KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,
MALIASILI NA MAZINGIRA IMEAGIZA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAKAZI PAMOJA
NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ZIKAE NA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI
ULIYOPO KWENYE HIFADHI YA TAIFA YA SAADANI
MAAGIZO HAYO YA KAMATI
YAMETOLEWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM NA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO
MBUNGE WA KAHAMA MHESHIMIWA JAMES LEMBELI.
KABLA YA KAMATI KUTOA MAAGIZO
KWA WIZARA HIZO,KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII DOKTA
ADELHELM MERU AMEIELEZA KAMATI KWAMBA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA ILITENGA ENEO HILO KUWA SEHEMU YA HIFADHI YA TAIFA YA SAADANI.
AMESEMA KATIBU HAPO AWALI ENEO
HILO LILIKUWA NI SHAMBA LA MIFUGO LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
AMBAPO NDANI YA MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI ZOTE ZIKAKUBALIANA KUTENGA
ENEO HILO KUWA HIFADHI YA AKIBA HADI MWAKA 2005 NDIPO ILIPOTANGAZWA
RASMI KUWA HIFADHI KAMILI.
NAYE KATIBU MKUU WA WIZARA YA
ARDHI BWANA ALPHAYOL HIDATA AMESEMA WIZARA YAKE HAPOAWALI HAIKUWA NA
TAARIFA ZA KUWA ENEO HILO LIMETENGWA KWA AJILI YA HIFADHI NA NDIPO
WAKAMMILIKISHA MWEKEZAJI KWA AJILI YA KILIMO CHA MIWA
No comments:
Post a Comment