Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Ntibenda
ameamua kutoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu huria cha
Arusha baada ya kutoridhishwa na majngo ya chuo hicho na kudai kuwa
hayana hadhi ya chuo hicho na kuwa yanaonekana kama nyumba ya mtumishi
wa serikali kuishi.
Pia mkuu huyo ametoa siku 30 kwa
Afisa Ardhi wa mkoa huo kutafuata kiwanja kwa ajili ya kuanza ujenzi
rasmi wa chuo ambacho kitakuwa na hadhi ya kuitwa chuo Kikuu.
Aliyasema hayo wakati alipofanya
ziara ya kukitembelea na kuonana na wafanyakazi na kufanya nao maongezi
pamoja na wahitimu wa chuo hicho kwenye mahafali ya 26 chuo hapa jijini
hapa.
Ntibenda alisema kuwa majengo hayo ya chuo yamemsikitisha kiasi
cha kutoa machozi hali ambayo inatakiwa kupatiwa ufumbuzi ndani ya mwezi
mmoja ilikuongeza umaridadi wa elimu inayotolewa chuoni hapo.
“Kweli kabisa mimi kama mkuu wa
mkoa ambaye raisi ameniona nafaa kuongoza mkoa huu sintakubali kuona eti
wanafunzi hata kama ni wa vyuo huria wanasoma katika majengo kama haya
badala yake nitahakikisha kuwa wanahama hapa na mnapata majengo mazuri
na ni haki yenu ninyi wanafunzi”aliongeza Ntibenda
Alifafanua kuwa chuo hicho hasa
masomo huria kinapokuwa na majengo mazuri kinasaidia wanafunzi kuweza
kupata hamasa kubwa katika masomo lakini kinapokuwa na majengo ambayo
hayana hadhi ya chuo basi hayapendezi wala kuvutia katika mazingira ya
masomo.
“Pamoja na kuwa mmesoma na matokeo
yenu ni mazuri sana tena ya kupigiwa mfano mimi nasema bado
kunauwezekano wa kufanya chuo hichi kikawa bora ni kwamba sote sisi
tukiungana na tuwe kimoja”aliongeza Ntibenda
Katika hatua Nyingine katibu wa
chama cha wanafunzi wa chuo kikuu huria Kasimu Mfinanga alisema kuwa
mapendekezo ya chuo hicho ni pamoja na kusogeza huduma ya elimu karibu
zaidi na wananchi hasa wale wa vijini lakini hata kwenye Wilaya Zote.
Mfinanga alimaliza kwa kusema kuwa mapendekezo mengine ni pamoja
na kuendelea kuelimisha jamii umuhimu wa kujiunga nacho kwani amendeleo
thabiti hayapatikani bila ya kuwa na elimu.
No comments:
Post a Comment