Meneja
wa Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo kuhusu
masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri wa
Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika
katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokeavifaa vya
kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na
Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous jana
Maelezo kuhusu masalia ya injini hiyo ya moshi iliyoachwa na wajerumani Benson Kibonge
Waziri
Nyalandu akitembela maeneo mbalimbali ya mbuga hiyo ya Selous kabla ya
kukabidhiwa vifaa hivyo ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya
wanyama ya Selous leo. anayemuongoza na Meneja wa mbuga hiyo
Waziri
Nyalandu akisalimiana na Ofisa Mawasiliano na Umma wa Ubalozi wa
Marekani nchini Tanzania, David Feloemann, alipowasili kwenye mbuga ya
Selous jana
Mkurugenzi wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye alialikwa kwenye hafla hiyo, akitazama mto Ruaha unaopita katika mbuga ya Selous |
Balozi
wa Marekani nchini, Mark Childress akizungumza kabla ya kutiliana saini
na Nyalandu mkataba ya kukabidhiana vifaa hivyo. Kushoto ni Balozi wa
Ujerumani Egon Kochanke
Balozi
wa Marekani Mark Childress na Waziri wa Maliasili na Utalii wa
Tanzania, Lazaro Nyalandu wakitiliana saini mkataba wa Marekani kuipa
Tanzania msaada wa mafunzo yakiwemo ya kikomandoo kwa askari wa
wanyamapori na vifaa vya kisasa vya kukabiliana na ujangili katika mbuga
ya wanyamapori ya Selous jana.
Waziri Nyalandu akibadilishana hati na Balozi wa Marekani, Mark
Childress baada ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani
Egon Kochanke
Waziri Nyalandu akibalidilishana hati na Balozi wa Ujerumani Tanzania
Egon Kochanke, baada ya kutiliana saini mkataba wa ujerumani kuipa
Tanzania msaada wa vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majangili katika
mbuga ya wanyama ya Selous jana
Waziri
Nyalandu akimshukuru balozi huyo wa Ujerumani baada ya kubadilishana
hati walizosaini. kulia ni Balozi wa Marekani Tanzania Mark Childress
Waziri Nyalandu akitoa maelezo baada ya kutiliana saini na mabalozi wa Marekani na Ujerumani
Vifaa
mbalimbali vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na
Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika mbuga ya
wanyamapori ya Selous
Askari
wa Wanyamapori Anita Albert akijaribu kionambali ambacho ni miongoni
vya vifaa vilivyotolewa kwa Tanzania na Seriali za Marekani na Ujerumani
kwa ajili ya kukabiliana na ujangili
Askari
wa wanyamapori wakikagua mahema ambayo ni miongoni mwa vifaa vya kisasa
vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya
kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous. Picha
zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment