Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akiwahutubia wageni mbalimbali
waliohudhuria sherehe sherehe za miaka 50 ya CBE leo jijini Dar es
salaam.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
…………………………………………………………………………………………………………
Mahmoud Ahmad Dar es Salaam
Chuo cha Biashara CBE kimetakiwa kufungua Tawi la chuo hicho
Zanzibar na serikali itatoa ushirikiano kufanikisha ilikuweza kusogeza
huduma ya chuo hicho na kuongeza wigo wa Udahili kwa wanafunzi wa Upande
wa Zanzibar kwani kitawanufaisha wananchi hao bila ya kusahau utoaji wa
elimu bora.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa
Pili wa Raisi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd
wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini ya chuo hicho yaliofanyika jijini
hapa huku akisema kuwa Mtu wa miaka hamsini si nongwa kuwa na watoto
watano akiwa na maana ya wao ya chuo hicho kufungua tawi 5 Zanzibar.
Balozi Idd alisema kuwa Serikali
ya SMZ itasaidia katika kuanzishwa kwa Tawi la chuo hicho Zanzibar ili
kuongeza udahili wa wanafunzi wengi wenye weledi kwa upande wa Zanzibar
kwenye sekta ya Biashara utakaosaidia ukuaji wa maendeleo endelevu na
nyadhifa ndani ya serikali huku akiwataka kutoa elimu bora yenye viwango
vya kitamaifa.
Alisema kuwa serikali imesikia
kilio cha uongozi wa chuo hicho kwenye changamoto mbali mbali zikiwemo
za ukarabati wa majengo,kunakotokana na kutopata udhamini wa serikali na
kuahidi kulishughulikia suala hilo na mengine ikiwemo pia suala za Oc
za wafanyakazi kuwa endelevu na kupatikana.
Alisema kuwa taifa linategemea
wataalamu wanaozalishwa katika chuo hicho katika kuhakikisha linajiletea
maendeleo huku akitanabaisha kuwa utoaji wa elimu ya ujasiriamali
chuoni hapo Serikali itasaidia ikitambua ni eneo muhimu kwa ukuaji wa
kiuchumi kwa wananchi .
“Serikali itakaa pamoja na Bodi ya
chuo kuhakikisha changamoto mbali mbali zinapatiwa Ufumbuzi na kuwa
inatambua ongezeko la udahili linaenda na changamoto mbali mbali
hususani kukarabati majengo ya chuo hicho”alisema Balozi Idd.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi
ya chuo hicho prof.Methwer Luhanga alisema kuwa Ongezeko la udahili
haliendani na uongezaji wa miundombinu ya chuo hivyo akaiomba serikali
kuipatia udhamini chuo hicho ilikuweza kukarabati miundo mbinu yake
kwani chuo kinauwezo wakulipa mikopo hiyo tena kwa wakati.
Luhanga alisema kuwa chuo kimepata
mafaniko kwa kuongeza stashada tangia kilipoanzisha kutoka moja hadi
kufikia tano na kuwa wapo mbioni kuanzisha stashahada ya TEHAMA mwakani
ikiwa ni pamoja na kuongeza wakufunzi zaidi wenye shahada za uzamili na
uzamivu kwani hapo awali hakukuwa na wakufunzi wenye kiwango hicho.
“Kupata dhamana ya Serikali ndio
tatizo la kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali za chuo chetu
hivyo tunakuomba utuwasilishie kadhia hiyo”aslisema Prof Luhanga
Nae Mkuu wa Chuo hicho Emanuel
Mjema alisema kuwa chuo hicho kilichanzishwa mwaka 1965 na wanafunzi 25
na kimepiga hatua na kimeweza kudahili wanafunzi elfu 14 hivi sasa
kikiweza kutoa kuanzia Astashahada hadi digrii ya uzamivu haya ni
mafanikio makubwa kwa kipindi cha mika hamsini tofauti na hapo
kilipoanzishwa kikitoa wanafunzi cheti tu
Alisema kuwa chuo hicho kimeweka
mikakati ya kutoa elimu bora itakayowasaidia wanafunzi wa chuo hicho
kuendana Miataala ya soko la kimataifa itakayosaidia wahitimu kuzitumia
fursa zilizopo hapa nchini tena kwa weledi.
Alisema kuwa chuo hicho kwa sasa
kinatoa kozi ya shahada ya Mizani na vipimo ambapo ni chuo pekee kwa
nchini za kusini jangwa kutoa somo hilo na kuwa wapo mbioni kutoa somo
la Tehama chuoni hapo baadae mwaka huu,
No comments:
Post a Comment