zauanachama

Ridhiwani Kikwete ashiriki mazishi Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa Pwani, SALEHE MPWIMBWI



 KAKA wa Rais Jakaya Kikwete Selemani Kikwete akiweka mchanga katika
  Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la Salehe Mpwimbwi aliyezikwa   katika makaburi yaliyopo nje kidogo ya kijiji cha Miono, mazishi   yaliyofanyika juzi baada ya Mpwimbwi kupata ajali akiwa kwenye gari   yake binafsi akitokea kijiji cha jirani kumpeleka mgonjwa ambapo   njiani gari lake lilipasuka taili na kupinduka. (PICHA NA OMARY SAID).
MBUNGE Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiweka mchanga kwenye
  kaburi la Salehe Mpwimbwi aliyezikwa katika makaburi yaliyopo nje
  kidogo ya kijiji cha Miono, mazishi yaliyofanyika juzi baada ya
  Mpwimbwi kupata ajali akiwa kwenye gari yake binafsi akitokea kijiji   cha jirani kumpeleka mgonjwa ambapo njiani gari lake lilipasuka taili na kupinduka. (PICHA NA OMARY SAID).

PINDA AMTEMBELEA MBUNGE VITA KAWAWA HOSPITALI ALIKOLAZWA

Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akimpa pole Mbunge wa Namtumbo, MheshimiwaVita Kawawa ambaye amelazwa katika hospitali ya AMI jijini Dar es salaam kwa matibabu. Kushoto ni mke wa mbunge huyo, Siwa Kawawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Matukio Picha Hafla ya Wanahabari na Kampuni ya Afrika Internet Holding

Meneja wa Kampuni ya Lamudi nchini Tanzania, Godlove Nyagawa akizungumza na wageni waalikwa wanahabari na wadau wengine wa kampuni hiyo kwenye hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na Afrika Internet Holding.
Meneja wa Kampuni ya Lamudi nchini Tanzania, Godlove Nyagawa akizungumza na wageni waalikwa wanahabari na wadau wengine wa kampuni hiyo kwenye hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na Afrika Internet Holding.Meneja wa Kampuni ya Kaymu.com nchini Tanzania, Erfam Mosgani (kushoto) akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya kufahamiana na kubadilishana uzoefu na wanahabari iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Holding.
Meneja wa Kampuni ya Kaymu.com nchini Tanzania, Erfam Mosgani (kushoto) akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya kufahamiana na kubadilishana uzoefu na wanahabari iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Kutoka kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Kaymu.com nchini Tanzania, Erfam Mosgani (kushoto), Meneja Mwendeshaji wa Mo Blog, Mr. Zainul M. na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Mahusiano Kaymu.com, Angaza Nkurlu wakibadilishana uzoefu katika hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Holding.
Kutoka kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Kaymu.com nchini Tanzania, Erfam Mosgani (kushoto), Meneja Mwendeshaji wa Mo Blog, Mr. Zainul M. na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Mahusiano Kaymu.com, Angaza Nkurlu wakibadilishana uzoefu katika hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na kampuni ya Ofisa Msaidizi Kitengo cha Uhusiano wa Kampuni ya Lamudi Tanzania, Lilian Kisasa (katikati) akibadilishana uzoefu na baadhi ya wanahabari katika hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Holding.
Ofisa Msaidizi Kitengo cha Uhusiano wa Kampuni ya Lamudi Tanzania, Lilian Kisasa (katikati) akibadilishana uzoefu na baadhi ya wanahabari katika hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Holding.
Afrika Internet Holding.
Meneja wa Kampuni ya Jumia nchini Tanzania, Sabrina Dorman (kushoto)akizungumza na baadhi ya wageni waaliwa (wanahabari) katika hafla ya kufahamiana na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding.
Meneja wa Kampuni ya Jumia nchini Tanzania, Sabrina Dorman (kushoto)akizungumza na baadhi ya wageni waaliwa (wanahabari) katika hafla ya kufahamiana na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding.IMG_0032 IMG_0027 Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.Meneja wa Kampuni ya Jumia nchini Tanzania, Sabrina Dorman (katikati) akizungumza na baadhi ya wageni waaliwa (wanahabari) katika hafla ya kufahamiana na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding.
Meneja wa Kampuni ya Jumia nchini Tanzania, Sabrina Dorman (katikati) akizungumza na baadhi ya wageni waaliwa (wanahabari) katika hafla ya kufahamiana na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Carmudi Afrika Mashariki, William Day (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa maofisa wa kampuni yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Carmudi Afrika Mashariki, William Day (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa maofisa wa kampuni yake.Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.

WANANCHI MKURANGA WAASWA KUCHANGIA DAMU.

Jengo la Wodi ya watoto la hospitali ya wilaya ya Mkuranga litakalonufaika na msaada wa mashuka yaliyotolewa na chuo cha CBE jana. 

