NA Eleuteri Mangi- MAELEZO
Uelimishwaji bado unahitajika kwa
wafanya biashara nchini katika na kuhakikisha wazingatia na kusimamia
matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za EFD.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha
Saada Mkuya Salum alipofanya ziara ya kushtukiza katika soko la
Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia
matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia
mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na
kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini.
“Nasisitiza wafanyabiashara wote nchini kutumia mashine za
kielektroniki za EFD katika biashara zao, niwaombe muwe na mwamko wa
ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi yetu ” alisema Waziri Saada.
Zaidi nya hayo, Waziri amesisitiza kuwa wafanyabiashara
wajisajili katika mfumo wa VAT ili kuokoa mapato yanayopotea ambapo
ameeleza kuwa nchi zilizoendelea wanatoa misaada kwa nchi zinazoendelea
kutokana na makusanyo ya wananchi wa nchi hizo kujali na kuthamini
kulipa kodi kutoka wafanyabiashara na watumishi wengine.
Pia Waziri Saada aliuagiza uongozi wa TRA kuwa karibu na
wafanyabiashara kwa naq kutoa namba zao za simu ili wateja waweze
kuwasiliana nao mara mashine zao zinapokuwa na hitilafu na kutoa taarifa
kwa haraka badala na kuwa na ufanisi wa haraka nan wenye tija kwa
taifa.
Naye Kaimu Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Elias Balongo amesema kuwa wataendelea kutoa elimu
kwa wananchi wote kutambua umuhimu wa kudai risiti baada ya kununua
bidhaa na kwa wafanyabiashsra kutoa risiti baada ya kuuza bidhaa.
Kwa upande wake mfanyabiashara wa Namanga jijini Dar es salaam
Saleh Kassim Seif alisema kuwa wanaishukuru Serikali kuanzisha mfumo wa
matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD kwani unamanufaa kwao ambapo
unawasaidia kujua mauzo yao ya siku, wiki, mwezi hadi mwaka ili ambapo
wameweza kuboresha bishara zao kwa kuwa na kumbukumbu sahihi ya mauzo
yao.
Aidha, mfanyabiashara huyo alisema kuwa wanapata changamoto ya
mashine hizo kuharibika wanaomba zitengenezwe ndani ya saa 24 ili waweze
kutoa huduma yenye kuzingatia sheria, kanuni na taraibu za buiashara
nchini.
Katika ziara hiyo, Waziri wa Fedha aliandamana viongozi wa wa
mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA, waandishi wa habari na baadhi ya
maafisa wa saerikali.
No comments:
Post a Comment