Jengo la
Wodi ya watoto la hospitali ya wilaya ya Mkuranga litakalonufaika na msaada wa
mashuka yaliyotolewa na chuo cha CBE jana.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) msaada wa mashuka yenye 90 yaliyotolewa na chuo hicho kusaidia wagonjwa katika hospitali hiyo.Makabidhiano hayo yalifanyika jana wilayani Mkuranga kama sehemu ya Chuo hicho kuadhimisha miaka 50 toka kianzishwe mwaka 1965.
Baadhi ya Wauguzi na wahudumu wa afya wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga wakiangalia moja ya shuka kati ya mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na chuo hicho katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga ikiwa ni sehemu ya mpango wa chuo hicho kutoa huduma kwa jamii.
Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga jana.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) kabla ya kukabidhiwa msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na CBE kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

18/1/2015. Mkuranga,
Pwani.
Wananchi wilayani
Mkuranga wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwenye benki ya damu iliyoko katika hospitali ya
wilaya hiyo ili kupunguza tatizo la uhaba wa damu linaloikabiri hospitali hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa
jana wilayani Mkuranga na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya hiyo, Dkt. Anwar Milulu wakati akipokea
msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kwa lengo la kuwasaidia
wagojwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Alisema kuwa hospitali
hiyo kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu kutokana na mwamko
mdogo wa wakazi wa wilaya hiyo wanaojitokeza kuchangia damu jambo
linalosababisha upungufu wa damu na usumbufu kwa wagonjwa wanaohitaji
kuongezewa damu .
“Kama mnavyoona hospitali
yetu iko barabarani kwa sasa tunakabiliwa na tatizo la upungufu wa damu, baadhi
ya wagonjwa hutufikia wakiwa katika hali mbaya ya kuhitaji kuongezewa damu kiasi cha kutufanya tuwapeleke katika hospitali ya
Taifa Muhimbili kuokoa maisha yao”
Alisema Dkt. Milulu.
Alieleza kuwa lishe
duni na kutozingatia ulaji wa mboga za majani kama inavyoshauriwa na wataalam
wa afya ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuendelea kwa tatizo la upungufu
wa damu kwa akina mama wajawazito na watoto.
Dkt. Milulu alifafanua
kuwa hospitali hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wagonjwa hususan akina mama
wajazito na watoto pindi wanapohudhuria Kliniki kwa lengo la kuwaeleza umuhimu
wa uzingatiaji wa lishe bora na namna ya
kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu miongoni mwa jamii.
Aidha, alisema Serikali
inaendelea kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya ukosefu wa maji,uhaba wa
miundombinu na dawa yanayoikabili
hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa kawaida na wale walio
katika makundi maalum wanaohudumiwa na hospitali hiyo ikilinganishwa na uwezo
wake.
“Serikali inaendelea
kushughulikia tatizo la maji,miundombinu na upungufu wa dawa unaoikabili
hospitali yetu maana idadi ya wananchi tunaowahudumia ni wengi ikilinganishwa
na uwezo wa miundombinu ya hospitali”
Kuhusu changamoto ya
rasilimali watu na wataalam wa kada mbalimbali alisema kwa sasa hospitali hiyo ina idadi inayoridhisha ya Madaktari, Wauguzi, wahudumu, wataalam wa
maabara na madereva ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Alitoa wito kwa uongozi
wa chuo hicho kuendelea kuisaidia hospitali hiyo katika masuala mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanafunzi wa chuo cha CBE kujitokeza kuchangia
damu mara kwa mara ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Nao baadhi ya wananchi
waliokuwa wakipatiwa huduma katika hospitali hiyo wakizungumza kwa nyakati
tofauti licha ya kuushukuru uongozi wa chuo cha CBE kwa kuwakumbuka kwa
kuwapatia msaada wa mashuka hayo walikiri kuwepo kwa mwamko mdogo wa
wananchi kuchangia damu katika benki ya
damu ya hosptali hiyo.
Aidha, waliiomba
Serikali kulishughulikia tatizo la maji
, miundombinu na uhaba wa dawa uliopo katika hospitali hiyo na kuwaomba wadau
wengine wajitokeze kuisaidia hospitali hiyo ili iweze kutoa huduma bora kwa
wananchi.
Awali akizungumza msaada
huo Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema alisema kuwa
chuo chake ifikapo Januri 21, 2015 Chuo cha Elimu ya Biashara kinatimiza miaka 50 hivyo
msaada walioutoa ni sehemu ya huduma kwa jamii.
Alisema katika kuelekea
kutimiza miaka 50 ya chuo cha CBE mbali
na kujikita katika masuala ya kuelimisha jamii katika taaluma mbalimbali ikiwemo Biashara, Ugavi na manunuzi,
Vipimo, TEHAMA na Utawala katika biashara kimekua kikitoa huduma mbalimbali kwa
jamii.
Alisema katika kuelekea
maadhimisho ya miaka 50 chuo hicho kimekuwa kikitoa misaada ya vitu mbalimbali
na elimu ya ujasiriamali kwa wananchi katika mikoa yote ambayo kina matawi yake
ikiwemo Dar es salaam, Mbeya, Zanzibar, Mwanza na Dodoma.
No comments:
Post a Comment