Kaimu
Mkurugenzi Wilaya ya Momba Bw. Severine Chamkaga akifungua semina ya
Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za
Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya. Wa pili kulia
ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Bibi Ester Riwa, wa kwanza kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka
Wizara hiyo Bi. Amina Sanga, na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha
Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele. Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa
akitoa mada wakati wa semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya
Momba Mkoa wa Mbeya.
Afisa
Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada wakati wa semina ya Vijana kuhusu
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi
jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya.
Mkuu
wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada wakati
wa semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali,
Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya.
Kijana
Adam Zacharia Kinyakile wa pili kulia anayeinua vipaji vya vijana na
kutengeneza ajira kwa vijana katika fani ya ufundi gereji Mji wa Tunduma
Wilaya ya Momba akiwaonyesha maafisa waliomtembelea katika shughuli
zake “Mobile Garage” aliyoitengeneza mwenyewe kwa kutumia vyuma
chakavu inayoitumia kufanyia kazi za gereji mahali popote
anapohitajika. Kushoto ni Mwenzeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamduni na Michezo Bibi Ester Riwa pamoja na timu kutoka Wizara hiyo.
Afisa
Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga wa pili kushoto (waliokaa) akizungumza na Vijana
wa kikundi cha Matunda Wilaya ya Momba walipowatembelea wakati wa ziara
ya kukagua miradi ya Vijana Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya. Wa kwanza
kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na
wa pili kushoto ni Mwenzeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa.
(Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo. Momba, Mbeya)
No comments:
Post a Comment