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) msaada wa mashuka yenye 90 yaliyotolewa na chuo hicho kusaidia wagonjwa katika hospitali hiyo.Makabidhiano hayo yalifanyika jana wilayani Mkuranga kama  sehemu ya Chuo hicho kuadhimisha miaka 50 toka kianzishwe mwaka 1965. 

 Baadhi ya Wauguzi na wahudumu wa afya wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga wakiangalia moja ya shuka kati ya mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu msaada wa mashuka  90 yaliyotolewa na chuo hicho katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga ikiwa ni sehemu ya mpango wa chuo hicho kutoa huduma kwa jamii.
Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga jana.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) kabla ya kukabidhiwa msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na CBE kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
18/1/2015. Mkuranga, Pwani.

Wananchi wilayani Mkuranga wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia  damu kwenye  benki ya damu iliyoko katika hospitali ya wilaya hiyo ili kupunguza tatizo la uhaba wa damu linaloikabiri hospitali hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Mkuranga na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya  hiyo, Dkt. Anwar Milulu wakati akipokea msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara Dar  es salaam (CBE) kwa lengo la kuwasaidia wagojwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.

Alisema kuwa hospitali hiyo kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu kutokana na mwamko mdogo wa wakazi wa wilaya hiyo wanaojitokeza kuchangia damu jambo linalosababisha upungufu wa damu na usumbufu kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu .

“Kama mnavyoona hospitali yetu iko barabarani kwa sasa tunakabiliwa na tatizo la upungufu wa damu, baadhi ya wagonjwa hutufikia wakiwa katika hali mbaya  ya kuhitaji kuongezewa damu kiasi cha  kutufanya tuwapeleke katika hospitali ya Taifa Muhimbili  kuokoa maisha yao” Alisema Dkt. Milulu.

Alieleza kuwa lishe duni na kutozingatia ulaji wa mboga za majani kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuendelea kwa tatizo la upungufu wa damu kwa akina mama wajawazito na watoto.

Dkt. Milulu alifafanua kuwa hospitali hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wagonjwa hususan akina mama wajazito na watoto pindi wanapohudhuria Kliniki kwa lengo la kuwaeleza umuhimu wa uzingatiaji wa lishe bora na namna ya  kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu miongoni mwa jamii.

Aidha, alisema Serikali inaendelea kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya ukosefu wa maji,uhaba wa miundombinu  na dawa yanayoikabili hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa kawaida na wale walio katika makundi maalum wanaohudumiwa na hospitali hiyo ikilinganishwa na uwezo wake.

“Serikali inaendelea kushughulikia tatizo la maji,miundombinu na upungufu wa dawa unaoikabili hospitali yetu maana idadi ya wananchi tunaowahudumia ni wengi ikilinganishwa na uwezo wa miundombinu ya hospitali”

Kuhusu changamoto ya rasilimali watu na wataalam wa kada mbalimbali alisema kwa sasa hospitali hiyo  ina idadi inayoridhisha ya  Madaktari, Wauguzi, wahudumu, wataalam wa maabara na madereva ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Alitoa wito kwa uongozi wa chuo hicho kuendelea kuisaidia hospitali hiyo katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanafunzi wa chuo cha CBE kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara  ili  kuokoa maisha ya wagonjwa.

Nao baadhi ya wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma katika hospitali hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti licha ya kuushukuru uongozi wa chuo cha CBE kwa kuwakumbuka kwa kuwapatia msaada wa mashuka hayo walikiri kuwepo kwa mwamko mdogo wa wananchi  kuchangia damu katika benki ya damu ya hosptali hiyo.

Aidha, waliiomba Serikali kulishughulikia tatizo la  maji , miundombinu na uhaba wa dawa uliopo katika hospitali hiyo na kuwaomba wadau wengine wajitokeze kuisaidia hospitali hiyo ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Awali akizungumza msaada huo Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema alisema kuwa chuo chake ifikapo Januri 21, 2015 Chuo cha  Elimu ya Biashara kinatimiza miaka 50 hivyo msaada walioutoa ni sehemu ya huduma kwa jamii.

Alisema katika kuelekea kutimiza  miaka 50 ya chuo cha CBE mbali na kujikita katika masuala ya kuelimisha jamii katika taaluma  mbalimbali ikiwemo Biashara, Ugavi na manunuzi, Vipimo, TEHAMA na Utawala katika biashara kimekua kikitoa huduma mbalimbali kwa jamii.

Alisema katika kuelekea maadhimisho ya miaka 50 chuo hicho kimekuwa kikitoa misaada ya vitu mbalimbali na elimu ya ujasiriamali kwa wananchi katika mikoa yote ambayo kina matawi yake ikiwemo Dar es salaam, Mbeya, Zanzibar, Mwanza na Dodoma.