Waziri wa nchi Ofisi ya Mkamu wa
pili wa Rais Fatuma Abdullhabibi Fereji amesema kuwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzbar imekuwa ikizisaidia nyumba za kurekebisha tabia
(Sober house) kwa kuzipatia ruzuku ya fedha kila mwaka ya kuendesha
nyumba hizo ili kuona vijana wao wanabadilika kitabia.
Hayo ameyasema leo huko Baraza la
Wakilishi Zanzibar wakati akijibu suali la Mjumbe wa Wawi Saleh Nassor
Juma alietaka kujua kama Serikali inajua kuwepo kwa nyumba za
kurekebisha tabia kwa miongozo ya dini ya kiislamu na vipi Serikali
inazisaidia nyumba hizo.
Fatma Ferej alisema kuwa Serikali
inajua kuwepo kwa nyumba hizo na wanazipatia ruzuku ijapo kuwa kwa
kiwango kidogo kulingana na bajeti inayopatikana.
Alisema uendeshaji wa nyumba hizo
hufuatia hatua kumi na mbili za kiislamu ambapo hutambulika kuwa ni
“Milat Islam”na hatua hizo zimeletwa hapa Zanzibar kuazia mwaka 2009
baada ya wafanyakazi wa tatu wa na kijana mmoja aliepata nafuu baada ya
kupata mafunzo huko Marekani.
Waziri huyo aliziomba Taasisi za
kiislamu kuzitembelea nyumba hizo kwa kutoa michango yao na daawa
itakazowapelekea vijana wanaoishi nyumba hizo kujitambua na kubadili
tabia
Alisema vijana hao wanahitaji kila
aina ya huduma kwani ni watoto wao ambao walijiingiza katika tabia
zisizo nzuri, hivyo kuwasaidia na kuwaelimisha ni kulijengea taifa
mstakabali mwema wa vijana hao..
Alisema kuna baadhi ya wazzee
kuwatupa watoto hao na kuwazarau kwa vile walitumbukia katika janga
baya, lakini alisema kufanya hivyo ni kosa na jambo linalohitajika ni
ushiriiano wa pamoja kati ya wananchi, Serikali na Taasisi nyengine
wakiwemo wakilishi na wabunge.
No comments:
Post a Comment